Msaada: Nina Millioni 10 itatosha kujenga nyumba?

Msaada: Nina Millioni 10 itatosha kujenga nyumba?

Yaaan wabongo kwa wivuu asee

Hiyo hela mbona nyingi asee, we jenga kanyumba ka kawaida ka vyumba vitatu choo, bafu inatosha kabisa
 
Afu chini afunge matairi ya trekta,asee ni ubunifu mkuu maana si Tanesco wala Dawasco(kama Dar) wataenda kudai bili zao,lazima wasahau tu wakidhani ni Gari LA mizigo[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Hahaha haha hahha Ebu toa ushauri acha masihara mkuu.
 
we anza kujenga sio pesa ila wito.
mimi nilianza ujenzi nikiwa na kiasi kidogo sana cha pesa nikajenga msingi na nikapandisha kozi nne nikakaa miaka minne ndipo nikaendelea lakini kwa sababu siko dar vinginevyo ningeshahamia.
pia babu yang baada ya kusumbuliwa na kodi mjini aliamia nyumba imejengwa upande ndo maana nakwambia we anza fedha zingine zitakuja wakati ukiendelea.
Kweli kabisa kama ana kiwanja we weka msingi wa mkubwa afu pandisha hata chumba mbili ulihamia utaona aibu na unalizia chap
 
Hiyo hela ni ndogo sana, huwezi kujenga nyumba labda kama unajenga kijijini. Ushauri wangu endelea kupiga vibarua uongeze zaidi, ila sasa hizo milioni kumi ulizo nazo anza ujenzi usikae nazo unaweza kuzitumia kunyume na matumizi ya ujenzi.
Huo ni ushauri mzuri. Ujanja ni kuanza kujenga kwa kiasi chochote ulichonacho!! Hapo utakuwa umepata mahali pa kuelekeza pesa zako utakazokuwa unapata. Tafuta ramani ambayo unaweza kuijenga kwa awamu. Unaweza kuinua chumba na sebule halafu ukahamia huku ujenzi unaendelea! Wanaosubiri wapate pesa nyingi ndio waanze kujenga huwa wanafia kwenye nyumba za kupanga!!
 
N
Madirisha,grills,vyoo/bafu,mashimo ya maji taka,plumbing na fundi wake,umeme na vifaa vyake na fundi wake,gypsum na ufundi wake,tiles,makabati ya jikoni. Hebu nipe gharama ya hivi vitu maanake wengi mnaweka gharama ya boma ambayo kwenye ujenzi ndio kitu rahisi. Nyumba nyingi zinakwama kwenye finishing. Kama mnazungumzia boma 10m inatosha.
Nyumba ni boma kwanza na kwenye boma mtu anaishi bila shida ili mradi maji na umeme uingie. Mambo mengine ya finishing taratibu!!!
Nilijenga nyumba yangu ya vyumba 4 vikubwa, sebule kubwa, dinning, jiko na car park nikaweza kuhamia. Baada ya miaka 4 nimeweza kufanya finishing kwa asilimia 75!!. Nilihamia kwenye rough floor nikaweka carpet, nikaweka maji na umeme maisha yakaendelea. Ningesubiri nipate pesa nyingi kwanza leo hii ningekuwa bado napanga!!
 
watu mna dharau, utadhani huku mitaani tunakoishi hizi nyumba tulizopanga ni za milioni 100.


ukitazama comment za humu utadhani sote tunaishi marekani.

hahahahhaa.

10M sio pesa ya kubeza.
Watu wanadharau sana,,hyo pesa inatosha hasa ukiwa tayali na kiwanja,,

Ukifata comment za humu unaweza potea kabsa
 
Inayotosha ni ngapi? Watu wamezeeka bila kujenga kwa sababu kila wakipata pesa wanaona kuwa hazitoshi hivyo kuishia kuchangia vikao vya harisi na send off na kununua vigari "baby seater" (IST, VITS, etc) na kununua simu kubwa huku wakijiunga kwa jero!!!!
Hahahah!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom