Msaada namna ya kupambana na Nyoka, naanza kuchoka

Ramon Abbas

JF-Expert Member
May 4, 2021
1,997
2,000
Hii nikiendelea kuviua siwezi kuisababishia hasara serikali?? Kwa kuua nyara za serikali?
Mazingira ya nje ni masafi?

hakikisha environmental cleanliness all the time

kisha fuga paka wa kuzuga zuga awe kama alarm siku kikinuka aanze kufa yeye kwa mpambano mkali na cobra.

Hao ni akina Junior wanatumwa kuja ku survey mazingira yakoje, One day atakuja baba lao yule King Cobra.

Otherwise niseme pole kwa hili sanga
 
jkipaji

JF-Expert Member
Sep 22, 2019
2,080
2,000
Hiyo itakuwa michezo ya baba mwenye nyumba kutaka kukupima kama uko fit. Kama hujang'atwa na hawa nyoka mpaka sasa basi uko fit, we endelea tu kula watoto wa watu huko.
Kuna Demu aliniambia kaachika,lakini kila nikienda kumgonga nikufudi home tu usiku nikiwasha tu taa lazima nikutane na nyoka wadogo wawili,mmoja anakua anatembea zake varandani kuelekea chumbani,na mwingine namkuta tahari yuko chumbani karibu na Kitanda! Ilinitokea Kama Mara tatu hivi, nikaamua kumtema yule Demu kimyakimya bila yeye kujua!! Duniani kuna mengi,sema tu Mungu anatulinda sana!!
 
Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,460
2,000
Paka ndiyo kiboko yake.

Kama mahali ulipo kuna mtu kutoka KAGERA yaani mwenyeji wa BUKOBA muulize kama anaujua mti unaitwa MWIITANJOKA au OMWIITANJOKA.

Kama anaujua akuonyeshe uchume vimiti na majani yake, Kisha tia jikoni viwake/viungue utapata matokeo.

Nyoka huwa hapendi harufu ya mti huo anauogopa sana. Watahama wote.
Katika kuhama ndipo unawapa taharuki unaweza wakuta ndani ya net
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
7,411
2,000
Haujagundua sehemu wanapoingilia?

Hicho choo kimekaaje, kina mfuniko?

Wanapenda kutembea sana kwenye mabomba ya maji taka na kuibukia chooni.

Hawaji kimiujiza, lazima kuna udhaifu pahali kwenye mjengo ndipo huingilia.

Zama tena kwenye uchunguzi na udhibiti wa mianya.
 
pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,706
2,000
Haujasema upo mkoa gani na eneo lako lipoje umezungukwa na mazingira gani utuonyeshe.....

Ila fanya hivi tafuta lile gallon la lita 5 lijaze oil chafu, kisha nunua mafuta ya taa lita tatu na nusu pakti ya chumvi ya unga, changanya halafu tikisa vichanganyike vema.

Baada ya hapo tafuta chupa ya maji ya kunywa hizi kama za uhai, itiboe kuweka tundu kisha kuwa unamiminia huo mchanganyiko na utumie hiyo chupa kunyunyiza eneo la kuzunguka nyuma unayoishi.

Unaweza kuogeza kipimo hata ndoo kubwa ya oil chafu ukapata na lita tano za mafuta ya taa na pakti nzima ya chumvi ya unga,kisha ukachanganya halafu ukamwaga eneo lote kwa maana ya vichaka, maficho, mashimo, eneo lenye makorokoro yaliyorundikwa.

Hiyo harufu nyoka kama wapo hapo watatoka ndani ya dakika kadhaa tu na pia kama wapo nje ya eneo hilo hawatasogea au watakimbia mbali na hapo.

Na ikitokea huo mchanganyiko ukamwagia nyoka direct aisee ni kitendo cha dakika kadhaa atachanika chanika ngozi yake utamuonea huruma anavyokufa kifo cha mateso na kukauka.
Huu mchanganyiko wako pia ni dawa ya mchwa!
Nimetumia Sana kutibu mchwa ni kiboko aisee,kumbe hata nyoka wanakufa kupitia mchanganyiko huu?
Katika huo mchanganyiko niliongezea na sabuni ya unga pakiti moja
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
18,871
2,000
Bro hao nyoka hawana madhara kbs wala hawaumi.NI BROWN HOUSE SNAKE..
Wanakusaidia kupunguza pest kama panya au wadudu wengine.
Hawana sumu kabisa bali ni constrictors(wanambana panya pumzi)kisha kummeza.

Uwe na amani kabisa...
Kirahisi rahisi hivi tukuamini. Ha ha ha haaa!
 
mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
5,542
2,000
Kuna Demu aliniambia kaachika,lakini kila nikienda kumgonga nikufudi home tu usiku nikiwasha tu taa lazima nikutane na nyoka wadogo wawili,mmoja anakua anatembea zake varandani kuelekea chumbani,na mwingine namkuta tahari yuko chumbani karibu na Kitanda! Ilinitokea Kama Mara tatu hivi, nikaamua kumtema yule Demu kimyakimya bila yeye kujua!! Duniani kuna mengi,sema tu Mungu anatulinda sana!!
Basi huyo demu kategwa na X wake ila hajijuwi tu
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,466
2,000
Paka ndiyo kiboko yake.

Kama mahali ulipo kuna mtu kutoka KAGERA yaani mwenyeji wa BUKOBA muulize kama anaujua mti unaitwa MWIITANJOKA au OMWIITANJOKA.

Kama anaujua akuonyeshe uchume vimiti na majani yake, Kisha tia jikoni viwake/viungue utapata matokeo.

Nyoka huwa hapendi harufu ya mti huo anauogopa sana. Watahama wote.
Dada, sasa hili ni Geto la Bachelor. Yaani huwa naishi kwa week au week mbili kasoro kisha naondoka. Sipiki wala sija jiko. Shukrani sana
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,466
2,000
Haujasema upo mkoa gani na eneo lako lipoje umezungukwa na mazingira gani utuonyeshe.....
Nipo Kigoma, Wilaya mojawapo nje kidogo ya Mji, maeneo nje ni masafi maana watu wamelima mashamba kwa ajili ya kulima.

Ni pasafi Ila pia nyumba iko U-Shaped na Mimi room ninayoishi iko huku makalioni, kwahio kwamba nyoka ameingilia getini, kisha akaacha mlango wa kwanza hadi wake huku kwangu, napata tabu kisogo maana getini had I mlangoni kwangu so chini ya mita sita au nane
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,466
2,000
Hiyo itakuwa michezo ya baba mwenye nyumba kutaka kukupima kama uko fit. Kama hujang'atwa na hawa nyoka mpaka sasa basi uko fit, we endelea tu kula watoto wa watu huko.
Haahhaahah sijawahi aiseeee hata kuwaza! Nikija huku nakua na very limited time! Najikuta hats kunywa nanywea room
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,466
2,000
Kuna Demu aliniambia kaachika,lakini kila nikienda kumgonga nikufudi home tu usiku nikiwasha tu taa lazima nikutane na nyoka wadogo wawili,mmoja anakua anatembea zake varandani kuelekea chumbani,na mwingine namkuta tahari yuko chumbani karibu na Kitanda! Ilinitokea Kama Mara tatu hivi, nikaamua kumtema yule Demu kimyakimya bila yeye kujua!! Duniani kuna mengi,sema tu Mungu anatulinda sana!!
Duh pole sana aiseeee! Tuache mademu was kuokota hovyo hovyo
 
Townchild

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,548
2,000
Waungwana eeegh hawa nyoka naelekea kuanza kuchoka.

Hii ni Mara ya pili sasa naua nyoka chumbani kwangu. Nimejaribu kuangalia ni wapi wanaweza kuwa wanapitia kwa kweli sijaona!

Niko Mkoani, kwahio niliamua kupanga chumba ili kupunguza gharama za Lodge kila mara maana huwa nakaa week au week mbili.

Hii nyumba niliyopanga ni mpya, mlangoni kwenye chumba changu nimepana na dekio la taulo ili kuzuia vumbi, chooni sioni possibility ya kupitia huko!

Dirishani ambapo ndipo kitanda kilipo huwa nafungua dirisha ila Kuna Mosquito net, je Nyoka anaweza kupanda ukuta aingie ndani? Maana nawakuta jirani tu na kitanda.

Haka ka Leo kalikua chini ya kiti, yaani wakati Niko kwa laptop nafanya kazi kumbe huyu mpuuzi yuko chini ya kiti.

Anyway, nisaidieni namna ya kuwamaliza kabisa, waache ujinga wao wa kuibuka usiku.

Wamenikata stimu kabisa, halafu wakati nakaua ghafla Tanesco wakakata umeme! Ila ukarudi faster......

Nje mazingira ni masafi maana ni mashamba, majirani zangu hawaja experience kiti kama hiki!

Ila Mimi nndio ishanitokea twice. Nipeni Dawa Wakulungwa.

View attachment 1986903
Kwani wewe hutaki wageni😂.
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,466
2,000
Njoo kwenye maombi mkuu hapo unatafutwa na ibilisi
Huyo Ibilisi ameshashindwa big time mwanangu, Mimi chumba changu ndio chumba changu cha ibada.

Mwaka juzi nilikua na shughuli kama hizi huko Njombe nika-opt kupanga geto kupunguza tena gharama za kuishi Guest. Basi Bibi nwenye nyunba alikua kigego balaa ila kwangu ali-blow.

Aliniweza Mara mbili tu, Siku moja nadhani sikusali vizuri halafu nikawa nimekunywa tu-Image tuwili au tatu hivi. Basi unaambiwa SAA kumi usiku nastuka nagusa maji maji kwenye MTO kama vile umande umedondokea MTO! Ila geto lilikua LA ceiling board sasa, nikajua labda nimedondosha udenda nikajichunguza nikakuta hapana ila kabla ya kile kitendo kutokea kulikua na mazingira Fulani hivi, Basi nikahitimisha tu kuwa nilikua na Wageni...

Mara ya pili nilikua namkabidhi room yake na kumuaga, kwahio nikapaki vitu vyangu maana Siku ile ndio nilikua nimefika Njombe, nikajishauri sana nilale Lodge ila nikaamua kulala geto ili niwaage kabisa, chumba kilikua nyumba ya main house....Basi unaambiwa ile asubuhi mida ya SAA kumi hivi, nilimuona Live kabisa yule Bibi. Anyway ndio maisha ya utafutaji
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom