Msaada namna ya kupambana na Nyoka, naanza kuchoka

blackcornshman

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
5,188
2,000
Kuna mti flani upo eswatini,kuna manyoka mengi kila kona kule ndiyo wanaoteshaga nyoka wanatimua nikipata jina lake ntaweka.
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,525
2,000
Maji ya upako ni kiboko ya mwamposa hutajutia fungulia chanel iitwayo arise and shine kila saa3 u fatisha maelekezo utaona maajabu
Mie nasikiliza Radio Upendo FM Evening and Morning Glory na kuna Online Radio inaitwa Mungu Kwanza! Nadhani ndio maana hawa nyoka wanakimbia. Huyu wa Jana nimemkata jicho hadi akaona aibu akashindwa hata kusogea! Maombi yana Nguvu sana Ndugu zangu. Kumwamini Mungu Ni raha sana
 
Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,823
2,000
Katika kuhama ndipo unawapa taharuki unaweza wakuta ndani ya net
Unachoma ukiwa ndani, Wao watakimbia kama walikuwa ndani wataelekea mbali na nyumba yako.

Hata kama walikuwa kwenye mashimo watatoka, watakimbia kuelekea mbali wakiimbia harufu ya moshi ya majani ya MWIITANJOKA.

Majani ya mti huu wa MWIITANJOKA yanafanya kazi kama TAIRI LA BAISKELI au LA GARI au ya MAPIRA ama zile PIRA zinazofunga mzingo kwenye BAISKELI, Nazo ukizichoma ile harufu yake NYOKA hapatani nayo anakimbia mbali na mji wako.
 
MTAU JR

Senior Member
Aug 29, 2021
144
250
Haujasema upo mkoa gani na eneo lako lipoje umezungukwa na mazingira gani utuonyeshe.....

Ila fanya hivi tafuta lile gallon la lita 5 lijaze oil chafu, kisha nunua mafuta ya taa lita tatu na nusu pakti ya chumvi ya unga, changanya halafu tikisa vichanganyike vema.

Baada ya hapo tafuta chupa ya maji ya kunywa hizi kama za uhai, itiboe kuweka tundu kisha kuwa unamiminia huo mchanganyiko na utumie hiyo chupa kunyunyiza eneo la kuzunguka nyuma unayoishi.

Unaweza kuogeza kipimo hata ndoo kubwa ya oil chafu ukapata na lita tano za mafuta ya taa na pakti nzima ya chumvi ya unga,kisha ukachanganya halafu ukamwaga eneo lote kwa maana ya vichaka, maficho, mashimo, eneo lenye makorokoro yaliyorundikwa.

Hiyo harufu nyoka kama wapo hapo watatoka ndani ya dakika kadhaa tu na pia kama wapo nje ya eneo hilo hawatasogea au watakimbia mbali na hapo.

Na ikitokea huo mchanganyiko ukamwagia nyoka direct aisee ni kitendo cha dakika kadhaa atachanika chanika ngozi yake utamuonea huruma anavyokufa kifo cha mateso na kukauka.
Umetisha mze baba nlisha wahi sikia iyo ishu kitambo
 
HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
29,985
2,000
Ugomvi wako na nyoka ulianzaje mkuu?

Give us a short story, inaonekana iko interesting maana nyoka hana nafasi tena moyoni mwako
Kwa bahati nzuri sijawahi kuishi kwenye mazingira yenye Nyoka, imetokea tu kwa upande wangu kuwa tofauti kabisa na Nyoka.

Siwapendi Nyoka.

Nawaogopa sana Nyoka
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,538
2,000
Nyoka wanaingia mlangoni, hasa kwa milango ambayo imeachia nafasi kwenye sakafu. Tafuta oil chafu kama lita moja au mbili toka garage. Changanya na mchanga na kisha zungushia nyumba yote kwa nje umbali wa 0.5m toka ukutani. Rudia zoezi hili kila baada ya miezi 3.
bora ungemshauri amwage pilipili mlangoni
 
Kirumberumbe

JF-Expert Member
Mar 28, 2017
430
500
Bro hao nyoka hawana madhara kbs wala hawaumi. NI BROWN HOUSE SNAKE.

Wanakusaidia kupunguza pest kama panya au wadudu wengine.

Hawana sumu kabisa bali ni constrictors (wanambana panya pumzi)kisha kummeza.

Uwe na amani kabisa.
Mkuu; Wanauma (wakichokozwa/wakibughudhiwa) ila hawana sumu. Ni vyema kuchukua tahadhari kwani akikuuma yapo madhara mengine e.g. jeraha, wasiwasi/hofu, n.k.
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,538
2,000
Waungwana eeegh hawa nyoka naelekea kuanza kuchoka.

Hii ni Mara ya pili sasa naua nyoka chumbani kwangu. Nimejaribu kuangalia ni wapi wanaweza kuwa wanapitia kwa kweli sijaona.

Niko Mkoani, kwahiyo niliamua kupanga chumba ili kupunguza gharama za Lodge kila mara maana huwa nakaa week au week mbili.

Hii nyumba niliyopanga ni mpya, mlangoni kwenye chumba changu nimepanga na dekio la taulo ili kuzuia vumbi, chooni sioni possibility ya kupitia huko!

Dirishani ambapo ndipo kitanda kilipo huwa nafungua dirisha ila Kuna Mosquito net, je Nyoka anaweza kupanda ukuta aingie ndani? Maana nawakuta jirani tu na kitanda.

Haka ka Leo kalikua chini ya kiti, yaani wakati Niko kwa laptop nafanya kazi kumbe huyu mpuuzi yuko chini ya kiti.

Anyway, nisaidieni namna ya kuwamaliza kabisa, waache ujinga wao wa kuibuka usiku.

Wamenikata stimu kabisa, halafu wakati nakaua ghafla Tanesco wakakata umeme! Ila ukarudi faster.

Nje mazingira ni masafi maana ni mashamba, majirani zangu hawaja experience kiti kama hiki!

Ila Mimi nndio ishanitokea twice. Nipeni Dawa Wakulungwa.

jacobcm8

Senior Member
Apr 10, 2014
160

Nunua peTrol lita ata 1.5 kisha weka kwenye kopo la maji yakunywa toboa hapo Juu kwenye kizibo. Petrol iwe inatoka mdo mdo faida kuu 3 utapata…. 1.hutakaa uone hao viumbe 2. Utakuwa unaamka ukiwa high 3. Geto litakuwa na manukato…….
 
am 4 real

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
699
1,000
Hili tukio litabakia akilini mwangu....
Nikiwa nahamisha kitanda chumbani kwa baba angu.... Upande wanao lazia vichwa nikakuta kuna nyoka mkubwa mweusi...nikamuwai kumuua.

Cha kujiuliza nyoka alifikaje fikaje na je? akikungata Usiku....du ni mambo ya kuogofya sanaa
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,538
2,000
Waungwana eeegh hawa nyoka naelekea kuanza kuchoka.

Hii ni Mara ya pili sasa naua nyoka chumbani kwangu. Nimejaribu kuangalia ni wapi wanaweza kuwa wanapitia kwa kweli sijaona.

Niko Mkoani, kwahiyo niliamua kupanga chumba ili kupunguza gharama za Lodge kila mara maana huwa nakaa week au week mbili.

Hii nyumba niliyopanga ni mpya, mlangoni kwenye chumba changu nimepanga na dekio la taulo ili kuzuia vumbi, chooni sioni possibility ya kupitia huko!

Dirishani ambapo ndipo kitanda kilipo huwa nafungua dirisha ila Kuna Mosquito net, je Nyoka anaweza kupanda ukuta aingie ndani? Maana nawakuta jirani tu na kitanda.

Haka ka Leo kalikua chini ya kiti, yaani wakati Niko kwa laptop nafanya kazi kumbe huyu mpuuzi yuko chini ya kiti.

Anyway, nisaidieni namna ya kuwamaliza kabisa, waache ujinga wao wa kuibuka usiku.

Wamenikata stimu kabisa, halafu wakati nakaua ghafla Tanesco wakakata umeme! Ila ukarudi faster.

Nje mazingira ni masafi maana ni mashamba, majirani zangu hawaja experience kiti kama hiki!

Ila Mimi nndio ishanitokea twice. Nipeni Dawa Wakulungwa.

Huu ni msimu wao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom