Msaada namna ya kupambana na Nyoka, naanza kuchoka

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
44,575
2,000
Waungwana eeegh hawa nyoka naelekea kuanza kuchoka.

Hii ni Mara ya pili sasa naua nyoka chumbani kwangu. Nimejaribu kuangalia ni wapi wanaweza kuwa wanapitia kwa kweli sijaona.

Niko Mkoani, kwahiyo niliamua kupanga chumba ili kupunguza gharama za Lodge kila mara maana huwa nakaa week au week mbili.

Hii nyumba niliyopanga ni mpya, mlangoni kwenye chumba changu nimepanga na dekio la taulo ili kuzuia vumbi, chooni sioni possibility ya kupitia huko!

Dirishani ambapo ndipo kitanda kilipo huwa nafungua dirisha ila Kuna Mosquito net, je Nyoka anaweza kupanda ukuta aingie ndani? Maana nawakuta jirani tu na kitanda.

Haka ka Leo kalikua chini ya kiti, yaani wakati Niko kwa laptop nafanya kazi kumbe huyu mpuuzi yuko chini ya kiti.

Anyway, nisaidieni namna ya kuwamaliza kabisa, waache ujinga wao wa kuibuka usiku.

Wamenikata stimu kabisa, halafu wakati nakaua ghafla Tanesco wakakata umeme! Ila ukarudi faster.

Nje mazingira ni masafi maana ni mashamba, majirani zangu hawaja experience kiti kama hiki!

Ila Mimi nndio ishanitokea twice. Nipeni Dawa Wakulungwa.

IMG_20211025_225935_617.jpg
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
44,575
2,000
Chemsha huyo nyoka, then bandua ngozi ya juu ukishamla kazi imeisha hiyo tena mtengeneze roast lakini umchane katikati utaona kautando keusi hako katoe, then mpige na dona yako safi uone mambo usiue wala kutupa mboga hiyo
Roast ya mchuzi? Na pilipili kwa mbali, sema wanakuja wadogo wadogo tu. Huyu nimemchoma akatoa kaharufu Fulani amazing sana
 

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,687
2,000
Paka ndiyo kiboko yake.

Kama mahali ulipo kuna mtu kutoka KAGERA yaani mwenyeji wa BUKOBA muulize kama anaujua mti unaitwa MWIITANJOKA au OMWIITANJOKA.

Kama anaujua akuonyeshe uchume vimiti na majani yake, Kisha tia jikoni viwake/viungue utapata matokeo.

Nyoka huwa hapendi harufu ya mti huo anauogopa sana. Watahama wote.
 

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
10,330
2,000
Haujasema upo mkoa gani na eneo lako lipoje umezungukwa na mazingira gani utuonyeshe.....

Ila fanya hivi tafuta lile gallon la lita 5 lijaze oil chafu, kisha nunua mafuta ya taa lita tatu na nusu pakti ya chumvi ya unga, changanya halafu tikisa vichanganyike vema.

Baada ya hapo tafuta chupa ya maji ya kunywa hizi kama za uhai, itiboe kuweka tundu kisha kuwa unamiminia huo mchanganyiko na utumie hiyo chupa kunyunyiza eneo la kuzunguka nyuma unayoishi.

Unaweza kuogeza kipimo hata ndoo kubwa ya oil chafu ukapata na lita tano za mafuta ya taa na pakti nzima ya chumvi ya unga,kisha ukachanganya halafu ukamwaga eneo lote kwa maana ya vichaka, maficho, mashimo, eneo lenye makorokoro yaliyorundikwa.

Hiyo harufu nyoka kama wapo hapo watatoka ndani ya dakika kadhaa tu na pia kama wapo nje ya eneo hilo hawatasogea au watakimbia mbali na hapo.

Na ikitokea huo mchanganyiko ukamwagia nyoka direct aisee ni kitendo cha dakika kadhaa atachanika chanika ngozi yake utamuonea huruma anavyokufa kifo cha mateso na kukauka.
 

mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
5,542
2,000
Waungwana eeegh hawa nyoka naelekea kuanza kuchoka.

Hii ni Mara ya pili sasa naua nyoka chumbani kwangu. Nimejaribu kuangalia ni wapi wanaweza kuwa wanapitia kwa kweli sijaona...
Hiyo itakuwa michezo ya baba mwenye nyumba kutaka kukupima kama uko fit. Kama hujang'atwa na hawa nyoka mpaka sasa basi uko fit, we endelea tu kula watoto wa watu huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom