sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Nipo natumia huduma hii tangu mwaka jana na msukumo wa kuja huku ilikuwa ni baada ya mitandao kupandisha bei za mabando, nadhani wote mnakumbuka mabando yalikuwa bei chee ila kuna wabongo hawakutosheka wakaanza kuyabipu makampuni ya simu kwamba vifurushi visiwe vina expire, Mb ni chache, n.k. ishu ikafika hadi wizarani ikawa ajenda kubwa, mitandao ikapiga na ndio ukawa mwanzo wa vifurushi kuuzwa bei kali, hakika huwezi jua thamani ya ulichonacho hadi kipotee!!
Ok back to the topic, Nipo na hawa tigo since last year na huu ndio mrejesho wangu.
Kupunguza gharama za internet - Kila mwez naungwa GB 80 kwa shilingi elf 60, hii ni sawa na shilingi 750 kwa kila GB, kwangu ni deal safi kabisa sijui kabisa mambo ya kuzima data,
kumekuwa na mabadiliko ya bei kwa wateja wapya lakini sisi wateja wa zamani hatuguswi na mabadiliko, kwa sasa wateja wapya bei zao hizi hapa, nao hawataguswa na mabadiliko yakija kufanyika.
Upigaji / Wizi - Kuna ule upigaji unakuta umejiunga gb 1 ila ukitumia MB 300 tu unaambiwa bando limeisha au unatumiwa sms kwamba umetumia 75%, Huku sijaona hicho kitu, Natumia router inayohesabu nimetumia gb ngapi, na nikiangalia salio kwenye mtandao kweli naona kuna uwiano. Mfano kwa hapa Kwenye router umetumija GB 2 na MB 207, kwenye salio la tigo inaonyesha zimebaki GB 77 na MB 793, kwa kifurushi changu cha GB 80 pana uwiano.
Speed - Mwanzoni speed nilikuwa napata changamoto nikitumia internet nyumbani nje kidogo ya mji tofauti na nikiwa ofisni sehemu za centre, yani nikifika home nlikuwa napata speed ndogo sana tena ikifika usiku ndio naweza kuzima kabisa, kipindi hiki nilikuwa natumia line yao kwenye simu yangu ya Samsung iliyokuwa na laini 2, Ndipo nilipokutana na kijana wetu wa IT ninapofanyia kazi akanishauri ninunue pocket router sababu ni kifaa maalum kwajili ya kukusanya mawimbi ya Net, Hio router ni 75,000 lakini niliingia group la facebook la mkoa nilipo nikapata iliyotumika kwa 20,000, niliongezea elf 10 ya mwanasheria kutuandalia mkataba wa kuuziana (mkataba unilinde endapo router ni ya wizi).
niliambiwa niiweke dirishani ila kwa speed ilipanda kidogo, kijana wa IT alikuja kunitafutia sehem yenye network zaidi, alichofanya alianza kudownload faili la Gb kwenye simu yake huku anatembea na router na kuipitisha maeneo kadhaa ya mle ndani, haoa alikuwa anacheki maeneo yenye speed kubwa, alipoiweka juu ya mlango speed ikafika MB 2 kwa sekunde, ndio sehemu nayotegesha router kila niwapo nyumbani.
Malipo - Kila Tarehe 1 inapofika bando linaingia , Napewa siku 9 za kukamilisha malipo kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 9.
Mobility - Niliwahi fikiria kufunga nyumbani fibre ya nguzo za ttcl elf 50 kwa mwezi unlimited, tatizo likawa ni mobility (utumiaji wa sehemu zaidi ya moja) ndipo paliponishinda, pia umeme ukikatika haitumiki, nguzo zikidondoka hakuna huduma, n.k. ni tofauti na post paid nabeba ki router changu sehemu yoyote napoenda hata nikiwa na drive.