Kwa mara Nyingine tena Nimechunguza uwiano wa bando nalolipia na matumizi halisi niliyotumia kwa mwezi, ungana nami katika matokeo ya Research

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Mtandao : TIGO

Bando / Kifurushi – Tigo Post-Paid 80 GB / Elf 60 Kila mwezi. (mawasiliano natumia mtandao mwengine kwasababu naitumia namba hio tangu 2006, naunga bando la elf 10 mitandao yote )

Kifaa nachotumia ni Router ya Tigo

Nipo Dsm, Mbezi Louis

Nimeanza kuhesabu from scratch (0 KB) kuanzia tarehe 1 saa sita kamili usiku kifurushi kipya kinapoingia hadi leo mwisho wa mwezi kilipofikia kikomo

Kiasi Nilichotumia kufikia kikomo = GB 77.3, salio linaonyesha kifurushi kimebaki MB 1

Kiasi chenye utata ni GB 2.7 (80 – 77.3) sawa na asilimia 3.4 %

Possibilities nazoziona

  • Huenda ni within margin of Error
  • Labda naongezewa matumizi (Napigwa) kwa asilimia 3.4%, kwa kila GB 1 kiuhalisia zinapunguzwa asilimia 3.4% sawa na MB 34 (GB 0.034), ama tuseme ya kwamba ni sadaka 😂
  • Labda tatizo lipo counter ya router inayohesabu matumizi,

My personal view
Wala si mbaya, sijaumia maana kuna mitandao nishawahi tumia, asilimia 20 hadi 50 inapotea kimiujiza, Nishawahi kutumia mtandao flani sio poa, hata sijaanza kutumia natumiwa meseji nimetumia asilimia 75%, sijakaa sawa nikapokea meseji inakuambia kifurushi kimekwisha.

Kwa hizo Gb 77 kwa siku 30 bado ninaweza kutumia GB 2 na nusu Daily, Possibilities zinaweza kuwa nyingi kwa matokeo niliyoyapata, siwezi kufanya conclusion haraka, kwa Research zaidi nitabadili router nitumie tofauti nione itakuwaje.

Sina dalili yoyote ya kuwahama Tigo, wanaupiga mwingi sana tu.

Research yangu ya kwanza hii >> hapa <<

Hii ni data Usage ya kwenye kioo cha Router
Img_20230831.jpg

Hii ni data Usage kwenye menu ya router
Screenshot_20230831-182939.png

Hii ni meseji ya salio lililobaki
Screenshot_20230831-182940.png
 
Sina maana umekosea ila mimi tu najiona sijaelewa
Oh , ok wacha nikueleweshe

Ni kwamba unaponunua kitu mfano kilo 1 ya unga unategemea iwe kilo moja, ukishanunua hio kilo ukienda nyumbani kuipima kwenye mzani ukiona zimepungua kilo 0.003 sio mbaya ila tu utakuwa na maswali kichwani na shauku ya kupata majibu kwanini isiwe kilo 1 kamili. huenda ni upepo umepuliza, huenda ni mitikisiko ya bajaji imefanya unga kidogo umwagike, huenda muuzaji kakupunja, huenda mzani ni mbovu, n.k.

Kwahio kwa Tigo nili tarajia kutumia GB 80 ila nimetumia GB 77.3 hapo ni kwamba 80- 77.3 jibu ni GB 2.7, kutafuta asilimi GB 2.7/ GB 80 * 100 = 3.375 %, kwa makadirio mepesi ni kama 3.4%
 
Oh , ok wacha nikueleweshe

Ni kwamba unaponunua kitu mfano kilo 1 ya unga unategemea iwe kilo moja, ukishanunua hio kilo ukienda nyumbani kuipima kwenye mzani ukiona zimepungua kilo 0.003 sio mbaya ila tu utakuwa na maswali kichwani na shauku ya kupata majibu kwanini isiwe kilo 1 kamili. huenda ni upepo umepuliza, huenda ni mitikisiko ya bajaji imefanya unga kidogo umwagike, huenda muuzaji kakupunja, huenda mzani ni mbovu, n.k.
Anhaaa sasa nimekuelewa.

Kwani hiyo usage uliipata kwa app iliyokuwa inapima matumizi au ulikuwa unaipima vipi?
 
Oh , ok wacha nikueleweshe

Ni kwamba unaponunua kitu mfano kilo 1 ya unga unategemea iwe kilo moja, ukishanunua hio kilo ukienda nyumbani kuipima kwenye mzani ukiona zimepungua kilo 0.003 sio mbaya ila tu utakuwa na maswali kichwani na shauku ya kupata majibu kwanini isiwe kilo 1 kamili. huenda ni upepo umepuliza, huenda ni mitikisiko ya bajaji imefanya unga kidogo umwagike, huenda muuzaji kakupunja, huenda mzani ni mbovu, n.k.
Okay nimeona kwenye router kupitia picha kumbe ilikuwa ina count matumizi
 
Hiyo ni sadaka... Achana nayo usiiwaze wala kudai.

Fikiria sisi tunaonunua GB 1.15 kwa Tsh 2500 kwa wiki lakini tunaitumia kwa siku 1
 
Hiyo ni sadaka... Achana nayo usiiwaze wala kudai.

Fikiria sisi tunaonunua GB 1.15 kwa Tsh 2500 kwa wiki lakini tunaitumia kwa siku 1
Tena kwa hizi simu za kisasa zinahitaji GB zisizo na mawazo maana kwa wenzetu huko zinakotengenezwa wao intenet zao hazinaga kikomo cha GB, shida inakuja kwetu, simu kali ila internet unapimiwa.
 
Mtandao : TIGO

Bando / Kifurushi – Tigo Post-Paid 80 GB / Elf 60 Kila mwezi.

Kifaa nachotumia ni Router ya Tigo...
Asante kwa taarifa mkuu. Nami nimechunguza nimeona mitandao yote ya simu ni wezi wa vifurushi lakini HALOTEL ni majizi ya kutupwa.

Ukiwa connected hata kama hutumii data yoyote wao wanahesabu tu. Yaani ni kama wanakata bando kwa kukisia. Kabla hata hujaanza kutumia unatumiwa meseji ya kufika 75%, mara hujakaa sawa unapokea meseji inakuambia kifurushi chako kimekwisha. Hawa wapuuzi ni majizi sana aisee.

Bora nami ninunue tu router ya tiGO isiwe taabu. Kuna siku nilienda dukani kwao wakaniambia zimeisha. Najiandaa kuhamia tiGO moja kwa moja niachane na haya majizi ya halotel.
 
Back
Top Bottom