Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

Inasikitisha sana kuona rais ambaye ni muisalam ambaye anashinda kutwa nzima amefunika kichwa chake huko China kuna kabila la Uyghurs ambalo wamesema ni haki yako kuabudi uislam wote wamekusanywa na kuwekwa kwenye concentration camp, shame on us!
Hela ndiyo zinaabudiwa kuliko hata imani raisi anayo shinda ana valia ushugi. Hawa ndiyo wawekezaji wa bagamoyo kwa muislam mwingine ambaye ni kama foreigner kwenye nchi yake anayezungukwa na watu masikini hohehahe wa kizaramo, elimu duni na afya mbili. …Magufuli alikuwa na inside informations za madudu yote ndiyo maana amekatishwa uhai wake na hicho ndiyo kisa kilichobaki mfikisha huko aliko
. Kinachofuatia ni kuwamaliza asikali watiifu wa Magufuli period, but time will tell.
Sikubaliani na jambo moja tu ulilotumia, la kuhusianisha uongozi na Imani ya mtu, hilo sikubaliani nalo, mimi naamini uongozi ni kipaji, na kipaji hakihusiani na Imani,

Ila umechangia bonge la hoja, natamani washauri wa Rais wawe wakweli wamshauri Vema mh Rais
 
Mikataba yote ambayo Kikwete alihusika ilijaa ufisadi wa hali ya juu hivyo bila shaka mkataba huo wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uligubikwa na ufisadi wa hali ya juu.
1624834372479.jpeg

Tunataka Miradi mingi katika taifa letu, Lakini tunataka miradi ambayo kiukweli italeta ukombozi wa maisha ya wananchi

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ni mradi mkubwa na unaumhimu wake, Lakini kwa nini usiwe wazi?

kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?

Kuanzisha mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuwepo uwazi wa mkataba uliotiliwa mashaka na viongozi mbalimbali wa nchi hii, ni uhujumu uchumi mkubwa na kuziua bandari zetu ambazo ni tegemeo kubwa la uchumi wetu

Hivi, Tanzania ni lini tutafahamu kwamba, uwingi wa miradi na sifa ya kuwepo wawekezaji wengi wasio na faida haituongezei chochote zaidi ya kutufanya tuwe taifa tegemezi na lisiloweza kujikomboa na umasikini..!

Kuwa na uwingi wa miradi haina maana kwamba umasikini ndiyo basi tena, Isipokuwa ni kuwa miradi yenye tija

Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu
 
Hivi mna matatizo gani lkn? Penda kufanya research ndo uje uandike hapa jukwaani. Unajitia aibu kwa huu mchango wakonwa chuki na ubinafsi hapa ujue. Acha kufata upepo. Mradi wa Bagamoyo una tija kwa Taifa. Hivi Ile chato airport haikusaidii?? Mbona mama alipoenda kigogo busisi hamkulalamika???
Huu ni mradi wa mchina? Ni wa miaka Mia moja ya umiliki? Huu ni mradi wako, hela ya kodi na lazima uidai kwa maendeleo ya Tanzania. Sasa wewe unaye sema tufanye research wewe umefanya ipi?
 
Mirandi kama bagamoyo hauna tatizo kama unavyofikiri maana muwekezaji anaweka hela zake mwenyewe.
Fitna za jpm ni kukosa 10% ktk huo mradi.
Anapenda aonekane yy ndo kafanya kila kitu ndo maana anasifia mloganzira na viwanda vya pwani eti ni yeye ameleta wawekezaji.
Hakuq na lolote zaidi ya kutunyanyasa watanzania
Lowassa naye alikosa nini, JPM alifafanua kwanini alikataa Leo mtu uko hai huwezi kujibu hoja za Hayati kweli watu hamnazo
 
Hivi mna matatizo gani lkn? Penda kufanya research ndo uje uandike hapa jukwaani. Unajitia aibu kwa huu mchango wakonwa chuki na ubinafsi hapa ujue. Acha kufata upepo. Mradi wa Bagamoyo una tija kwa Taifa. Hivi Ile chato airport haikusaidii?? Mbona mama alipoenda kigogo busisi hamkulalamika???
10% Upo?
 
Usalama wa Nchi unakuwa hatarini kiuchumi au kiulinzi? Maana kama Ni kiuchumi bado kuna makampuni kibao ya kichina yako hapo nchini Kama ni kiulinzi miundombinu mingi ya jeshi imejengwa na wachina, achia mbali mafunzo mbalimbali yanayotolewa na wachina kwa jeshi letu.

kuna watu wanachekesha sana, hajuu hata ule uwanja wa ndege wa ngerengere umejengwa na wachina, yaani hajui kama hata mafunzo mengi ya askari wetu yanafanywa na wachina hapa.. mwambie akaangalie ile fleer yetu ya ndege za kivita ukiondoa zile Mig nyingine katengeneza nani?.....la mwisho, hivi kwa teknolojia ya mchina akitutaka kijeshi na kiintelejensia anahitaji bandari yetu kweli?
 
tuna bandari tanga, mtwara, Lindi na Dar...hebu lete records ukiondoa bandari ya dar hizo nyingine zinaingiza mapato kiasi gani na meli ngapi zinafunga nanga kwa mwezi....Inawezekana mradi wa Bagamoyo hauko sawa lakini pia tunahitaji sababu za msingi vs faida zake...
 
Mirandi kama bagamoyo hauna tatizo kama unavyofikiri maana muwekezaji anaweka hela zake mwenyewe.
Fitna za jpm ni kukosa 10% ktk huo mradi.
Anapenda aonekane yy ndo kafanya kila kitu ndo maana anasifia mloganzira na viwanda vya pwani eti ni yeye ameleta wawekezaji.
Hakuq na lolote zaidi ya kutunyanyasa watanzania
Unaaminisha kwa sasa hawa wanaopigia debe huu uwekezaji usiozingatia maslahi ya nchi wamepewa 10%?

Unadhani kuwa hii ndiyo kazi tunayokuwa tunawapa viongozi wetu, badala ya kusimamia maslahi ya nchi waende kununuliwa kwa vipande vya fedha kukubali kutuuza bila kujali maisha yetu na mstakabali wa nchi yetu??

Embu,kwanza wewe umeishia darasa la ngapi? Mbona uko na ujingaujinga mwingi sana?

Daah?

Kama JPM alikataa 10% ili kulinda heshima ya watanzania unamwona ni mtu asiyefaa kweli?
 
Tunataka Miradi mingi katika taifa letu, Lakini tunataka miradi ambayo kiukweli italeta ukombozi wa maisha ya wananchi

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ni mradi mkubwa na unaumhimu wake, Lakini kwa nini usiwe wazi?
Hivi zile ndege za Mwendazake mnazoshangilia huku zikiendelea kulitia hasara taifa, mmeshawahi kudai uwazi kwenye ununuzi wake?
kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?
HIvi unadhani Lowassa ni kilaza namna hiyo?! Jombaa, that's politics... kama politics za Magu na CCM yake ya kutoa 50M kwa kila kijiji, na laptop kwa wanafunzi!!!

Moja ya hoja zinazotolewa na wapinzani wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni kwanini isijengwe Bandari ya Tanga!!! Sasa inakushangaza Lowassa akiwa Tanga kwenye kampeni kusema atasitisha Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na serikali yake ku-focus Bandari ya Tanga?
Kuanzisha mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuwepo uwazi wa mkataba uliotiliwa mashaka na viongozi mbalimbali wa nchi hii, ni uhujumu uchumi mkubwa na kuziua bandari zetu ambazo ni tegemeo kubwa la uchumi wetu
Hivi nyie wafuasi wa Magu mmewahi kuoneshwa mkataba upi tangu taifa hili lianzishwe?! Of course, suala la uwazi wa mikataba limekuwa ni kilio cha muda mrefu hadi bungeni, lakini mbona hatuwaoni mkililia kuonesha mikataba kama ya SGR, ununuzi wa ndege, Mradi wa Bwawa la Nyerere, n.k?!

Hivi ni kweli hoja yenu ni kuona mkataba au mnajaribu ku-justify hoja za Magu na kujificha kwenye issue ya mkataba?!
Hivi, Tanzania ni lini tutafahamu kwamba, uwingi wa miradi na sifa ya kuwepo wawekezaji wengi wasio na faida haituongezei chochote zaidi ya kutufanya tuwe taifa tegemezi na lisiloweza kujikomboa na umasikini..!
Umetumia vigezo gani ku-conclude hiyo hoja yako?! Magu alipuuza hata miradi ya gas kule kusini, na akaishia kudanganya watu kwamba eti gas imeuzwa bila kutaja wauzaji ni nani, na waliouziwa ni akina, na serikali yake inachukua hatua zipi!!

Je, unataka kusema uwekezaji kwenye gas hauna faida wakati hadi sasa kuna kiasi kikubwa kabisa cha umeme tunaotumia unatokana na gas, wakati ni sehemu ndogo tu ya gas iliyochimbwa hadi sasa!!
Kuwa na wingi wa miradi haina maana kwamba ni kuondoa umasikini, Umasikini unaweza kuondoka tu pale tutakapokuwa tukifanya uwekezaji wenye tija na kuingia miktaba isiyokandamizi,
Hiyo miradi mingi ni ipi?!
Kushindana ki miradi na nchi fulani bila kujali hiyo miradi inafaida gani ni kujiumiza sisi wenyewe

Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu
Tunashindana na nchi ipi?! Fuatilia historia uone ndoto ya bandari ya Bagamoyo imeanza lini!!!
 
Hauzingatii maslahi ya nchi kwa hoja ipi wakati kwenye thread yako umeonesha wazi kabisa kwamba hujaona mkataba?
Ndiyo mkuu, Mkataba upo lakini wenye utata, na mkataba wenye utataa..!, na waliousema unautata, sio sisi wananchi wa kawaida, ni viongozi wetu, ili kuthibitisha uwongo wa viongozi hawa...! basi uwekwe wazi, la sivyo sisi tunaita ni mkataba usiozingatia maslahi ya nchi!
 
Kwani serikali imepitisha tayari huo mkataba au imesema watakaa kwen meza ya mazungumzo...nadhani swala sio mradi ukiwa haukidhi Basi tunaukimbia lazima tuwe tunakaa nakufanya negositions in our favor kama mwekezaji hata ridhia Basi tunaachana nae.....
 
Hii ni njema sana mkuu, Tunashida moja sisi, ni umasikini usio wa kutosheka, Hata unapokuwa navyo vingi bado utataka tena, ndio huku kunakotuangusha sana, kufikilia matumbo na hofu ya kufa masikini

Hiyo 10% ndio inayotufanya tuwe vipofu, hata yasiyofaa tutaona yanafaa, kisa, tumbo
 
Unaaminisha kwa sasa hawa wanaopigia debe huu uwekezaji usiozingatia maslahi ya nchi wamepewa 10%?

Unadhani kuwa hii ndiyo kazi tunayokuwa tunawapa viongozi wetu, badala ya kusimamia maslahi ya nchi waende kununuliwa kwa vipande vya fedha kukubali kutuuza bila kujali maisha yetu na mstakabali wa nchi yetu??

Embu,kwanza wewe umeishia darasa la ngapi? Mbona uko na ujingaujinga mwingi sana?

Daah?

Kama JPM alikataa 10% ili kulinda heshima ya watanzania unamwona ni mtu asiyefaa kweli?
Kichekesho hiki kiko Tanzania tu, rais akatae 10% kwenye mradi wa bandari ya Bagamoyo, kisha anaenda kupora wananchi wake fedha za wenye Bureau de change, na kubambikia watu kodi kubwa🙆
 
Ndiyo mkuu, Mkataba upo lakini wenye utata, na mkataba wenye utataa..!, na waliousema unautata, sio sisi wananchi wa kawaida, ni viongozi wetu, ili kuthibitisha uwongo wa viongozi hawa...! basi uwekwe wazi, la sivyo sisi tunaita ni mkataba usiozingatia maslahi ya nchi!
Viongozi gani kama sio JPM ambae kuna mengi tu kayasema na sio ya kweli?! Kwa mfano, aliutangazia umma kwamba gas ya Mtwara imeshauzwa, je unaamini kwamba kweli gas imeshauzwa?!

Aliutangazia umma kwamba kabla yake mishahara ilikuwa inalipwa hadi tarehe 15 ya mwezi unaofuata... je, kuna ukweli wowote katika hilo?

Alipata kuutangazia umma kwamba alipoingia sukari ilikuwa inauzwa Sh. 5000, je kuna ukweli wowote kuhusu hilo?!

Wakati akiwa na washikaji zake alipata kusema ni namna gani ilivyo rahisi kutengeneza copper smelters (ya ku-extract gold from Copper) na hivyo akawa anazishangaa serikali zilizopita kwa hatua yake ya kupeleka makinikia nje!!

Je, hadi umauti unamkuta aliwezesha kujenga hizo smelters ambazo alidai ni rahisi sana?!!

Lakini kwa upande mwingine... hivi wewe katika kufuatilia kwako hili suala umeshawahi kusikia popote pale kwamba "Serikali imevunja mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo"?

Hivi unaamini kabisa kwamba mkataba unaweza kuvunjwa kirahisi rahisi tu?!
 
Kwa hiyo mlishausaini tayari siyo?
 
Back
Top Bottom