Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,459
Tunataka Miradi mingi katika taifa letu, Lakini tunataka miradi ambayo kiukweli italeta ukombozi wa maisha ya wananchi

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ni mradi mkubwa na unaumhimu wake, Lakini kwa nini usiwe wazi?

kwa nini tunadhani JPM pamoja na aliyekuwa mgombea Uraisi kupitia Chadema 2015 mh EL wamekuwa waongo kuukataa huu mradi kwamba hauna manufaa yoyote kwa nchi yetu?

Kuanzisha mradi wa Bandari Bagamoyo bila kuwepo uwazi wa mkataba uliotiliwa mashaka na viongozi mbalimbali wa nchi hii, ni uhujumu uchumi mkubwa na kuziua bandari zetu ambazo ni tegemeo kubwa la uchumi wetu

Hivi, Tanzania ni lini tutafahamu kwamba, uwingi wa miradi na sifa ya kuwepo wawekezaji wengi wasio na faida haituongezei chochote zaidi ya kutufanya tuwe taifa tegemezi na lisiloweza kujikomboa na umasikini..!

Kuwa na wingi wa miradi haina maana kwamba ni kuondoa umasikini, Umasikini unaweza kuondoka tu pale tutakapokuwa tukifanya uwekezaji wenye tija na kuingia miktaba isiyokandamizi,

Kushindana ki miradi na nchi fulani bila kujali hiyo miradi inafaida gani ni kujiumiza sisi wenyewe

Mungu ibariki Tanzania na Mungu bariki viongozi wetu
 
Naona kama Rais mwanamke amepata akili kuliko wa-tz wote! Hii ndo hali ya kawaida kwa viongozi wa kiafrika. Wakipata madaraka tu, wanaamini wana akili kuliko wengine wote, hata ktk hali ya Rais wetu anayefahamu wazi ana urais wa urithi.

Rais anaelekea kujifanya kuwa ni Rais wa mageuzi ktk kila kitu, hata mambo ambayo yana mifano mibovu kwa nchi zingine. Badala ya kuanzisha miradi na mipango mizuri ya kwake, yeye amekuwa ni mtu wa kufufua yaliyokataliwa na taifa hili. Tunakubali bandari, mkataba ni upi?
 

Lowassa: Serikali yangu itaangalia jinsi ya kuvunja mkataba wa bandari ya Bagamoyo
Sasa wakati huo alikuwa CCM au unaona raha tu kuninukuu.
 
Hii Bandari ina maana Hayati alitudanganya?

Kwa maslahi mapana ya Taifa mikataba iwekwe wazi

Kwa nchi nzima itakua haina maana.

Labda Kwa Wizara,Wakuu wa Taasisi za Uwajibikaji nchini na Wadau wa muhimu.
 
Mama ajiridhishe tu, Kama vipi ijengwe tu.Mbona mwenda zake alijenga uwanja wa ndege kwao
Mkuu, nakuunga mkono, lakini kwa nini tunataka kukata tamaa kiasi hiki, unadhani ni sahihi tuendelee kukomoana kwamba mbona huyu alifanya ujinga huu, acha na mwingine afanye ujinga huu!

Pingu za maisha na ujinga juu ya taifa letu, ni wakati wa kuchana karatasi lake sasa na kutupilia mbali huo ujinga
 
Hivi unaendelea utaendelea kinyemela kabla ya kila wenye macho kuona ni nini kilichomo?

Hawa wanasiasa ndio wanafanya Siasa ipate sifa mbaya.
 
Waliporudishiwa hela akina Mbowe something fishy was coming! Duh hii nchi kuna watu ni professional! Kuna mtu ana swali?
 
Kwanini ile proposal ya kwanza isiwekwe hadharani tujisomee wenyewe? JPM atleast alipoint out vipengele vya kipigaji kusema ni kichaa pekee angeweza kukubali. Waliokuwa wanamshauri JPM wapo wapi? Mama kawatupa nje?

Mama Samia sijui anakuwa guided na nani? Hii ni hatari kwa usalama wa Nchi
 
Back
Top Bottom