Mpokea hundi wa CRDB Holland House anadharau sana

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
nimekuwa mteja wa kudumu wa CRDB kwa kipindi cha mwaka wa Tano sasa, tangu nimerejea nyumbani Tanzania karibu miezi 3 sasa kuna kazi nafanya ambayo malipo yake ni kwa hundi, sasa kila ninapoenda kujiwekea akiba kwenye akaunti yangu pale CRDB TAWI LA Holland hakika huwa nakwazika kutokana na majibu ya kejeli, masimango na dharau za huyo binti bahati mbaya sijajua jina lake.

wajihi wake ni Dada Mweupe, anavaa hereni ndefu~ndefu, ana cheni za dhahabu shingoni na mikononi.

wakati najiandaa kuhamia Azikiwe Branch kwa huduma zangu utawala lazima ujue swala hili kinaga ubaga.
 
Siku moja mvizie na umpigge picha na uje uiweke hapa tumjuwe... Halafu tuambie anakaa kichumba gani...
 
Hivyo vidada huwa vinalewa na viyoyozi vya pale ndani msamehe bure isee
 
Hahahahaha huyo ni balaa me ni banker pia pindi tuondapo kufanya special clearance haishi nyodo na kwa bank zetu za kibongo usitarajie hata ukimuona branch manager atakuwa na maajabu hiyo ndio level yao ya huduma kwani nilishawahi kwenda nbc nyerere road nikasumbuliwa kwenda kwa branch manager hakuna msaada alionipa zaidi ya kunisukumia kwa manager huduma kwa wateja
 
imenisikitisha sana, unajua mwanzoni nilijua kuwa labda hakuwa kwenye mood ya kazi, lakini naona sasa miezi inakatika, hathamini wateja anajisahau kuwa kupitia fedha zetu yeye ndio anapata mshahara na bonus zake,.
 
Hayo ndio madhara ya kuajiri watu kwa kujuana,urembo na kadhalika wanajiamini kwakuwa ni chakula ya wakubwa so wanafanya watakalo
 
Tanzania kwa ujumla wake tuna tatizo kubwa sana kwenye Huduma kwa wateja, ni kila mahali, Nenda Hotelini, Madukani hali ni hiyo hiyo,

Mfano: Unaweza ingia Dukani ukashangaa unahudumia na mtu aliye weka headphone masikioni, anakula mziki huku anakuhudumia,
 
Si ungeenda kwa branch manager tu na kumueleza hili
Umechagua njia ndefu,ngumu na isiyo na uhakika katika kuondoa udhia huu

Yaani by now angeshaitwa na kuonywa

Na hiyo ingekua njia bora zaidi kwa sababu angesaidia na wateja wengine kuliko yeye akiondoka atakua amejinasua yeye lakini ameacha uozo uendelee kwenye hiyo branch.
 
hii ni sawa na barua ya wazi, vitengo vyao vya habari kwa umma vinasoma hii mitandao, ujumbe utawafikia sawia na hatua kuchukuliwa.

ninawaomba wafanya udadisi wao, wataupata ukweli.
na kama dada atasoma ujumbe huu bila shaka nikifika pale atanitambua vyema, maana jana tu ametoka kunipasha vidonge vyangu
 
Haya sasa majungu kwanini usiende Kwa uongozi wa tawi pale unapoona anafanyadharau sasa wewe unaleta huku kwanini?
 
Ndio shida ya masista duuuu...akishakaakwenye kale kakiyoyozi baaaasi anajivika "imagery" kuwa yeye ndo benki na benki ndo yeye, kumbe vitengo wenyewe wametulia tu na wanapiga mpunga wa kutakata. uashauri wangu wapunguze nyodo nyodo zao.
 
Back
Top Bottom