CRDB badilikeni mapema, tutawakimbia sana msipoangalia

Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,663
842
Ndugu wanabodi,

Heshima sana kwenu. Naomba nijielekeze kwenye mada mohja kwa moja. Tangu niifahamu sekta ya fedha niliiona CRDB kama moja ya benki zenye kasi, ubunifu na hata umakini kiutendaji. Kutokana na hayo niliamua kwa hiyari yangu pamoja na wenzangu kujiunga na benki hii miaka kadhaa iliyopita baada ya kuchoshwa na benki fulani hivi hapa nchini (sitaitaja jina kwa sababu za kibiashara).

Mwanzoni nilifurahia sana huduma za CRDB na sikua na shaka iliposemekana ni premier bank kwa customer service nzuri na ya haraka kwa nchi yetu. Lakini kwa siku za karibuni nimekuwanakutana na huduma zisizorishisha ndani ya benki hii katika matawi mbalimbali. Siku moja nilienda pale CRDB mlimani city kiroho safi kabisa kusukuma mambo yangu. Huwezi amini nilikaa foleni ndefu sana huku tellers wakiwa wawili tu wanaohudumia msururu mrefu wa wateja kede kede walioonekana kutokuridhishwa na huduma walizokutana nazo pale. SBaadhi ya wateja walihamaki walipoona ni tellers wawili pekee wanaohudumia ilihali mstari ni mrefu huku tawili liko kwenye potential area kama ile.

Siku nyingine nilienda CRDB waterfront pale. Hali ni hiyo hiyo. Mstari ni mrefu na tellers ni wawili tu ilhali kuna clearing agents kibao wanaotaka ku-deposit mamilioni ya kodi, tozo mbalimbali na hata malipo makubwa kwa makampuni mbalimbali karibu na bandari kubwa ya nchi (Dar es Salaam). Hali hii huzua mitafaruku ya kuwahiana foleni kwa wateja na hata kujibizana sometimes (jambo ambalo si afya) na kama litaendelea kuna hatari ya benki kupoteza wateja wengi kwa muda mchache ujao kama hawatakuwa makini.

CRDB Azikiwe Premier nako kuna wateja wengi ila angalau kwa mbali japokuwa sometimes kunakuwa na mstari mrefu sana. CRDB Makumbusho nako ni vile vile. Watu wengi na tellers wachache. CRDB Masika morogoro nadhani ndiyo branch kubwa zaidi kwa mkoa ule na ina watu wengi sana japo niliwahi kuhudumiwa pale wanajitahidi sana (mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni). Office space yao ni ndogo sana na Morogoro inazidi kuwa mji mkubwa kila siku. Tafadhali Director of Procurement na Director of Administration shughulikieni hili jambo kwa haraka. Pale Masika morogoro wanapiga kazi sana lakini muwawezeshe office spec kubwa zaidi. Sina shida nao kwa kweli.

List ni ndefu sana lakini jambo nililoligundua ni kwamba CRDB kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi jambo linalopelekea kuzorotesha huduma kwa matawi yao mengi makubwa hasa hapa jijini Dar es Salaam. Uongozi wa CRDB hauna budi kulishughulikia suala hili mapema kabla halijageuka kuwa kansa itakayodumaza utendaji wa taasisi. Na kwa ulimwengu huu wa ushindani ninawajibika kusema kama CRDB wasipojipanga, basi soko litawapanga.

Lingine ambalo linazidi kuwa chukizo kwa watu wengi ni makato makubwa tunayokutana nayo wateja pale tu tunapofanya miamala na hata kupata huduma mbalimbali. Siku moja nilitoa pesa pale CRDB Lumumba ghafla nikaona nimekatwa elfu 12. Nikashanga na sikuridhishwa. Nilijiapiza jioni ile kuwa kutakjapokucha mguu wangu mguu wa branch manager anieleze hayo makato yametoka wapi. Nilisogea pale customer service na walichonieleza kiliniduwaza kwa kweli. Waliniambia hayo makato niliyokatwa yanaitwa annual card fees. Nilishangaa na kujawa na hasira kali kwa sababu sikuelezwa hicho kitu mwanzoni kabisa.

Siku nyingine nilienda ku-renew kadi yangu iliyoisha muda ila nikaelezwa kwamba gharama yake ni Tshs 25,000/=. Nilighafirika sana ila kwa sababu nilikuwa na shida nilikubali utaratibu uendelee ili nitoa akiba yangu iliyokuwepo wakati huo. Matukio hayo yaliniacha na vidonda vikubwa kiasi cha kuanza kutafuta mbadala wa CRDB bank mapema kabisa. Hivi sasa nasubiri nimalizane na mkopo wao niondoke kama wataendelea na utaratibu huu usioridhisha.

Wito wangu kwa uongozi na menejimenti ya CRDB, mnapaswa kuchukua hatua mapema kabla hamjakimbiwa na wateja kwa mpigo. Soko linabadilika na malalamiko kwa utendaji wenu yamekuwa makubwa sana siku za karibuni. Msipochukua hatua na kujipanga mapema, soko litawapanga aminini nawaambia.

Ninaipenda sana CRDB bank lakini mwenendo wake kwa siku za karibuni unanikatisha tamaa kabisa.

Am out.

Nawasilisha hoja.
 
Benki kuna muda ukienda withdraw hela inaitwa chamber kuulizwa hela zote hizi unapeleka wapi.

Mbona huwa waulizi wakati wa kuchukua
 
Afu sijui nani aliambia mabenki kwamba ni vyema kusimamisha wateja katika mistari wakiwa wanaenda kufanya deposit au with-drawl
 
CRDB mwaka huu wamepoteza wateja wengi sana kwenye vyuo vikuu. Mfano huku nilipo wanafunzi wote first year wameambiàna wahamie NMB maana makato ya CRDB yanamaliza boom yao. Na wengine hela ikiingia tu wanahamisha fasta kwenye bank yenye unafuu kwao.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Alaf atm ukienda unambiwa hakuna pesa unaweza zungukua utoe pesa na usipate
 
Mimi kiukweli Nashukuru nina mwaka sasa siko nao sababu kubwa ni makato tu, angalau NMB ndio niko nao so far wako Vizuri.
 
Niliwahi enda fanya interview sehemu fulani hivi tulikua washkaji sita. Wote tumechomekea, jamaa mwingine akaja kavaa suti kabisa, yaani wote tupo serious kimuonekano.

Tumekaa tunamsubiri boss.

Boss kafika kavaa pensi ya jinzi iliyokatwa fulana na ndala. Ndiyo nikajua hela ni nini.
 
Niliwahi enda fanya interview sehemu fulani hivi tulikua washkaji sita. Wote tumechomekea, jamaa mwingine akaja kavaa suti kabisa, yaani wote tupo serious kimuonekano.

Tumekaa tunamsubiri boss.

Boss kafika kavaa pensi ya jinzi iliyokatwa fulana na ndala. Ndiyo nikajua hela ni nini.

We ulienda apply kazi za Hotel Management nn ?? Kazi gani ya maana boss aje kavaa hivyo ??
 
Nilishahama CRDB tangu mwaka jana, sitaki stress wakati hela zangu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom