CRDB badilikeni, tutawakimbia sana msipoangalia

Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,663
842
Ndugu wanabodi,

Heshima sana kwenu. Naomba nijielekeze kwenye mada mohja kwa moja. Tangu niifahamu sekta ya fedha niliiona CRDB kama moja ya benki zenye kasi, ubunifu na hata umakini kiutendaji. Kutokana na hayo niliamua kwa hiyari yangu pamoja na wenzangu kujiunga na benki hii miaka kadhaa iliyopita baada ya kuchoshwa na benki fulani hivi hapa nchini (sitaitaja jina kwa sababu za kibiashara).

Mwanzoni nilifurahia sana huduma za CRDB na sikua na shaka iliposemekana ni premier bank kwa customer service nzuri na ya haraka kwa nchi yetu. Lakini kwa siku za karibuni nimekuwanakutana na huduma zisizorishisha ndani ya benki hii katika matawi mbalimbali. Siku moja nilienda pale CRDB mlimani city kiroho safi kabisa kusukuma mambo yangu. Huwezi amini nilikaa foleni ndefu sana huku tellers wakiwa wawili tu wanaohudumia msururu mrefu wa wateja kede kede walioonekana kutokuridhishwa na huduma walizokutana nazo pale. SBaadhi ya wateja walihamaki walipoona ni tellers wawili pekee wanaohudumia ilihali mstari ni mrefu huku tawili liko kwenye potential area kama ile.

Siku nyingine nilienda CRDB waterfront pale. Hali ni hiyo hiyo. Mstari ni mrefu na tellers ni wawili tu ilhali kuna clearing agents kibao wanaotaka ku-deposit mamilioni ya kodi, tozo mbalimbali na hata malipo makubwa kwa makampuni mbalimbali karibu na bandari kubwa ya nchi (Dar es Salaam). Hali hii huzua mitafaruku ya kuwahiana foleni kwa wateja na hata kujibizana sometimes (jambo ambalo si afya) na kama litaendelea kuna hatari ya benki kupoteza wateja wengi kwa muda mchache ujao kama hawatakuwa makini.

CRDB Azikiwe Premier nako kuna wateja wengi ila angalau kwa mbali japokuwa sometimes kunakuwa na mstari mrefu sana. CRDB Makumbusho nako ni vile vile. Watu wengi na tellers wachache. CRDB Masika morogoro nadhani ndiyo branch kubwa zaidi kwa mkoa ule na ina watu wengi sana japo niliwahi kuhudumiwa pale wanajitahidi sana (mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni). Office space yao ni ndogo sana na Morogoro inazidi kuwa mji mkubwa kila siku. Tafadhali Director of Procurement na Director of Administration shughulikieni hili jambo kwa haraka. Pale Masika morogoro wanapiga kazi sana lakini muwawezeshe office spec kubwa zaidi. Sina shida nao kwa kweli.

List ni ndefu sana lakini jambo nililoligundua ni kwamba CRDB kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi jambo linalopelekea kuzorotesha huduma kwa matawi yao mengi makubwa hasa hapa jijini Dar es Salaam. Uongozi wa CRDB hauna budi kulishughulikia suala hili mapema kabla halijageuka kuwa kansa itakayodumaza utendaji wa taasisi. Na kwa ulimwengu huu wa ushindani ninawajibika kusema kama CRDB wasipojipanga, basi soko litawapanga.

Lingine ambalo linazidi kuwa chukizo kwa watu wengi ni makato makubwa tunayokutana nayo wateja pale tu tunapofanya miamala na hata kupata huduma mbalimbali. Siku moja nilitoa pesa pale CRDB Lumumba ghafla nikaona nimekatwa elfu 12. Nikashanga na sikuridhishwa. Nilijiapiza jioni ile kuwa kutakjapokucha mguu wangu mguu wa branch manager anieleze hayo makato yametoka wapi. Nilisogea pale customer service na walichonieleza kiliniduwaza kwa kweli. Waliniambia hayo makato niliyokatwa yanaitwa annual card fees. Nilishangaa na kujawa na hasira kali kwa sababu sikuelezwa hicho kitu mwanzoni kabisa.

Siku nyingine nilienda ku-renew kadi yangu iliyoisha muda ila nikaelezwa kwamba gharama yake ni Tshs 25,000/=. Nilighafirika sana ila kwa sababu nilikuwa na shida nilikubali utaratibu uendelee ili nitoa akiba yangu iliyokuwepo wakati huo. Matukio hayo yaliniacha na vidonda vikubwa kiasi cha kuanza kutafuta mbadala wa CRDB bank mapema kabisa. Hivi sasa nasubiri nimalizane na mkopo wao niondoke kama wataendelea na utaratibu huu usioridhisha.

Wito wangu kwa uongozi na menejimenti ya CRDB, mnapaswa kuchukua hatua mapema kabla hamjakimbiwa na wateja kwa mpigo. Soko linabadilika na malalamiko kwa utendaji wenu yamekuwa makubwa sana siku za karibuni. Msipochukua hatua na kujipanga mapema, soko litawapanga aminini nawaambia.

Ninaipenda sana CRDB bank lakini mwenendo wake kwa siku za karibuni unanikatisha tamaa kabisa.

Am out.

Nawasilisha hoja.
 
Mkuu mpaka leo unaenda branch kuweka au kuchukua hela wakati mawakala wamejaa kila kona, na unaweza fanya transaction kubwa za kuchukua au deposit hata 10m. Mm kwa kweli sikimbuki lini nimeingiza branch. Hawa mawakala wamewapunguzia sana mzigo no wonder hata wao wamepunguza tellers kwenye zile counters zao
 
Kuna mtu nilimshauri ahame NBC aende CRDB sababu ya mambo flani.
Kafungua fixed account muda ukafika akaenda kuweka tena awamu ya pili.
Wakampigia hesabu faida yake na kuweka tena.
Kabla hajafika nyumbani kwake anapigiwa simu tulikosea mahesabu njoo ujaze upya fomu akawaambia nipo mbali labda siku nyingine. Aliyempigia simu akamuambia nitumie kwenye simu fedha ya ziada niliyokosea mahesabu ili fixed account yako iendelee.
Yule mteja akamjibu nitakuamini vipi kama haunitapeli na wizi wote huu wa mtandaoni/simu?

Baada ya siku chache kakuta pesa yake imeingizwa kwenye account yake ya kawaida(savings account) amekatwa faida yake yote. Ni kwamba alitunza pesa yake bure bila faida.

Walishindwa nini kumsubiri apate ruhusa kazini aje ajaze fomu zao hadi wamekula faida yake yote?
Kukotoa walikosea wao watumishi wa bank.

Suala hili tukipata muda tunakwenda kuwashitaki bank na kuwadai fidia wajiandae CRDB tawi la UDSM. Walimuona yule mdau siyo mjuaji wa sheria au mtu wa kawaida hatawasumbua, hawakujua ANA WATU wajuaji na watata.
 
Vipi si kwamba ni utopolo wa roaster na usimamizi au utopolo wa manager mateller kujiondokea au kupewa kazi za back office au rather kupewa kazi nyingi, au ndio benk ishaenda digital ila wateja ndio bado analogy, usalama wa kuweka pesa kwa wakala ukoje?na je mawakala wanajosheleza? I think hizi banks za wazungu they act europe but we customers in africa should be particularised in our contexts as slow moving emerging markets. Banks in Africa exploit the concept of business captivity as monstars.
 
Kuna mtu nilimshauri ahame NBC aende CRDB sababu ya mambo flani.
Kafungua fixed account muda ukafika akaenda kuweka tena awamu ya pili.
Wakampigia hesabu faida yake na kuweka tena.
Kabla hajafika nyumbani kwake anapigiwa simu tulikosea mahesabu njoo ujaze upya fomu akawaambia nipo mbali labda siku nyingine. Aliyempigia somu akamuambia nitumie kwenye simu fedha ya ziada niliyokosea mahesabu ili fixed account yako iendelee.
Yule mteja akamjibu nitakuamini vipi kama haunitapeli na wizi wote huu wa mtandaoni/simu?

Baada ya siku chache kakuta pesa yake imeingizwa kwenye account yake ya kawaida(savings account) amekatwa faida yake yote. Ni kwamba alitunza pesa yake bure bila faida.

Walishindwa nini kumsubiri apate ruhusa kazini aje ajaze fomu zao hadi wamekula faida yake yote?
Kukotoa walikosea wao watumishi wa bank.

Suala hili tukipata muda tunakwenda kuwashitaki bank na kuwadai fidia wajiandae CRDB tawi la UDSM. Walimuona yule mdau siyo mjuaji wa sheria au mtu wa kawaida hatawasumbua, hawakujua ANA WATU wajuaji na watata.
Pole kamanda thats too much of customer bulling, painful and funny at the same time.
 
duuh juzi juzi tu hapa nimejiunga na hio bank,lakini naona kelele kila kona kuhusu hio bank,mbona mnanishitua
 
Mkuu unayongea ni kweli hzo branch zote nimeenda ni takataka kama mliman pale huwez kuta wafanyakazi kwa heshima ya pale mliman city kuna foreigners kibao, watu kibao wanataka huduma unakuta teller 2 tu afu folen kama yote branch kidogo wanajitahid kwa dar ni vijana ya pale lumumba kidogo wako vzr sijui kwkaua wapo karibu na CCM. Nilishachoma card ya CRDB muda sana niko NMB sahiv naenjoy. Wale wafanyakazi wa CRDB wanaonaga kama wamewin maisha sana wanaringa sana qmmmk
 
Mkuu mpaka leo unaenda branch kuweka au kuchukua hela wakati mawakala wamejaa kila kona, na unaweza fanya transaction kubwa za kuchukua au deposit hata 10m. Mm kwa kweli sikimbuki lini nimeingiza branch. Hawa mawakala wamewapunguzia sana mzigo no wonder hata wao wamepunguza tellers kwenye zile counters zao

Mkuu kuna watu tunafanya transactions above 100m siwez kwenda kwa wakala aseee lazma niende direct bank na kwa usalama wa pesa.
 
ujiulizi kwa nini mabenki mengi yanapenda kuja tanzania zaidi !?

tanzania shamba la bibi na hakuna wa wakuwazuia kuanzia riba,makato na utumbo wowote
Kwa hiyo Tanzania Kuna benki nyingi kuliko nchi yyte ile!!?..utaratibu wa riba upo vp nchi zingine ukilinganisha na tz!?
 
Online Purchase nayo siku hizi CRDB imekuwa hovyo sana! Ukiwa na Online Refunds siku hizi hawaweki direct mpaka uanze kuwasiliana nao kwanza! CRDB Ina loose quality yake kwa Kasi sana!
 
wanajivunia miaka mingi ya mageuzi ya masuala ya kibenki tz, huzungumzi mageuzi makubwa ya sekta ya kibenki bila kuitaja hao mabwana, bwana nsekela hebu pitia huku muweze kuadapt opinions za wateja, kuweni bank ya kuwamotivate wafanyakazi wenu..walipeni vzuri sawa na hadhi ya benki yenu ilipofikia ili wawe na molari ya kazi wasiwe wanatoa majibu ya kunya..wafanyakazi wengi bank mshahara laki tisa tek home af mikopo on top unakuta yuko off mood all the time
 
CRDB wako wapi, wajibu tuhuma hizi, na Dodoma ATMs zao fedha ni za kubahatisha unaweza tembea hata branch tatu bila mafanikio, Mwisho wa siku ukaamua kutolea tawi jingine tofauti kabisa.
 
Mimi nashangaa mteja sio mtumishi lakini Ni mteja wao wa muda mrefu takribani miaka 20 lakini kwenye huduma ya mikopo walioweka online mteja hawezi kukopa kwasababu tuu eti Hana mshahara unsopitia kwao tubadilike aisee.Mteja anatumia bank yenu ana miaka zaidi ya ishirini na income yake mnsiona Sasa hii inakuaje?
 
Kuna mtu nilimshauri ahame NBC aende CRDB sababu ya mambo flani.
Kafungua fixed account muda ukafika akaenda kuweka tena awamu ya pili.
Wakampigia hesabu faida yake na kuweka tena.
Kabla hajafika nyumbani kwake anapigiwa simu tulikosea mahesabu njoo ujaze upya fomu akawaambia nipo mbali labda siku nyingine. Aliyempigia simu akamuambia nitumie kwenye simu fedha ya ziada niliyokosea mahesabu ili fixed account yako iendelee.
Yule mteja akamjibu nitakuamini vipi kama haunitapeli na wizi wote huu wa mtandaoni/simu?

Baada ya siku chache kakuta pesa yake imeingizwa kwenye account yake ya kawaida(savings account) amekatwa faida yake yote. Ni kwamba alitunza pesa yake bure bila faida.

Walishindwa nini kumsubiri apate ruhusa kazini aje ajaze fomu zao hadi wamekula faida yake yote?
Kukotoa walikosea wao watumishi wa bank.

Suala hili tukipata muda tunakwenda kuwashitaki bank na kuwadai fidia wajiandae CRDB tawi la UDSM. Walimuona yule mdau siyo mjuaji wa sheria au mtu wa kawaida hatawasumbua, hawakujua ANA WATU wajuaji na watata.

Kwanza inabidi huyo jamaa apeleke malalamiko kimaandishi CRDB na benki kuu kuna dawati au kitengo cha kushughulikia kero za wateja wanaopata matatizo kwenye mabenki.
 
Ndugu wanabodi,

Heshima sana kwenu. Naomba nijielekeze kwenye mada mohja kwa moja. Tangu niifahamu sekta ya fedha niliiona CRDB kama moja ya benki zenye kasi, ubunifu na hata umakini kiutendaji. Kutokana na hayo niliamua kwa hiyari yangu pamoja na wenzangu kujiunga na benki hii miaka kadhaa iliyopita baada ya kuchoshwa na benki fulani hivi hapa nchini (sitaitaja jina kwa sababu za kibiashara).

Mwanzoni nilifurahia sana huduma za CRDB na sikua na shaka iliposemekana ni premier bank kwa customer service nzuri na ya haraka kwa nchi yetu. Lakini kwa siku za karibuni nimekuwanakutana na huduma zisizorishisha ndani ya benki hii katika matawi mbalimbali. Siku moja nilienda pale CRDB mlimani city kiroho safi kabisa kusukuma mambo yangu. Huwezi amini nilikaa foleni ndefu sana huku tellers wakiwa wawili tu wanaohudumia msururu mrefu wa wateja kede kede walioonekana kutokuridhishwa na huduma walizokutana nazo pale. SBaadhi ya wateja walihamaki walipoona ni tellers wawili pekee wanaohudumia ilihali mstari ni mrefu huku tawili liko kwenye potential area kama ile.

Siku nyingine nilienda CRDB waterfront pale. Hali ni hiyo hiyo. Mstari ni mrefu na tellers ni wawili tu ilhali kuna clearing agents kibao wanaotaka ku-deposit mamilioni ya kodi, tozo mbalimbali na hata malipo makubwa kwa makampuni mbalimbali karibu na bandari kubwa ya nchi (Dar es Salaam). Hali hii huzua mitafaruku ya kuwahiana foleni kwa wateja na hata kujibizana sometimes (jambo ambalo si afya) na kama litaendelea kuna hatari ya benki kupoteza wateja wengi kwa muda mchache ujao kama hawatakuwa makini.

CRDB Azikiwe Premier nako kuna wateja wengi ila angalau kwa mbali japokuwa sometimes kunakuwa na mstari mrefu sana. CRDB Makumbusho nako ni vile vile. Watu wengi na tellers wachache. CRDB Masika morogoro nadhani ndiyo branch kubwa zaidi kwa mkoa ule na ina watu wengi sana japo niliwahi kuhudumiwa pale wanajitahidi sana (mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni). Office space yao ni ndogo sana na Morogoro inazidi kuwa mji mkubwa kila siku. Tafadhali Director of Procurement na Director of Administration shughulikieni hili jambo kwa haraka. Pale Masika morogoro wanapiga kazi sana lakini muwawezeshe office spec kubwa zaidi. Sina shida nao kwa kweli.

List ni ndefu sana lakini jambo nililoligundua ni kwamba CRDB kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi jambo linalopelekea kuzorotesha huduma kwa matawi yao mengi makubwa hasa hapa jijini Dar es Salaam. Uongozi wa CRDB hauna budi kulishughulikia suala hili mapema kabla halijageuka kuwa kansa itakayodumaza utendaji wa taasisi. Na kwa ulimwengu huu wa ushindani ninawajibika kusema kama CRDB wasipojipanga, basi soko litawapanga.

Lingine ambalo linazidi kuwa chukizo kwa watu wengi ni makato makubwa tunayokutana nayo wateja pale tu tunapofanya miamala na hata kupata huduma mbalimbali. Siku moja nilitoa pesa pale CRDB Lumumba ghafla nikaona nimekatwa elfu 12. Nikashanga na sikuridhishwa. Nilijiapiza jioni ile kuwa kutakjapokucha mguu wangu mguu wa branch manager anieleze hayo makato yametoka wapi. Nilisogea pale customer service na walichonieleza kiliniduwaza kwa kweli. Waliniambia hayo makato niliyokatwa yanaitwa annual card fees. Nilishangaa na kujawa na hasira kali kwa sababu sikuelezwa hicho kitu mwanzoni kabisa.

Siku nyingine nilienda ku-renew kadi yangu iliyoisha muda ila nikaelezwa kwamba gharama yake ni Tshs 25,000/=. Nilighafirika sana ila kwa sababu nilikuwa na shida nilikubali utaratibu uendelee ili nitoa akiba yangu iliyokuwepo wakati huo. Matukio hayo yaliniacha na vidonda vikubwa kiasi cha kuanza kutafuta mbadala wa CRDB bank mapema kabisa. Hivi sasa nasubiri nimalizane na mkopo wao niondoke kama wataendelea na utaratibu huu usioridhisha.

Wito wangu kwa uongozi na menejimenti ya CRDB, mnapaswa kuchukua hatua mapema kabla hamjakimbiwa na wateja kwa mpigo. Soko linabadilika na malalamiko kwa utendaji wenu yamekuwa makubwa sana siku za karibuni. Msipochukua hatua na kujipanga mapema, soko litawapanga aminini nawaambia.

Ninaipenda sana CRDB bank lakini mwenendo wake kwa siku za karibuni unanikatisha tamaa kabisa.

Am out.

Nawasilisha hoja.

Tangu aondoke KIMEI, CRDB is no more. Huyu jamaa aliyepo siyo kabisa. Kwanza ni mtu mwenye dharau, uelewa wake kwenye mambo kadhaa unamipaka lakini ninanusa harufu ya kutokukubali hata anaposhauriwa na wanaojua mambo asiyoyajua. Kwa ujumla jamaa ni wa hovyo.
Hili nililitegemea kuwa linakuja.
Tatizo la CRDB liko katika ngazi ya juu ya uongozi wao.
 
Labda wapo kwenye mpango wa kupunguza wateja, maana mfano airtel walikuwa na watu wengi wakazingua now offer kila siku. Wako wapi NBC walilinga hadi basi sasa naona full matangazo
 
Ni kweli lakini kwa pesa hiyo huwezi panga foleni kwa wale teller wa kawaida, utaingia kwa kale kachumba ka bulk cash, so issue ya foleni wala haitakusumbua

Mkuu hukohuko unakuta teller hayupo au anakwambia mtandao haupo
 
Back
Top Bottom