Wadau,
Ni kweli kuwa katika benki nyingi hakuna Customer care, lakini angalau CRDB Sio wabaya sana, unaweza kutofautiana na mtu lakini bado credibility ya benki ikawa iko juu, kwa benki zetu za kibongo CRDB Mimi binafsi nawakubali sana, Nafanya Transactins na benki nyingi, Lakini CRDB Wako vizuri, Mimi binafsi ni Mteja Holland House na account zangu na za ofisi ziko pale, huyo Dada mnayemsema kiukweli sijawahi kupata naye shida simtetei lakini nasema kuwa huwa ananihudumuia vizuri na sio yeye tu Hata wafanyakazi wengine pale Holland house wanatoa huduma vizuri, kwa hiyo tusimuhukumu dada wa watu kwa kuwa mmetofautiana kidogo, labda kama kuna kitu kingine ambacho hujasema.