DOKEZO Mpanda hali ni mbaya, Watoto wengi hawaendi shule, wanaingia mtaani kufanyabiashara, Serikali iko wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Hali ya biashara ya vyuma chakavu na matunda mbalimbali inaendelea kushamiri katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na imekuwa ikifanywa kwenye maeneo ya Manispaa hiyo na watoto wadogo ambao wanapaswa kuwa Shuleni kwenye shule za Msingi.

Licha ya Serikali kufanya jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya elimu hali ya watoto wadogo katika Manispaa ya Mpanda ni tofauti kabisa kwani muda ambao watoto hao wanatakiwa kuwa shuleni wao wanatumia muda huu kufanya biashara mitaani na kwenye nyumba za starehe.

Biashara ambazo watoto hao wengi umri wao ni kati ya miaka tisa hadi 13 wanazozifanya ni vyuma chakavu na matunda kama ndizi, tango, Karanga, machungwa na maembe.

Mmoja wa watoto hao Mkazi wa Mtaa wa Shanwe ambae jina limehifadhiwa amesema kuwa wamekuwa hawaendi shule na badala yake wamekuwa wakizunguka mitaani kutafuta vyuma chakavu na kwenda kuviuza.

Amebainisha kuwa soko lao kubwa la kuuza vyuma chakavu lipo maeneo ya madukani katikati ya Manispaa ya Mpanda ambapo kilo moja ya chuma chakavu wamekuwa wakiuza kwa bei ya shilingi 500.

Naye mtoto mwingine mkazi wa Kawajense amesema licha ya kuwa bado na umri mdogo lakini kufanyabiashara muda wa masomo wanaona ni jambo la kawaida kabisa kwani hakuna hatua zozote ambazo wanachukuliwa wao wala wazazi wao.

Ameitaja changamoto ambayo wamekuwa wakikutana nayo wanapokuwa wanafanyabiashara za kuuza matunda na mbogamboga kutakiwa kimapenzi has ana watu wazima bila kujali kuwa wao bado ni watoto wadogo bado.
Watoto.jpg

TAMKO LA SERIKALI
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph amesema “Tumeshachukua hatua na tunaendelea kuchukua hatua kupitia Ustawi wa Jamii kwa maana ya kumuelekeza Mkurugenzi na Afisa Ustawi ili kudhibiti hiyo hali.

“Wanaokuwa nyuma ya pazia ya vitendo hivyo hasa ni Wazazi, wao ndio ambao huwa wanakuwa nyuma ya vitendo hivyo, inapotokea wanabainika kuhusika wanaadhibitiwa lakini baada ya muda Watoto wanarejea tena mtaani.

“Hatua zinazochukuliwa na mamlaka mara nyingi ni kuwapiga faini na kampeni hiyo inafanyika kila mwezi.”

“Chanzo kikubwa ni wazazi ndio ambao wanachangia, wanawatumia watoto kama kitega uchumi.”


USTAWI WA JAMII WAELEZA HALI ILIVYO
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mpanda, Agness Buraganya amesema “Changamoto ipo na huwa tunatoa elimu na kuingia mtaani kuwakamata Watoto wanaotoroka au kukwepa shule, tunawaelewesha wazazi na walezi wajue kuwa kumtumikisha mtoto ni kosa.

“Tangu Mwaka 2022 hadi Machi 2023 kuna Watoto 34 ambao tumewakamata kwa makosa ya kukwepa kwenda shule na kuingia mtaani.

“Kuhusu wazazi, ambaye amekamatwa na kupigwa faini ni mmoja, alitozwa faini ya Tsh 50,000 kwa mujibu wa Sheria.

"Wazazi au walezi wengine hata tunapowakamata kunakuwa na changamoto kadhaa ikiwemo Watoto wenyewe kufanya hivyo kwa kuwa hawana chakula nyumbani.

“Wengine wanaishi katika mazingira magumu, wanalazimika kutafuta chochote, ukimkamata mtoto anakwambia hana hata daftari.

“Watoto wengine wanaishi na bibi au babu zao ambao hawana uwezo na ukisema uwapige faini wanakuwa hawana uwezo wa kuilipa hiyo."
 
Mtoto anayefanya biashara sasa hivi baadala ya kwenda shule ana akili sana.
 
Serikali ifanye nini zaidi ya kuwapa shule wajifunze wanayoyaweza? Hao watoto wana akili sana, wameona kuliko kwenda kupotezewa muda halafu mwishoni watangaziwe wamefeli mtihani wameona bora wajikite kwa kile wanachoweza kufanya ili kujiletea maendeleo wangali wadogo.

Nini tafsiri yake? Ni kwamba mfumo wa elimu umekuwa mkongwe na hauna tija kwa wanafunzi tena zaidi ya kupoteza muda kujifunza vitu ambavyo hawatavifanya maishani mwao
 
Hali ya biashara ya vyuma chakavu na matunda mbalimbali inaendelea kushamiri katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na imekuwa ikifanywa kwenye maeneo ya Manispaa hiyo na watoto wadogo ambao wanapaswa kuwa Shuleni kwenye shule za Msingi...
Karbia Asilimia 50 ya wakazi wa Mji wa Mpanda ni WAKIMBIZI WA BURUNDI lawama ziende kwa Masha Mbunge wa Nyamagana wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alipewa anachojua yeye mwaka 2014 Wakimbizi wooote LAKI 2 na ushee wa Makazi ya Katumba na Mishamo wakapewa Uraia.

Watanzania hawakusema chochote na kinachofanyika sasa hao WARUNDI wanazaaa watoto kuanzia 10 na kuendelea ili waijaze Tanzania na Madaraka wanayataka sana tu na wengine tayari ni Viongozi wenu.

Hao watoto uliowaona wametapakaa hapo Mjini ndio zao la Uovu huo uliofanywa kwa Ushirikiano wa Masha na UNHCR.

ANYWAY Mwalalauli.....Oni....
 
Tanzania hii watoto wengi hasa wa wafugaji hawaendi shule kabisa.
na watusua maisha
Fikiria baba ana wake 3 Kila MKE ana ng'ombe 100na ana watoto 4 mtoto shulenyake ni mifugo tuu by the time mtoto Ana miaka 18ana ng'ombe 100 anaoa anaanza maisha by the time ana 30ngombe 500
 
Back
Top Bottom