Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Hamis Misigalo ambaye ni Diwani wa Kata ya Mpanda Hoteli na William Mbogo Diwani wa Kata ya Majengo wamesema Wanawake hao wamekuwa kero na kikwazo katika maadili ya Mtanzania ambapo kila wanapokamatwa na kuchukuliwa Sheria kali lakini bado wamekua wakirudi katika nyumba hizo ambapo wameomba Sheria kali itungwe ya kuthibiti tabia hiyo ya Wanawake kuishi katika madangulo.
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Deudatus Kangu amesema jumla ya makahaba 15 wamekamatwa katika Kata ya Shanwe ambapo amesema sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo faini.
Biashara haramu ya ngono inayofanywa na baadhi ya mabinti na wanawake katika baadhi ya mitaa ya manispaa imekithiri wamekuwa wanafukuzwa na kukamatwa lakini bado ongezeko linakua kubwa kila kukicha.