Muvi gani seriously ulijikuta unatoa machozi (wakati unaiangalia au baada ya kuiangalia) kutokana na uhalisia wake kukugusa sana moyoni...achana na ile umeingalia ikakugusa na kuikubali tu kwa kuwa ni nzuri...NO..ILIYOKUTOA CHOZI!!
Sina uhakika kama hii topic ilishawahi jadiliwa humu maana nimejaribu ku search ila sijapata ninachokitaka..
Kwa upande wangu mimi ni hizi..
1. Marley and me
...hii nilivyoangalia mara ya kwanza baada tu ya kuisha nikaingia zangu chooni kujifungia ili nifute machozi maana tulikuwa tunaangalia watu wengi..kila mtu alinyanyuka kivyake ofcoz so sijui wengine kama nao walilia au la..
2. Pursuit Of Happiness
...nilijikuta tu machozi yanandondoka mwenyewe wakati muvi inaendelea..
3. Hatchiko the Dog Story
...inatia huruma sana hii..
4. Armeggedon
...ni SCI-FI movie ila pale mwisho chozi lilitoka kimtindo..
5. JOHN Q
6. Rango (Animation)
...hii machozi kwa kucheka...very touching ila inachekesha balaa..
7. Black Hawk Down
8. Blood Diamond
...hizi ni baadhi ya nnazozikumbuka harakaharaka...ningependa kuonza na nyingine zaidi ya hizi kwa msaada wenu..
kuna movie ya kihindi flani nimeisahau jina
kuna jamaa ana mpenda demu bt kwa kuwa dini n tofauti inakuwa zonge mara akapata kipigo akaumia ubongo akapelekwa katika hoapital ya vichaa full minyororo,akapata nafuu kujieleza si chizi jamaa hawamuelewi,huku demu analazimishwa kuolewa,siky moja akaenda kumcheki jamaa hospital mchizi akawa kalala demu kumuona jamaa kaumia maana alijaribu kutoroka akandondoka akaumia,saa demu alipoona akaondoka analia jamaa anaamka anamuona yule demu anaondoka kwa mbali anamuita wapi maana vichaa wanapiga makelele dah
demu kurudi home siku ta harusi ndo imefika akicheki jamaa kawa chiZi,na aanalazimishwa kuolewa na mtu mwingine,akamua kujiua huku mchizi akafanikiwa kutoroka hoapital hadi kwa kina yule demu anafika tu anakuta msibaaa dahh sasa kule hospital wanamtafuta na magariii
mchizi kuona demu wake kafaa na yy alikuwa hospital japo kapona akaona hakuna aja n heri arudi akatokaa nje,jinsi alivyokuwa anatoka anakutana na kaka yake,shemeji yake rafiki zake wanambembeleza na kulia kumshika miguu asieende kwenye gari jamaa wapi ndo kwanza analia anazidi kuchapa mwendo...hapa nilitoa chozi maana jama akaona heri akaishi ktk hospital ya vichaaaaa kuliko kuishi uraian wakati demu wake kajiuaaa kwa wazazi kumchagulia mchumba kisa dini daaah
Dah mkuu,nimesoma maelezo ikawa km yale matukio nayaona tna,kwakweli inasikitisha,so saad.
watched over five times ndio nikaimaliza, nilikuwa nikifika pale wanashushwa train station then wazee wanabebwa kwenye matela wanapelekwa kwenye tanuru, nabofya stop ...eject narudisha kwenye kasha naenda kufanya kitu au shughuli yoyote tu nijisahaulishe.
Movie ya amistad ilinifanya niwe racist hadi leo. Ilipotoka tutulienda kuiangalia na ragiki yangu mmarekani mweusi ambae mmoja wa mababu zake ni survivor wa ile trip ya meli. Tulilia throughout the movie while holding hands. Niliongeza interest kwenye black history. Cnn documentaries za ubaguzi wa south africa ziliniharibu kichwa kabisa ninabreak down na kulia. Pamoja na mibhange im very emotional na kwenye movie nyingi hasa uonevu wa maskini na unyanyasaji wa mwanamke.
Parsuit of happyness nayo iliniliza na kunifanya nimchukie yule mwanamke. Not wiyhout my daughter made us cry (na mamangu and my sisters miaka hiyo). Switched at birth nayo haikuwa rahisi kwangu. Slumdog millionnaire made me shout to the screen.
Kuna movie ya kidosi inaitwa Kal Ho Naa HoMuvi gani seriously ulijikuta unatoa machozi (wakati unaiangalia au baada ya kuiangalia) kutokana na uhalisia wake kukugusa sana moyoni...achana na ile umeingalia ikakugusa na kuikubali tu kwa kuwa ni nzuri...NO..ILIYOKUTOA CHOZI!!
Sina uhakika kama hii topic ilishawahi jadiliwa humu maana nimejaribu ku search ila sijapata ninachokitaka..
Kwa upande wangu mimi ni hizi..
1. Marley and me
...hii nilivyoangalia mara ya kwanza baada tu ya kuisha nikaingia zangu chooni kujifungia ili nifute machozi maana tulikuwa tunaangalia watu wengi..kila mtu alinyanyuka kivyake ofcoz so sijui wengine kama nao walilia au la..
2. Pursuit Of Happiness
...nilijikuta tu machozi yanandondoka mwenyewe wakati muvi inaendelea..
3. Hatchiko the Dog Story
...inatia huruma sana hii..
4. Armeggedon
...ni SCI-FI movie ila pale mwisho chozi lilitoka kimtindo..
5. JOHN Q
6. Rango (Animation)
...hii machozi kwa kucheka...very touching ila inachekesha balaa..
7. Black Hawk Down
8. Blood Diamond
...hizi ni baadhi ya nnazozikumbuka harakaharaka...ningependa kuonza na nyingine zaidi ya hizi kwa msaada wenu..
Not without my daughter, Neria,
Hiyo ya wazamiaji wa kiafrika inaitwa DEADLY VOYAGE, ni filamu kali na inasikitisha sana. Hili ni tukio la kweli lililotokea huko Ghana miaka ya '90, itafute mkuu.Jumong wakati mama yake alipouwawa,
Neria wakati yule mama alipokuwa akipata yale mateso
"Kuchkuch hota he" ya kihindi wakati Anjel anakwenda kumwambia Rahul kuwa anampenda na Rahuli anasema na yeye atasema hivyo hivyo nani Tina. kisha wanapoachana Rahuri anakwenda kumwambia Tina kuwa anampenda basi Anjel anarudi nyumbani akilia anamwambia matron the love is not for me na ule wimbo ukipigwa hakika machozi yalinidondoka.
Halafu kuna nyingine huwa siikumbuki ilikuwa inaitwaje ila kuna waafrika walizamia meli ya kwenda ulaya walikuwa kama nane, walivyoingia kwenye meli walijificha kwenye mizigo ambako baadhi ya mizigo yalikuwa ni magunia ya karanga. ambacho ndicho kilikuwa chakula chao.
Baada ya meli kuenda masafa marefu wakawa wamezoea kule chini, kila Wale wazungu walipokuwa wakiangalia usalama wa mizigo wanajificha bahati mbaya siku moja mzungu mmoja akaona gunia la karanga limetobolewa akaamua kuweka mtego bila wao kujua akawaona basi yale mateso waliyopata ya kuuwawa mmoja mmoja ndipo paliponiliza lakini mwisho kuna mmoja alifanikiwa kuokoka wakati meli inamtia nanga kwenye mji ilokuwainaenda yule jamaa wakati wanahangaika kumkamata wamuuwe kama wenzao akajitosa majini akaogelea huku akiwa amechoka kwa njaa na mateso ya melini na wale wazungua wanajitajidi wahakikishe anakufa vile anafika nchi kavu akaanza kukimbia akapate msaada na wale wanamfukuza wamuue kupoteza ushaidi wa kuwauwa wenzake wakikaribia kumkamata akadondoka chini akazimia lakini wale askari wa bandari walimwona wakaja kumuokoa.
kwa yeyote anayeijua naomba jina la hii movie niitafute.
nyingine ni hadithi ya Adili na nduguze, bint chura n.k
Asante Katavi ngoja nijaribu kuitafuta kwenye mtandao kama nitaipata niipakue.Hiyo ya wazamiaji wa kiafrika inaitwa DEADLY VOYAGE, ni filamu kali na inasikitisha sana. Hili ni tukio la kweli lililotokea huko Ghana miaka ya '90, itafute mkuu.
Anza kanooni ,sina hakika na spelling ila ni picha ya kihindi
Usisahau na Sholay mkuu.Hatya..
Infact sio kunitoa machozi but ni movie ambazo zimewahi kunisikitisha sana
1. Everybody's Baby the rescue of Jessica Mcclure
2. The green mile
3. The way back
4. The boy in the striped pyjamas
5. After shock
6. Rules of Engagement
7. Saving private Ryan
8. A day in Iraq: American Soldier
9. We were soldiers
10. Nightmare on Elm street
11. Behind enemy line
hizi ni kati ya best movie zilizowahi kunisikitisha sio zote lakini ziko nyingi
Nimeipata lakini ni mp4 sijui jinsi ya ku-convert ili niweze kuiona kwenye DVD nyumbani nimeishi kuiangalia kwenye computer. si unajua DVD zetu nyingi ni MPEG2. Je ndugu katavi unaweza nisaidia how to convert nifaidi na wengine.Asante Katavi ngoja nijaribu kuitafuta kwenye mtandao kama nitaipata niipakue.