Moto wa kisasi unawaka ndani yangu!

Moto wa kisasi unawaka ndani yangu!

Ningekua mimi, ningekula nao sahani moja bila kujali kama nitaacha ushahidi ama la...
 
Hongera kwa kukubali ushauri wa kusahau yaliyopita..tulia mumtunze,mumlee na kumfariji mama yenu ambaye sasa ni mjane..kulipiza kisasi kungemletea maumivu mapya kwani ungelazimika kukimbia au ungekamatwa na kupelekwa jela..chukua muda utazoea.

Thanks mkuu!
 
Kama wengi walivyokushauri...songa mbele

And if I were you hata huko mahakamani nisingekata rufaa coz muuaji hata akinyongwa haiondoi uhalisia kwamba babako kauawa.

Nimepata kuwa kwenye situation hiyo...wauwaji waliachiwa lakini me and my bro being the eldest tulikubaliana focus yetu iwe mama na siblings wetu.
Wauaji walitusababishia umaskini lakini hawakuchukua umoja wetu na upendo kwa mama yetu.

Baada ya miaka 20 leo mama anakula kivulini na wadodo zetu mambo yao si haba...

Muuwaji wa babako akiuawa sasa hivi familia yake nao watataka kulipa kisasi....hiyo vita huwa haina mwisho.

Embrace forgivess....
 
Mkuu pole sana kwa yote yalokukuta, Kumbuka kuwa kisasi hulipwa na Mwenyezi Mungu pekee. Hivyo basi muombe Mungu akupe ujasiri wa kusahau na pia Muombee Baba apumzike kwa amani.Rejea Warumi 12:19, na Mithali 20:22
 
nitafute nikupatie bastola ya kutengenezwa kwa mkono na risasi zake ukamalize kazi
 
Hii kesi inafanana sana na ya yule kigogo wa CCM Mwanza aliyeenda shambani na bunduki akaishiia kukumbana na mob justice. Nadhani ilikuwa mwaka jana. Na kama nakumbuka vizuri kuna uzi ulikuwepo hapa JF.
 
Salam wanaJF! Ni mwaka mmoja tangu baba yangu auawe kikatili,lilikuwa tukio baya,lililoniumiza sana. Kilichoniumiza sana sio kifo chake, kwa kuwa najua fika kuwa kila nafsi itaonja mauti,kilichoniumviza ni swali la kwanini wamuue kikatili kiasi kile? Namshukuru Mungu nilifarijika kuona wauaji wakikamatwa na kuwekwa rumande. Katika hali ya kushangaza wauwaji wale wameachiwa jana ikiwa ni siku chache kabla ya "deathdate" ya baba yangu mpendwa! Wauaji na familia zao wamefanya karamu kubwa ya ushindi! Mpaka sasa nashindwa kuelewa wameachiwa vipi ili hali kuna mashahidi walioshuhudia tukio hilo? Wameachiwa vipi wakati kesi haijasilizwa hata siku moja? Je,wameachiwa kwa dhamana? Tangu lina kesi ya mauaji ikawa na dhamana? Kuachiwa kwao kumeamsha uchungu wa msiba upya, mama yangu na wadogo zangu wanalia sana.Nina uchungu mwingi sana kiasi cha kuona kuwa napaswa kulipa kisasi kwa mkono wangu mwenyewe,kwasababu nilitegemea sheria itachukua mkondo wake lakini nimedhihirisha kuwa HAKUNA HAKI DUNIANI,nikisema nimwachie Mungu naona kwa MUNGU MBALI! Wadau nishaurini cha kufanya,kwani roho ya kisasi imeshanivaa.
Mkuu Mimi Nina the same kesi Kama Hyo Hyo Na Mimi nataka nilipe kisasi Na Niko tayar ila sitaki kumshirikisha ndugu hata mmoja naomba unipm mkuu tuyajenge
 
Pole sana kwa hali unayopitia. Mimi nilishasamehe na sasa maisha yanaendelea. Nakushauri nawe ufanye hivyo ili upate amani ya moyo.
 
Katika maisha neno msamaha ndio neno kubwa sana limebeba mambo mengi hapa duniani kuna mengi sana usipo samehe utaua wengi.
 
Pole sana kwa hali unayopitia. Mimi nilishasamehe na sasa maisha yanaendelea. Nakushauri nawe ufanye hivyo ili upate amani ya moyo.
Hongera kwa uamuzi wa busara! Mwenyezi Mungu azidi kukusimamia!
 
Achana na ufala wa kusamehe mjomba... kuna mambo ya kusamehe.....

Eye for an eye wapige tukio hao jamaa bt tumia akili sana usidakwe ila wafanyizie... watakulaje bata mtaani wakati wametoa uhai wa mzee na unawajua kabisa
 
Salam wanaJF! Ni mwaka mmoja tangu baba yangu auawe kikatili,lilikuwa tukio baya,lililoniumiza sana. Kilichoniumiza sana sio kifo chake, kwa kuwa najua fika kuwa kila nafsi itaonja mauti,kilichoniumviza ni swali la kwanini wamuue kikatili kiasi kile? Namshukuru Mungu nilifarijika kuona wauaji wakikamatwa na kuwekwa rumande. Katika hali ya kushangaza wauwaji wale wameachiwa jana ikiwa ni siku chache kabla ya "deathdate" ya baba yangu mpendwa! Wauaji na familia zao wamefanya karamu kubwa ya ushindi! Mpaka sasa nashindwa kuelewa wameachiwa vipi ili hali kuna mashahidi walioshuhudia tukio hilo? Wameachiwa vipi wakati kesi haijasilizwa hata siku moja? Je,wameachiwa kwa dhamana? Tangu lina kesi ya mauaji ikawa na dhamana? Kuachiwa kwao kumeamsha uchungu wa msiba upya, mama yangu na wadogo zangu wanalia sana.Nina uchungu mwingi sana kiasi cha kuona kuwa napaswa kulipa kisasi kwa mkono wangu mwenyewe,kwasababu nilitegemea sheria itachukua mkondo wake lakini nimedhihirisha kuwa HAKUNA HAKI DUNIANI,nikisema nimwachie Mungu naona kwa MUNGU MBALI! Wadau nishaurini cha kufanya,kwani roho ya kisasi imeshanivaa.
Pole sana! Ni haki yako kulipa kisasi kwa msogeza huyo katili kwa Mungu halafu huko utamwachia Mungu na baba yako wakutane mahakani yao!
 
Mkuu pole sana kwa yote yalokukuta, Kumbuka kuwa kisasi hulipwa na Mwenyezi Mungu pekee. Hivyo basi muombe Mungu akupe ujasiri wa kusahau na pia Muombee Baba apumzike kwa amani.Rejea Warumi 12:19, na Mithali 20:22
Ubarikiwe 🙏🏻
 
Poleh sana jamani
Kusamehe ni kazi ngumu sana

Kisasi ni mtihani sana pia

Chagua unachooka kitakupa maisha mazuri baadaye
 
Back
Top Bottom