Moto wa kisasi unawaka ndani yangu!

Moto wa kisasi unawaka ndani yangu!

Ednatha

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
489
Reaction score
666
Salam wanaJF! Ni mwaka mmoja tangu baba yangu auawe kikatili,lilikuwa tukio baya,lililoniumiza sana. Kilichoniumiza sana sio kifo chake, kwa kuwa najua fika kuwa kila nafsi itaonja mauti,kilichoniumviza ni swali la kwanini wamuue kikatili kiasi kile? Namshukuru Mungu nilifarijika kuona wauaji wakikamatwa na kuwekwa rumande. Katika hali ya kushangaza wauwaji wale wameachiwa jana ikiwa ni siku chache kabla ya "deathdate" ya baba yangu mpendwa! Wauaji na familia zao wamefanya karamu kubwa ya ushindi! Mpaka sasa nashindwa kuelewa wameachiwa vipi ili hali kuna mashahidi walioshuhudia tukio hilo? Wameachiwa vipi wakati kesi haijasilizwa hata siku moja? Je,wameachiwa kwa dhamana? Tangu lina kesi ya mauaji ikawa na dhamana? Kuachiwa kwao kumeamsha uchungu wa msiba upya, mama yangu na wadogo zangu wanalia sana.Nina uchungu mwingi sana kiasi cha kuona kuwa napaswa kulipa kisasi kwa mkono wangu mwenyewe,kwasababu nilitegemea sheria itachukua mkondo wake lakini nimedhihirisha kuwa HAKUNA HAKI DUNIANI,nikisema nimwachie Mungu naona kwa MUNGU MBALI! Wadau nishaurini cha kufanya,kwani roho ya kisasi imeshanivaa.
 
Piga chini songambele na mambo yako binafsi Mungu atawalipia.
 
Lipiza tu wala hapo hakuna kuuliza mtu. mimi pia nasubiri hukumu ya muuaji wa mtoto wa dadangu aliuawa kikatili na watu watatu sasa baada ya upelelezi kufanyika polisa wakawafundisha watuhumiwa na kusema wajichague mmojawao aseme kuwa mimi nimeua peke yangu hawa wenzangu wamesingiziwa. baada ya hapo wawili waliruhusiwa na amebaki mmoja nasubiria itakuwaje
 
pole mkuu
achana na mawazo ya kisasi kabisa
songa mbele....kisasi hakitakusaidia chochote..kinaweza kuharibu maisha yako mwenyewe

The Heart that forgives is strong
dont be weak.....they will pay in due time...in same way or the other...keep calm..and move on mkuu
 
Mkuu, ni sababu zipi zilipelekea hao watu kufanya hayo mauaji?
 
Relax Bro, MUNGU atadili nao tu na ninakuhakikishia hutakufa kabla ya kuona maajabu ya MUNGU juu yako, atawatenda jambo na wewe utaishia kufurahi. Relax, Please Relax najua how painful it is, najua sana but tulia ili upate the best solution, tulia nakuomba sana
 
2.jpgSamahani bro unajua kutumia hii kitu?
 
pole mkuu
achana na mawazo ya kisasi kabisa
songa mbele....kisasi hakitakusaidia chochote..kinaweza kuharibu maisha yako mwenyewe

The Heart that forgives is strong
dont be weak.....they will pay in due time...in same way or the other...keep calm..and move on mkuu

mhh unaujua uchungu wa kuuliwa baba yako?...
Sijui mtoa mada ana uchungu kiasi gani,nampa poleh..lakini nikijaribu kujiweka in his shoes,mhhhh...i can't imagine,
kusamehe is easier said than done
 
pole sana mkuu japo hujaeleza ukatili wa kifo chenyewe lakini vifo vya kikatili ama hakika vinaumiza sana!
mkuu yaliyopita yamepita kilichobaki muachie mungu we ganga na yajayo.
 
Jifunze kusamehe though inauma mkuu!!

There is lot to enjoy in life!
 
Kabla hujalipiza kisasi jua kuwa kisasi hakina mwisho. Mtamalizana familia zote hamna atakae kubali kushindwa, cha msingi fuata utaratibu ujue wametokaje tokaje ukizingatia kesi haijafika hata mahakamani though kufika mahakamani hakugurantee wao kufungwa ama kunyongwa hiyo itategemea na ushahidi.

Ila kisasi si kitu kizuri, nguvu unayotaka kutumia kulipa kisasi itumie kupata haki unayoona unastahili kuipata
 
Mkuu, ni sababu zipi zilipelekea hao watu kufanya hayo mauaji?

Hilo nalo muhimu kufahamu inawezekana na wao walikua wanalipa kisasi. Kwahiyo na yeye akiendeleza kulipa kisasi ni watauana mpaka mwisho wa dunia kama upo
 
Aiseee. Kaa chini punguza hasira. Ukishalipa kisasi hta hivyo baba yako hatarudi sana sana utakuwa umemkosea Mungu na wewe na kujiingiza kwenye matatizo zaidi.

Jua lolote utakalofanya la kulipa kisasi mkono wa sheria utakutafuta na kukupa haki yako stahili badala ya kupunguza uchungu utakuwa umeongeza uchungu mara mbili. Pia utakuwa umeongezea familia yako matatizo zaidi.

UFANYE NINI BASI

1. Samehe kabisa.

Ukisamehe na kuachilia huo uchungu wote moyoni utaisha na kusonga na maisha

2. Kuwa mtu wa ibada.

Kama mkristo soma sana neno la Mungu kufanya maombi kwa bidii utapata faraja ya. kweli

3. Kaa karibu na watumishi wa Mungu wakuombee itasaidia sana kuvunja hiyo roho ya kisasi ndani yako.

4. Focus kwenye kazi zako zaidi. Fanya kwa bidii zaidi usiruhusu hiyo roho kukutawala itakurudisha nyuma kimaendeleo.

5. Usipende kujitenga tenga kwenye hiki kipindi. Jaribu ku-socialize na wenzako. Kama michezo fanya au chochote kile halali kitakachoifurahisha nafsi yako ukiwa na wenzako

Kumbuka kisasi huwa analipa Mungu na siyo mwanadanu. Ukifanya vyema Mungu atawalipieni kisasi kwa haki.
 
najua ana maumivu makali sana yasiyo na mfano...ila kisasi sio suluhisho..watalipa tu kwa wakati wao..na yatakua malipo ya aibu.....malipo hapahapa...mbinguni hesabu
mhh unaujua uchungu wa kuuliwa baba yako?...
Sijui mtoa mada ana uchungu kiasi gani,nampa poleh..lakini nikijaribu kujiweka in his shoes,mhhhh...i can't imagine,
kusamehe is easier said than done
 
Back
Top Bottom