Moto wa kisasi unawaka ndani yangu!

Moto wa kisasi unawaka ndani yangu!

Salam wanaJF! Ni mwaka mmoja tangu baba yangu auawe kikatili,lilikuwa tukio baya,lililoniumiza sana. Kilichoniumiza sana sio kifo chake, kwa kuwa najua fika kuwa kila nafsi itaonja mauti,kilichoniumviza ni swali la kwanini wamuue kikatili kiasi kile? Namshukuru Mungu nilifarijika kuona wauaji wakikamatwa na kuwekwa rumande. Katika hali ya kushangaza wauwaji wale wameachiwa jana ikiwa ni siku chache kabla ya "deathdate" ya baba yangu mpendwa! Wauaji na familia zao wamefanya karamu kubwa ya ushindi! Mpaka sasa nashindwa kuelewa wameachiwa vipi ili hali kuna mashahidi walioshuhudia tukio hilo? Wameachiwa vipi wakati kesi haijasilizwa hata siku moja? Je,wameachiwa kwa dhamana? Tangu lina kesi ya mauaji ikawa na dhamana? Kuachiwa kwao kumeamsha uchungu wa msiba upya, mama yangu na wadogo zangu wanalia sana.Nina uchungu mwingi sana kiasi cha kuona kuwa napaswa kulipa kisasi kwa mkono wangu mwenyewe,kwasababu nilitegemea sheria itachukua mkondo wake lakini nimedhihirisha kuwa HAKUNA HAKI DUNIANI,nikisema nimwachie Mungu naona kwa MUNGU MBALI! Wadau nishaurini cha kufanya,kwani roho ya kisasi imeshanivaa.
Ukishindwa kusamehe lipa kisasi.

Lakini Je, kwa sababu gani hasa baba yako aliuawa?
 
Jiridhishe kwanza na uchunguzi binafsi. Inaonekana kinachokuumiza ni tukio la kuuliwa mzazi wako,hujazingatia sababu zilizopelekea tukio hilo. Chunguza kwa makini,utapata jibu sahihi kuhusu kisasi.
Absolutely true.

Kwa Nini hao Watu waachiwe huru?
Kwa Nini Kesi haikusikilizwa hata siku moja? Kuna kitu kipo nyuma ya pazia jeusi, siyo bure hata kidogo.
Achunguze kwanza kwa kina kuhusu sababu zilizopelekea baba yake kuuawa.
Huenda pengine yeye ndiye alikuwa chanzo Cha kuuawa kwake
 
Salam wanaJF! Ni mwaka mmoja tangu baba yangu auawe kikatili,lilikuwa tukio baya,lililoniumiza sana. Kilichoniumiza sana sio kifo chake, kwa kuwa najua fika kuwa kila nafsi itaonja mauti,kilichoniumviza ni swali la kwanini wamuue kikatili kiasi kile? Namshukuru Mungu nilifarijika kuona wauaji wakikamatwa na kuwekwa rumande. Katika hali ya kushangaza wauwaji wale wameachiwa jana ikiwa ni siku chache kabla ya "deathdate" ya baba yangu mpendwa! Wauaji na familia zao wamefanya karamu kubwa ya ushindi! Mpaka sasa nashindwa kuelewa wameachiwa vipi ili hali kuna mashahidi walioshuhudia tukio hilo? Wameachiwa vipi wakati kesi haijasilizwa hata siku moja? Je,wameachiwa kwa dhamana? Tangu lina kesi ya mauaji ikawa na dhamana? Kuachiwa kwao kumeamsha uchungu wa msiba upya, mama yangu na wadogo zangu wanalia sana.Nina uchungu mwingi sana kiasi cha kuona kuwa napaswa kulipa kisasi kwa mkono wangu mwenyewe,kwasababu nilitegemea sheria itachukua mkondo wake lakini nimedhihirisha kuwa HAKUNA HAKI DUNIANI,nikisema nimwachie Mungu naona kwa MUNGU MBALI! Wadau nishaurini cha kufanya,kwani roho ya kisasi imeshanivaa.
Pole
 
Hao mbwa maliza mmoja mmoja. Kama mtu anafanya kosa kubwa la jinai kama kuua na sheria inashindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Basi hiyo sheria haina kazi na kama haina kazi basi sheria hakuna tena. Kinachobaki ni kuchukua hatua mkononi kwako. Kama wao walitoka, na wewe ungetoka. Kama usingetoka haijalishi sababu tayari wao washapata wanachostahili.

Kama hicho ni kigumu sana basi ungesoma sheria au ungeingia jeshini. Lakini kamwe usingewasamehe. Adhabu ya kifo ni kifo kama hakuna sheria.
 
Back
Top Bottom