ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,956
- 7,005
Nakukaribisha kwenye last supper
![]()
Na the best supper should be rost ya nguruwe na ndizi. Hapo shushia na sparleta baridi au mirinda nyeusi
Nakukaribisha kwenye last supper
![]()
Salam wanaJF! Ni mwaka mmoja tangu baba yangu auawe kikatili,lilikuwa tukio baya,lililoniumiza sana. Kilichoniumiza sana sio kifo chake, kwa kuwa najua fika kuwa kila nafsi itaonja mauti,kilichoniumviza ni swali la kwanini wamuue kikatili kiasi kile? Namshukuru Mungu nilifarijika kuona wauaji wakikamatwa na kuwekwa rumande. Katika hali ya kushangaza wauwaji wale wameachiwa jana ikiwa ni siku chache kabla ya "deathdate" ya baba yangu mpendwa! Wauaji na familia zao wamefanya karamu kubwa ya ushindi! Mpaka sasa nashindwa kuelewa wameachiwa vipi ili hali kuna mashahidi walioshuhudia tukio hilo? Wameachiwa vipi wakati kesi haijasilizwa hata siku moja? Je,wameachiwa kwa dhamana? Tangu lina kesi ya mauaji ikawa na dhamana? Kuachiwa kwao kumeamsha uchungu wa msiba upya, mama yangu na wadogo zangu wanalia sana.Nina uchungu mwingi sana kiasi cha kuona kuwa napaswa kulipa kisasi kwa mkono wangu mwenyewe,kwasababu nilitegemea sheria itachukua mkondo wake lakini nimedhihirisha kuwa HAKUNA HAKI DUNIANI,nikisema nimwachie Mungu naona kwa MUNGU MBALI! Wadau nishaurini cha kufanya,kwani roho ya kisasi imeshanivaa.
UPDATES:
Asanteni sana wadau,kwa kunifariji/kunitia moyo na kunishauri. Kuna watu wamehoji source ya mauaji,ni kwamba kulitokea mgogoro wa ardhi kati ya mzee na wauaji,mgogoro uliopelekea kwenda baraza la ardhi la kata,hukumu iliwapa ushindi wauaji.Mzee akakata rufaa baraza la ardhi la wilaya likampa ushindi mzee. Wauaji wakakata rufaa baraza la ardhi mkoa,huko nako mzee akashinda kesi!
NOTE: nawaita wauaji kwakua,mdogo wangu alishuhudia tukio la mauaji na aliwaona.
there is no murder which happen without leaving tracesKama umepanga kulipa kisasi,u have to learn on how to comit a perfect murder,usiruhusu hasira zikakuongoza,mwisho wake unaweza usitimize lengo lako.In order to perform a perfect murder u must ensure the absence of physical evidance.
pia unaweza mwachia Mungu akakulipia kisasi..Kwani unapomua mtu unayemjua ni rahis sana kugundulika,kwani polisi uwa wanajua wapi pa kuanzia.Hata kama mda wa tukio we utakuwa mbali na eneo hilo kwani upelelezi wao utaanzia na kuonanisha mambo.
Aliuwawa mwezi May 2013,tuna mashahidi 5 , nilisoma maelezo ya mashahidi,source ya mauaji ni mgogoro wa ardhi.
Mimi sipo mkuu!
Ubarikiwe sana , mwenye thread please I beg you to follow this. Na kamwe hutojutia uamuzi wako.Mkuu Ndohu kwanza pole sana kwa yaliyokupata.
Kwanza nikuhakikishie kuwa uchungu ulio nao mimi pia nilishaupitia na unaishilia kwa sasa.
Wazazi wangu(baba na mama) waliuwawa pia kikatili sana. Vyombo vya usalama wakiwemo maafisa wajuu walitufuata wakatuuliza kama tungependa wafanyeje kuhusu muuaji. Tunamshukuru MUNGU wazazi walitulea kimaadili ya dini kwa kiasi kikubwa.Kuna kipindi nakumbuka tukiwa tunasali jioni walituhubiria kuhusu kusamehe(ilikuwa ni utaratibu kusali kila asubuhi na jioni).
Kwahiyo sisi kama watoto wa marehemu tulijitenga pembeni kwa siku kadhaa tukamwomba MUNGU atupe namna katika hili na baadae tukashauriana kwa kina. Kila mtoto akakubali kwa roho safi kabisa kuwa TUSAMEHE yote na kamwe hatutakuwa na haja ya kumwona muuaji.Hivyo ndivyo tulivyowajibu pia vyombo vya usalama.
Tulifanya hivyo tukiamini kuwa
1. MUNGU kama alikubali roho zao ziache miili yao basi anajua namna ya kushughulika na muuaji.
2. Pili MUNGU ana namna nzuri ya kumuadhibu yeyote anayetoa roho ya kiumbe wake pasipo sisi wafiwa kudhurika kiroho wala kimwili.
3. Tungelipa kisasi sisi isingeturudishia wazazi wetu na pia ingezidi kutukumbusha machungu kila leo tunapokuwa kwenye kesi au kuonana na familia ya muuaji.n.k
4. Tusingewafurahisha wazazi wetu huko walipo kwa kuwa kwa wao suala la kusamehe wao lilikuwa ni kanuni kuu ya maisha yao.Hivyo tuna hakika wamefurahi kuona kuwa TULISAMEHE.
5. Tungejichumia dhambi za bure ambapo pengine zingeandama na vizazi vyetu kwa jambo ambalo hatuna uwezo nalo.
Mpaka leo naamini muuaji alihudhuria msiba wa wazazi wetu na alishuhudia machungu aliyotusababishia na kwa vyovyote vile ataishi na machungu hayo milele.
USHAURI:
Masuala haya hutegemea sana KIWANGO CHA IMANI ya mtu na jinsi mtu anavyoyachukulia mambo anayokutana nao.
Kama unaamini kisasi kitawapa faraja na kufanya mioyo yenu ITULIE na KURIDHIKA kabisa basi fanya kisasi huku ukiwa na UHAKIKA PASIPO SHAKA kuwa hao jamaa ndio waliomuua baba yako.
Kama huna uhakika usiingie KAMWE kwenye huo mtego.
Amin nakwambia furaha yao na kupongezana kwao ni kwa muda tu.
kisasi si njia nzuri ya kufurahisha moyo wako... ingawa kuna baaddhi ya imani kisasi kwao si dhambi..think twice mkuu.Lipiza tu wala hapo hakuna kuuliza mtu. mimi pia nasubiri hukumu ya muuaji wa mtoto wa dadangu aliuawa kikatili na watu watatu sasa baada ya upelelezi kufanyika polisa wakawafundisha watuhumiwa na kusema wajichague mmojawao aseme kuwa mimi nimeua peke yangu hawa wenzangu wamesingiziwa. baada ya hapo wawili waliruhusiwa na amebaki mmoja nasubiria itakuwaje
AMIN.Ubarikiwe sana , mwenye thread please I beg you to follow this. Na kamwe hutojutia uamuzi wako.
Nawashukuru wote mlionishauri,mlionifariji na kuniombea;sina cha kuwalipa ila MWENYEZI MUNGU atawalipa! Ushauri wenu,dua zenu na maombi yenu hakika yamezima moto wa kisasi uliokuwa ndani yangu. Ukweli ni kwamba niliumia sana ila nimeamua kumwachia Mungu, kama wengi wenu mlivyonishauri kwani naamini kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu! Nilifuatilia mahakamani kujua kilichosababisha kuachiwa kwao,nimebaini mazingira ya rushwa ya wazi kabisa,hivyo kuna hatua za kisheria tumeamua kuzifuata japo this time tunafuatilia tukijua fika kuwa duniani hakuna haki!
Aidha nawashukuru pia wale wote walionishauri kulipa kisasi kwani naamini kuwa walinishauri vile kwa kuwa waliguswa na mkasa huu!
Hongera kwa kukubali ushauri wa kusahau yaliyopita..tulia mumtunze,mumlee na kumfariji mama yenu ambaye sasa ni mjane..kulipiza kisasi kungemletea maumivu mapya kwani ungelazimika kukimbia au ungekamatwa na kupelekwa jela..chukua muda utazoea.Nawashukuru wote mlionishauri,mlionifariji na kuniombea;sina cha kuwalipa ila MWENYEZI MUNGU atawalipa! Ushauri wenu,dua zenu na maombi yenu hakika yamezima moto wa kisasi uliokuwa ndani yangu. Ukweli ni kwamba niliumia sana ila nimeamua kumwachia Mungu, kama wengi wenu mlivyonishauri kwani naamini kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu! Nilifuatilia mahakamani kujua kilichosababisha kuachiwa kwao,nimebaini mazingira ya rushwa ya wazi kabisa,hivyo kuna hatua za kisheria tumeamua kuzifuata japo this time tunafuatilia tukijua fika kuwa duniani hakuna haki!
Aidha nawashukuru pia wale wote walionishauri kulipa kisasi kwani naamini kuwa walinishauri vile kwa kuwa waliguswa na mkasa huu!