"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

Mwanakijiji, do you have an axe to grind in this? Maana unamtetea sana Mengi aisee....

yeah.. I have been here before... kwenye suala la Amina na Zitto.. I stand on my principle. The Principle ambayo I have articulated masterfully before. Ni principle ile ile ya kuwatetea kina Nsia, na wenzao.

Katika hili sina hofu ya kumtetea mtu yeyote awe a sworn enemy or a loyal friend.
 
Inabakia pale pale, ikiwa baada ya uchunguzi itabainika magazeti yaliandika uongo:

- Basi yatashusha hadhi kwa kuandika udaku na ana haki ya etc etc
- Kama yameandika ukweli na ushahidi utathibitisha basi Mengi atakuwa Muongo na Mnafiki. Sifa ambazo hazifai kwa kiongozi.
Sasa hapa kitu gani kinabakia pale pale.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu come on now, kwa lugha yako kibongo bongo tunasema una maana Lilian ni Kicheche tu kama wengine wanaopita..
Trust me, Mwanakijiji sisi wote tumepitia Uhuni lakini ktk Umri huu ni vigumu sana kupiga picha na mwanamke chumbani hasa akiwa girlfriend tu ambaye huna mbele naye, kwa sababu picha ni kumbukumbu ambayo siwezi kuikana kesho..

Ok lets say sii mkewe, na hawajafunga ndoa na waliyoyafanya yote wameyafanya kwa mapenzi yao, then kwa nini hili neno NDOA limekuwa big deal wakati ndio sifa kubwa ya mwisho ktk relation yoyote!..
Kama ningekuwa mimi ningefurahi sana na kucheka kuwa waandishi wa habari wamepotea maboya!...wamenipa hadhi ya ndoa kumbe mimi kama mkristu wa kweli napiga vitu bila kutiwa maji!..
Na hakika ningetegemea Mengi angekuja na kukubali tu hiyo relation badala ya kubishana na waandishi wakati Lilian mwenyewe anakaa nyumbani kwake..Kwa sisi waswahili tutasema Mengi anafanya Uhuni, mtu mzima ukipenda vuta ndani kabisa, na uwekewe ubani maanake kuna vijana huko nje kina Masha!... haaa haa haa! na sio kumpa mtu ufunguo wa nyumba wakati ni hawala tu, ndio desturi na tamaduni yetu..

Ndio maana nikasema pengine anachokataa ktk taarifa zote ni Ufisadi na ndoa imepachikwa tu kwa sababu mengi yamezungumzwa ktk ndoa hiyo yamehusisha zaidi Ufisadi kuliko ndoa yenyewe.. Au pengine anachokataa ni kufungishwa ndoa na huyo Mkuu wa wilaya wakati kaifunga kanisani - who knows!
 
Mwanakijiji,

Nani kakwambia ya kuwa Harusi zote Tanzania lazima zifungwe kwa mkuu wa wilaya ?
 
Sawa;



Sawa; Unaposema "mtoto" unamaana ya mpenzi wake na siyo mtoto kwa maana ya umri au uwezo wa kiakili, i presume;




Sidhani kama umeona mahali ambapo Mengi kazikana hizo picha au kulalamika kuchukuliwa picha na mpenzi wake. Kama alitaka kupiga picha na mtu anayempenda ambaye kwa maneno yake watu tayari wanajua, how would that tarnish his image? Kama watu walikuwa wanajua tayari kuwa yuko na Lilian, kwa jinsi gani picha zitaongeza kitu tofauti ya kile ambacho tayari kinajulikana.

Mimi nilikuwa najua and so many other people knew about this relationship. Nilipoona picha nikasema "wamependeza"! Ilinibadili mawazo yangu juu yao not really just confirmed to me that love is sometimes stronger than magnet.. na inaweza kukufanya ufanye things deemed to be unconventional.



Si mkewe lakini pia si dadake! Nimeziangalia na kuona ni watu wawili wenye akili timamu, watu wazima na ambao wana haki ya kufanya kile ambacho wao wawili wamekubaliana kufanya.



Kwanini unasema kujirahisisha; kaamua kufuata kile anachotaka kwa mapenzi yake mwenyewe akiwa na akili timamu akijua kuwa amewahi kuolewa na mengi amewahi kuoa na wote wawili wanawatoto na wenzi wengine. Hivi kweli unafikiri Mengi na Lilian hawakujua hayo yote hadi wakakubaliana mapenzi au ni mimi na wewe ndiyo tumegundua hilo?





Habari kwamba yuko Lilian (ambazo umesema tayari zinajulikana) au habari kuwa amepiga picha chumbani akiwa na Lilian, au kwamba habari kuwa yeye hajafunga ndoa rasmi na Lilian kitu ambacho hakijajulikana? Maana kama ni image imeshachafuka, sijui anaweza kuichafua vipi zaidi.

kwamba akae kimya na kuendelea kuzushiwa au kudaiwa mambo ambayo ukweli wake ni rahisi kuupata.


Nagundua mzee yuko makini katika kucheza kati ya kanisa (mke mmoja tu babuu) na real life (Nyege haina adabu).

Mzee ana"masquerade" behind a mask...Mtoto amechukua lakini hajaoa 🙂 Hii sio marriage na sio de facto marriage.

Tatizo liko upande wa kanisa tu kwa sisi wengine haina matatizo.

"Catholics who do not marry according to the laws of the Church exclude themselves from the right to receive Eucharist until they have corrected their situation according to the Church."
 
Mwanakijiji,

Nani kakwambia ya kuwa Harusi zote Tanzania lazima zifungwe kwa mkuu wa wilaya ?

harusi zote zote Tanzania lazima ziandikishwe na Msajili wa Ndoa. Na katika sheria ya ndoa, ndoa si ndoa hadi iwe imefungishwa na mtu anayekubalika kisheria kufungisha ndoa.

Katika hili utaona kuwa imetajwa aliyefungisha ndoa ni Mkuu wa Wilaya siyo maneno yangu. Hivyo, huyo Mkuu wa Wilaya anayetajwa ndiye anaweza kusema alifungisha ndoa au la, ama sivyo?
 
Nagundua mzee yuko makini katika kucheza kati ya kanisa (mke mmoja tu babuu) na real life (Nyege haina adabu).

Mzee ana"masquerade" behind a mask...Mtoto amechukua lakini hajaoa 🙂 Hii sio marriage na sio de facto marriage.

Tatizo liko upande wa kanisa tu kwa sisi wengine haina matatizo.

"Catholics who do not marry according to the laws of the Church exclude themselves from the right to receive Eucharist until they have corrected their situation according to the Church."


Well.. ni mtu mzima ana akili timamu na mwanamke ni mtu mzima na akili timamu, unless tunataka kuwa maaskari wa ndoa! Kama kanisa lake au dini yake haimkemei kama anajua anachofanya ni kinyume na dini yake hilo suala ni la mimi na wewe?
 
- Ninaomba kusema mara moja tu, wakuu what is this? JF Where we dare! Tukiweka topic zinazomhusu Mengi zinafutwa, lakini akiweka flani hazifutwi. Wiki mbili zilizopita niliweka topic ya kuuliza swali kama kweli Tetesi niliyosikia kwa kuonyeshwa picha ni kweli kwamba Mengi ameoa? Ile tpic ikafutwa, sasa leo inaletwa topic ya kumsafisha Mengi na habari ile ile, ila kwa kuwa imeletwa na wenye nguvu inaachwa, hata bila ya kuhamishwa leave alone kufutwa, this is JF where we dare to talk openly!

- Tunalia hapa kila siku jinsi viongozi wetu wanavyotufanya wananchi wajinga, lakini here we are na the semo semo stuff, lakini tunategemea viongozi wa taifa watu-treat tofauti na sisi wenyewe tunavyojiongoza hapa, is that so?, sasa with all respect naomba kuwauliza mnaohusika hivi sisi wanachama wengine wa hii forums kuacha nyinyi wachache au wengi, mnatuonaje hasa? Kama nilivyosema majuzi my status hapa JF na nje ya hapa inanizuia mara kwa mara kutosema yanayonishangaza hapa JF kuhusiana na utawala wa JF, lakini sasa mlipofikia mnaenda mbali mno wakuu, sisi wengine sio watoto wadogo wa kuchezewa vichwa vyetu namna hii, I mean what is this na Mengi na hii forums?

- Wakuu stop this madness ya kutufanya wengine wajinga hapa, hamuwezi kuwa mnafuta wengine wakiandika kuhusu Mengi, halafu wengine mnaruhusu that is foolish. Mengi ni nani hasa tufikie kudhalilishwa namna hii hapa JF? With all due respect kwa Mengi, ambaye ninamfhamu sana kuliko wengi hapa wanavyjidai naye please mzee tupe heshima kidogo, tunakuheshimu sana na mchango wako wka taifa on vita vya mafisadi, binafsi I worked so hard kukusadia sana kwenye vita vyako na Manji, behind the scene and you know that kwa sababu nilijua mapema sana kwamba jamaa wanakutafuta na ishu ya treason, ninajua all the things you are doing katika vita hivi na ni nani unaoshirkiana nao, lakini nakuomba sana mzee basi tuachie hapa nafasi either tukuajdili kwa kila ishu na sio unazotuamulia tu, au tusikujadili kabisa lakini kutuchezesha vichwa namna hii sio haki, kwa sababu hatuwapendi mafisadi kutokana na tabia kama hizi tunazofanyiwa na ishu zako hapa JF.

- Watu wangapi wazima wameoa, kuanzia wananchi wa kawaida mpaka viongozi, sasa what is a big deal na wewe kuoa au kutokuoa kwamba inabidi tuache ishus muhimu za taifa kujadili wewe this time na ishu kama hizi za ndoa? What is this ndugu zangu hapa JF? Mwinyi, Kikwete mbona tumewahi kuambiwa wameoa na hakuna aliyejali, sasa kwa nini kwako iwe tatizo namna hii mpaka tunafikia mahali pa kuacha kujadili taifa, sasa inakua ndoa ya Mengi kama ipo au haipo, kweli mzee wangu unaona hii ni fair kwetu wananchi wanyonge?

Kwa kweli haya mambo yanakatisha tamaa sana, unajaribu kuheshimu watu hapa na nje ya hii forums lakini in return wanakushangaza, kweli tumeacha ishus tunapoteza all this pages na this? na wala hii topic haifutwi wala kuhamiwshwa, haya wenye nguvu ngoja tuwapishe, endeleeni kutushangaza wakuu wenye nguvu humu ndani,

- eti kweli ndio tukipewa taifa tutafanya mambo tofauti na walioko sasa madarakani? Ndugu zangu umasikini ni kitu kibaya sana.

Mungu Aibariki Tanzania na JF Pia.
 
Nimesema mwanzoni na nitaendelea kusema , Mengi ameonyesha sio mtu makini katika hizi picha . Tatizo ni kuwadate watoto wadogo , ingekuwa ni mtu mzima mwenzake hizi picha zisingevuja. Hizi picha zimemwondelea kabisa credibility kama mzungumzaji wa masuala ya ukimwi.
 
Hakuna tatizo Mengi kuoa au kuishi na mwanamke ampendae. Yule dada ana watoto wake na Mengi ana watoto wake. Wote ni matured individuals. Hakuna kosa alilofanya kikatiba, tatizo ni kwamba anataka kuwa Church guy na hapo hapo anataka mambo ya kidunia. Ni mtu mkubwa na nina uhakika kanisa wataangalia upande mwingine kuliko kumkaripia kama mfano kwa young Christians:


"The Sacrament of Marriage is a sign of God's love for humanity and Christ's love for the Church. Couples who cohabit (that is, who live together in a sexual relationship when not married), have not formally pledged themselves to these values, nor has the Catholic Christian community formally committed itself to supporting the couple. Lacking a public acknowledgment, the community cannot be sure of the couples' intentions. Such a couple cannot sacramentally model God's love for humanity and Christ's love for the Church. Therefore, the Church doesn't approve of cohabitation, nor see it as a fitting or appropriate preparation for marriage."

Binafsi ningefuata moyo wangu kama Mengi alivyofanya
 
Mzee Mwanakijiji said:
The Principle ambayo I have articulated masterfully before.

Here you sound more like the Professor...lol...eti ni principle ambayo umei-articulate "masterfully"....Lol

Ni principle ile ile ya kuwatetea kina Nsia, na wenzao.

Nsia yule wa kule sehemu sehemu?....I hope hujamwandikia kumwomba aache anachokifanya "masterfully"...

Katika hili sina hofu ya kumtetea mtu yeyote awe a sworn enemy or a loyal friend.

I hope you will stick up for me one day if I'm in deep s#!&t....
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu come on now, kwa lugha yako kibongo bongo tunasema una maana Lilian ni Kicheche tu kama wengine wanaopita..

Hapana sina maana hiyo, kwani siwezi kuwa na maana hiyo.

Trust me, Mwanakijiji sisi wote tumepitia Uhuni lakini ktk Umri huu ni vigumu sana kupiga picha na mwanamke chumbani hasa akiwa girlfriend tu ambaye huna mbele naye, kwa sababu picha ni kumbukumbu ambayo siwezi kuikana kesho..

Sidhani kama nyinyi nyote mmepitia uhuni, wengine hatujapitia uhuni. Lakini na wengine wana magirlfriend wao wanaoishi nao kama wake zao na wanapiga nao picha kila kukicha na nyumbani hawa wanaitwa hadi "wake"!

Ok lets say sii mkewe, na hawajafunga ndoa na waliyoyafanya yote wameyafanya kwa mapenzi yao, then kwa nini hili neno NDOA limekuwa big deal wakati ndio sifa kubwa ya mwisho ktk relation yoyote!..

Kuna watu wanaamini katika ndoa na kuna watu wamewahi kuwa katika ndoa na hawaamini katika ndoa tena wanafurahia maisha yao wapendavyo. Well, tunayo haki ya kuwalazimisha waoane kwa sababu sisi tunaamini ni 'sifa kubwa ya mwisho katika relation yoyote".


Kama ningekuwa mimi ningefurahi sana na kucheka kuwa waandishi wa habari wamepotea maboya!...wamenipa hadhi ya ndoa kumbe mimi kama mkristu wa kweli napiga vitu bila kutiwa maji!..

kuukubali uongo kwa sababu unampatia mtu sifa njema ni kuupa uongo hadi isiyostahili.

Na hakika ningetegemea Mengi angekuja na kukubali tu hiyo relation badala ya kubishana na waandishi wakati Lilian mwenyewe anakaa nyumbani kwake..

Sisi wewe ungetemea kama nani kwa upande wa Mengi? Tusema unawakilisha maslahi ya nani? Mimi binafsi nakubaliana na wewe kuwa kama wangeweza kufunga ndoa ingekuwa vyema, but for who? Ndipo hapo ninakwama. Kwamba wafunge ndoa waniridhishe mimi, wewe, kanisa, dini, mungu, au mioyo yao?

Lakini jingine ni kuwa hawa tayari wameshawahi kufunga ndoa na zimewashinda!!
Kwa sisi waswahili tutasema Mengi anafanya Uhuni, mtu mzima ukipenda vuta ndani kabisa, na uwekewe ubani maanake kuna vijana huko nje kina Masha!...

Hivi hao waliofunga ndoa wote wamewazuia watu kama kina Masha? Au tunafunga ndoa ili kutimiza wajibu tu na kuwaridhisha wazazi. Si kwamba tunafunga ndoa kwa sababu tunaamini katika tunu hiyo na tunaamini katika nguvu ya upendo tulionao. NI kosa gani kama tunaamua kuwa rasmi bila kufunda ndoa nyingine?

haaa haa haa! na sio kumpa mtu ufunguo wa nyumba wakati ni hawala tu, ndio desturi na tamaduni yetu..

Hizi tamaduni nimeshakataa hapo nyuma kwa sababu tunazikimbilia pale zinapotufaa tu! Nakumbuka tulikuwa tunaooa mabikira, tulikuwa na jando na unyago..

Ndio maana nikasema pengine anachokataa ktk taarifa zote ni Ufisadi na ndoa imepachikwa tu kwa sababu mengi yamezungumzwa ktk ndoa hiyo yamehusisha zaidi Ufisadi kuliko ndoa yenyewe.. Au pengine anachokataa ni kufungishwa ndoa na huyo Mkuu wa wilaya wakati kaifunga kanisani - who knows!

Point nzito hiyo! Kwa sababu nyuma ya haya ni mapambano dhidi ya ufisadi. Mafisadi wametusababisha tuanze kubishana juu ya ndoa na si ndoa ya Mengi kana kwamba ndicho kitu muhimu kwenye Taifa. Lakini upande mwingine tusipozungumzia tunawakubalia uongo wanaoeneza.
 
Here you sound more like the Professor...lol...eti ni principle ambayo umei-articulate "masterfully"....Lol

only you would catch that part! LOL


Nsia yule wa kule sehemu sehemu?....I hope hujamwandikia kumwomba aache anachokifanya "masterfully"...

hapana nimekuwa nawasiliana naye katika kumshauri masuala kadhaa.. you know some PR stuff!

I hope you will stick up for me one day if I'm in deep s#!&t....

Hilo wala lisikutie shaka as long as you are not making me break one principle in attempting to hold onto another!
 
it was a MASQUERADE BALL..sio BDAY PARTY OR HARUSI.
it was an exclusive invitees only event,nyumbani kwa bwana mengi kinondoni

only 100 people.
PARTY PLANNER FLEW IN FROM S.AFRICA,THE EVENT COSTED MILLIONS OF Tshillings.

NI KWELI MR MENGI ALIMTAMBULISHA LILIAN KIMARO AS HIS WIFE,NA WASHAVALISHANA PETE BUT NO PLANS FOR HOLDING A WEDDING FOR REASONS KNOWN TO EVERYONE......AMEOA ALREADY!!
Can anyone do that and get away with it?
 
Kwenye ile picha aliyotoa YO YO yule dada alikuwa amevaa ring mkononi , mimi naona kama ni wedding ring. Sasa kama ni hivyo na Mengi anapinga haikuwa harusi , basi mheshimiwa anatembea na mke wa mtu!
 
Soma gazeti la Tazama Tanzania linalomilikiwa na Karamagi, Lowasa &Co. la leo. Habari yake kubwa 'Chadema yang'oa wabunge 10 wa CCM. Ukisoma habari hiyo, imejaa uzushi wa dhahiri, inachefua na kutukana taaluma ya habari. unaweza kusoma hapa:MAGAZETI YA TANZANIA VIA KENNEDY: Chadema yang'oa wabunge kumi CCM

Kwakweli inakera sana, tumefikia pabaya.

Mkuu nimesoma hiyo habari hata kabla ya kuja hapa. kusema kweli kama waziri hatalichukulia hatua, basi tutajua kuna namna. wizimtupu! ni kiwango duni mno cha uandishi wa habari!
 
Mzee Mwanakijiji,
Sidhani kama nyinyi nyote mmepitia uhuni, wengine hatujapitia uhuni. Lakini na wengine wana magirlfriend wao wanaoishi nao kama wake zao na wanapiga nao picha kila kukicha na nyumbani hawa wanaitwa hadi "wake"!
Mkuu haya nakuomba unipe mfano wa mtu mzima yeyote mwenye hadhi ya Mengi amepiga hizo picha za chumbani na mpenzi wake kisha akazitoa hadharani...

Mkuu, kufikiria kuwa wapo watu ni tofauti sana na kufahamu kuwa wapo wanaopiga picha na wapenzi wao chumbani wakati kwanza sii mkewe halafu wewe hapo huna Umri wala nafasi kama ya Mengi. Ni fikra tu waulize wazee wako watakwambia...
 
TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa muda mrefu sasa, magazeti yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu. Kwa mfano:-

• Mengi anataka kumng'oa JK 2010?
• Mengi hatari kama Hitler
• Ndoa ya Reginald Mengi na CHADEMA yabainika
• Mengi na kashfa ya ufisadi – Tume ichunguze bilioni 40 za ukimwi.
• Mengi aoa tena – harusi yafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe

Taarifa zote hizi ni za uongo mtupu.

Kama nilivyokwishasema awali, mafisadi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma ambazo zingetumika kwa kujengea shule na kupiga vita maradhi na umaskini wamekuwa wanazitumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi kwa kujijengea majumba ya kifahari huko Dubai, Uswisi na Afrika ya Kusini, na kubwa zaidi, sasa wanazitumia kudhoofisha nguvu zinazopiga vita ufisadi.
Mafisadi hawa wameanzisha magazeti zaidi ya 15 ambayo yanasambaza fitina na uongo uliotungwa.

Nia na madhumuni ya mafisadi kutunga na kusambaza fitina na uongo ni kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.

Fitina na uongo wa mafisadi hawa ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani. Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Hadi hapo Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha (privacy) endapo waandishi wa habari wanaoheshimu taaluma yao ya kuandika ukweli wataandika uchafu wa maisha hayo, wasilalamike.

Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa. Hautazimika kamwe, na jitihada zao za kudhoofisha nguvu za vita dhidi ya ufisadi zitageuka kuwa kichocheo cha moto huo hata kama watafanikiwa kuwatokomeza watu wanaopiga vita ufisadi.
____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
10 Februari,2009


My Take:
Nashindwa kuelewa kwenye nchi ambayo ina sheria kali ya magazeti na ambapo watu wanaimba kila siku suala la maadili ya "kitanzania", kwanini tumefika hapa tulipofika? Waziri wa Habari ataendelea kukaa pembeni na kuangalia kusambaa huku kwa habari za kupakana matope hadi kwenye vitanda vya watu?

Nimeshasema huko nyuma nikimnukuu mwalimu wangu "ukivunja kanuni kubwa, kanuni hiyo itatafuta namna ya kukuvunja". Sasa magazeti kadhaa yanaanza kushindana kuandika nani anajua uchafu wa kiongozi gani zaidi na siku si nyingi hili litafika hadi kwa Rais, na mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kuwa ni fair target. Somebody got to stop this or as a people we ough to be prepared to pay a huge price for the silence we maintain.

yetu mashoo mweyekusubiri hacho tuome uhai
 
Kwenye ile picha aliyotoa YO YO yule dada alikuwa amevaa ring mkononi , mimi naona kama ni wedding ring. Sasa kama ni hivyo na Mengi anapinga haikuwa harusi , basi mheshimiwa anatembea na mke wa mtu!

tafsiri yako ni wewe umeona kuwa ni "wedding ring". Halafu kama anatembea na "mke wa mtu" huyo mwenye mke ndiye anatakiwa kulalamika au kufanya big deal, umewahi kumsikia akilalamika? Upande mwingine kwanini isiwe huyo dada anatembea na mme wa mtu?

Tatizo hapa ni kuwa tunassume wao hawajui maana ya mme au mke wa mtu au hawajui kuwa ndoa ni kitu gani hadi tuwakumbushe!
 
Back
Top Bottom