Mwan mpambanaji
JF-Expert Member
- Apr 3, 2008
- 482
- 131
Ni kweli nitaliwa,ila sitaliwa mwenyew,pia wasi wasi wngu mkubwa ni kuhusu watanzania walio wengi itakuaje?na je tutaliwa hadi lini?
Nani alifungisha ndoa?
Mpiga picha alishuhudia, labda nani aliyefungisha hiyo ndoa ya aina gani, kimila, kidini au kiserikali. Kama sivyo aseme kama picha zilikuwa za kutengeneza (photoshop) au ilikuwa party ya kusherehekea mwaka mpya.
Hata kama wana ndege hayamhusu ni za kwao mbona yeye anavyotumia brand za watu hatusemi ?? Radio 1 , itv si brand za watu wengine ? The gurdian si brand ya watu wengine ?? Kwanini asiwe mbunifu awe na vyake ??
Mpiga picha alishuhudia, labda alishuhudia na anajua nani aliyefungisha hiyo ndoa, na ni ya aina gani, kimila, kidini au kiserikali. Kama sivyo aseme kama picha zilikuwa za kutengeneza (photoshop) au ilikuwa party ya kusherehekea mwaka mpya.
Pili, sisi watanzania tunapenda sana story za udaku na kuongea mambo ambayo hatuna uhakika nayo.
Hahahahaaa..Bwana/ Bibi Skasuku, siyo wabongo tu wanaopenda mambo ya udaku na mambo ambayo hatuna uhakika nayo. Kupenda mambo hayo ni asili ya binadamu (human nature).
Unajua siku moja nilikuwa Publix kwenye foleni nikisubiri ku check out. Sasa nikaanza kusoma cover za yale magazeti yanayowekagwa kwenye lane ambazo watu hupanga foleni. Nikaona moja linadai eti Raisi Obama (then candidate Obama) ni gay na kuna picha ya mpenzi wake ndani kwenye ukurasa sijui wa ngapi....come on now....though I won't put it past anybody, does anybody really think Obama is gay?
Hivi unajua Bill na Hillary Clinton wamezushiwa mambo mangapi na haya magazeti ya udaku? Au hata marehemu Princess Di na mumewe Prince Charles?
Uzushi ni asili ya ubinadamu na hata upige marufuku magazeti au redio na luninga kutangaza udaku, huwezi kupiga marufuku watu kuongea.
Kuna mambo mengineambayo Mengi anayafanya ambayo yanaharibu kazi nzuri anazozifanya. Kuanzisha magazeti kwa ajili ya kuwashambulia walioanzisha magazti yanayomshambulia, si mfano wa kuigwa. Hii ni sawa na hadhithi ya kichaa aliyeiba nguo za jamaa aliyekuwa anaoga mtoni.
Najiuliza, kama Mengi ameamua kupiga vita ufisadi, kuna haja ya yeye kutafuta huruma ya jamii namna hii? Kama ni hivyo, atakuwa amejitolea nini? Ni kweli baadhi ya magazeti yake yamefanya kazi nzuri sana kupambana na mafisadi, namuunga mkono kwa hilo. Alipaswa kukumbuka kuwa kinachoafanywa na magzeti hayo ni ubomoaji mkubwa na wa uhakika kwa dhidi ya mafisadi kuliko cheap stories ambazo mafisadi walikuwa wanaweka kwenye magazeti yao dhidi kaye. Kuwaiga kufanya hivyo ni kujishushia hadhi na mimi binafsi nimeanza kupatwa na wasi wasi iwapo kweli Mengi anajua anachokifanya
Mheshimiwa Mwanakijiji,
Ujue mamluki wanafanikiwa kuiteka nyara hoja yako na kuweka crap...
Mimi naunga mkono vita dhidi ya mafisadi maana bila wao vijana wetu wengi wangepata elimu nzuri na kupunguza wimbi la vibaka mitaani.
pia naunga mkono juhudi zaa wanabodi mnaoweka nondo njema humu ndani ya baraza letu...
Ila nawashangaa wanaotoa mishipa ya shingo na kusema kuwa "KAMA KIONGOZI WA CCM KAFISADIKA NI YEYE WALA CHAMA HAKIKUMTUMA", ila hawathubutu kusema "KAMA MWANACHAMA WA CCM KASHINDA UCHAGUZI, HIYO NI YEYE WALA CHAMA HAKIKUMTUMA"....
Kwani mengi hana msemaji wake au ipp haina msemaji wake ? Au ni masuala binafsi ndio maana akaamua ajibu yeye binafsi ?
TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa muda mrefu sasa, magazeti yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu. Kwa mfano:-
Mengi anataka kumng'oa JK 2010?
Mengi hatari kama Hitler
Ndoa ya Reginald Mengi na CHADEMA yabainika
Mengi na kashfa ya ufisadi Tume ichunguze bilioni 40 za ukimwi.
Mengi aoa tena harusi yafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe
Taarifa zote hizi ni za uongo mtupu.
Kama nilivyokwishasema awali, mafisadi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma ambazo zingetumika kwa kujengea shule na kupiga vita maradhi na umaskini wamekuwa wanazitumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi kwa kujijengea majumba ya kifahari huko Dubai, Uswisi na Afrika ya Kusini, na kubwa zaidi, sasa wanazitumia kudhoofisha nguvu zinazopiga vita ufisadi.
Mafisadi hawa wameanzisha magazeti zaidi ya 15 ambayo yanasambaza fitina na uongo uliotungwa.
Nia na madhumuni ya mafisadi kutunga na kusambaza fitina na uongo ni kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.
Fitina na uongo wa mafisadi hawa ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani. Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Hadi hapo Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha (privacy) endapo waandishi wa habari wanaoheshimu taaluma yao ya kuandika ukweli wataandika uchafu wa maisha hayo, wasilalamike.
Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa. Hautazimika kamwe, na jitihada zao za kudhoofisha nguvu za vita dhidi ya ufisadi zitageuka kuwa kichocheo cha moto huo hata kama watafanikiwa kuwatokomeza watu wanaopiga vita ufisadi.
____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
10 Februari,2009
Shida nyengine ni kwamba waandishi uchwara ambao hata maadili hawajui ndiyo reporters wa magazeti yanayoasisiwa na vinara wa ufisadi,
huko Rwanda na Burundi waandishi aina hii ndiyo walipelekea vita na mauaji ya halaiki.....
Shime waandishi mnapoitwa kwenye confereces halafu mtoa mada ni fisadi basi apopolewe na viatu.
Mkuu mwanakijiji katika kukujibu ni kwamba hilo gazeti lilipaswa kufutwa na si kufungiwa...