"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Moto umewawakia, hawawezi kuuzima" - Mengi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 10, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI

  Kwa muda mrefu sasa, magazeti yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu. Kwa mfano:-

  • Mengi anataka kumng'oa JK 2010?
  • Mengi hatari kama Hitler
  • Ndoa ya Reginald Mengi na CHADEMA yabainika
  • Mengi na kashfa ya ufisadi – Tume ichunguze bilioni 40 za ukimwi.
  • Mengi aoa tena – harusi yafungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe

  Taarifa zote hizi ni za uongo mtupu.

  Kama nilivyokwishasema awali, mafisadi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma ambazo zingetumika kwa kujengea shule na kupiga vita maradhi na umaskini wamekuwa wanazitumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi kwa kujijengea majumba ya kifahari huko Dubai, Uswisi na Afrika ya Kusini, na kubwa zaidi, sasa wanazitumia kudhoofisha nguvu zinazopiga vita ufisadi.
  Mafisadi hawa wameanzisha magazeti zaidi ya 15 ambayo yanasambaza fitina na uongo uliotungwa.

  Nia na madhumuni ya mafisadi kutunga na kusambaza fitina na uongo ni kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.

  Fitina na uongo wa mafisadi hawa ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani. Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.

  Wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu mno. Hadi hapo Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha (privacy) endapo waandishi wa habari wanaoheshimu taaluma yao ya kuandika ukweli wataandika uchafu wa maisha hayo, wasilalamike.

  Ninarudia tena kusema kwamba ni lazima mafisadi waelewe kwamba kutapatapa kwao ni jitihada za wafamaji kwa sababu moto wa vita dhidi yao umekwishawaka na hawawezi kuuzima au kuukwepa. Hautazimika kamwe, na jitihada zao za kudhoofisha nguvu za vita dhidi ya ufisadi zitageuka kuwa kichocheo cha moto huo hata kama watafanikiwa kuwatokomeza watu wanaopiga vita ufisadi.
  ____________________
  Reginald A. Mengi
  Mwenyekiti Mtendaji
  IPP Limited
  10 Februari,2009


  My Take:
  Nashindwa kuelewa kwenye nchi ambayo ina sheria kali ya magazeti na ambapo watu wanaimba kila siku suala la maadili ya "kitanzania", kwanini tumefika hapa tulipofika? Waziri wa Habari ataendelea kukaa pembeni na kuangalia kusambaa huku kwa habari za kupakana matope hadi kwenye vitanda vya watu?

  Nimeshasema huko nyuma nikimnukuu mwalimu wangu "ukivunja kanuni kubwa, kanuni hiyo itatafuta namna ya kukuvunja". Sasa magazeti kadhaa yanaanza kushindana kuandika nani anajua uchafu wa kiongozi gani zaidi na siku si nyingi hili litafika hadi kwa Rais, na mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kuwa ni fair target. Somebody got to stop this or as a people we ough to be prepared to pay a huge price for the silence we maintain.
   
 2. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  kumbe ajaoa tena. ???????????
   
 3. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #3
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  vibaraka wa mengi mko wengi
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mipaka ya uhuru wa vyombo vya habari uwa unaishia sehemu gani au wapi?
   
 5. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #5
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  na mipaka hiyo anaiweka MCT, mahakama au nani? muda si mrefu vyombo vya habari vyote vitakuwa UDAKU UDAKU UDAKU
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  - Wakuu

  - kuna wanajamvi walibandika kuwa IPP wameanzisha Magazeti mengine mawili (kama sikose) na kwa mujibu wa waleta habari inaonyesha kama msimamo wake ni kupambana na magazeti hayo mengine yalionzishwa na pro-fisadi (right?)

  - Kuna heading moja imeletwa humu akiongelea Waziri mkuu msaafu blah blah shoga! Hii imetoka kwenye gazeti moja la IPP (right?)

  - Sasa nani anamchafulia nani jina?
   
 7. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,324
  Trophy Points: 280
  Nimekumbuka wimbo mmoja wa Msondo kama sikukosea``ùkiona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo....``

  Nawaambieni engi kulialia mbele ya vyombo vya habari si kawaida kwa mtu mzima na mwenye uwezo kama mengi. Kuna mambo mengi na mazito yanafanyika nyuma ya pazia tupeani muda tu tutaliona. Lakini je nani ataumia na nani atafaidikia????? Lets wait
   
 8. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #8
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hilo bandiko na mimi nimeliona mahali likisema hivi


  • HUYU REGINARL MENGI MBONA ANAMAMBO YA KITOTO JAMANI! AMAKWELI UZEE MBAYA NA HUYU ANAZEEKA VIBAYA, ETI KAANZISHA GAZETI LA KUMSEMA MUME MWENZIE MASHA ‘SEMA USIKIKE’ NA KAFUFUA LILE LA TAIFALETU NA KUMNANGA KARAMAGI KUWA KAKIMBIWA NA MKEWE ANACHUKUA WAKE ZA WATU, MBONA NAYEYE KAMUACHA MJASIRIAMALI MWENZAKE ANAFAKAMIA WATOTO ZA WATU NA WAKE ZAO.
  ILA HONGERA ZAKE KWA KUMSOMESHA MTOTO WA LILIAN KIMARO ARUSHA INTERNATIONAL SCHOOL.
   
 9. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwanakijiji, Waziri wa Habari hawezi kucheza mchezo huu. Huu ni mchezo wa hatari sana kwake. Nadhani anatamani kuingilia, ila dhamira yake ya kisiasa haimtumi kufanya hivyo. Maana akifanya hivyo, anahisi anaweza kupotea katika ulingo wa siasa.

  Mkuu, nadhani mafisadi hawatumii akili vizuri. Wanaangaika sana kupambana na Mengi kwa kujaribu njia mbali mbali kumbomoa na kubomoa nguzo anazozitegemea. Wanajua kuwa Mengi anaheshimiana sana na Mkuu wa Nchi. Na hilo linawakera. Hivyo wakavumisha kuwa anataka kugombea urais. Wakaona hilo limekwama hadharani wakaingia nyumbani kwake. Wakavumisha kuwa ameoa Bomani. Hili walijua lingewasha moto mkali home kiasi kwamba Mengi angeshindwa kuendelea ku-focus kwenye mapambano na mafisadi. Sidhani kama wamefanikiwa hilo. Wataendelea kila sehemu wanazoona Mengi ana nguvu ili wazivunje. Ila najua watashindwa pia.

  Mafisadi hawajui adui yao. Adui yao mkubwa sio Mengi peke yake, ni waTanzania wote. Kila mwananchi anawachukia, na anawachukia kwa nguvu sana. Hata hao wanaokaa nao na kuwafariji, ni wanafiki tu. Wanatumika pia kuwateketeza. Wajue hawana rafiki mpaka warudishe walichoiba, waombe msamaha ikiwezekana wapate hukumu na wabadilike kabisa kuwa watu wa wema kwa jamii nzima.

  Uchaguzi unakuja. Hivyo watajitahidi sana kurudi kwenye ulingo wa siasa. Na kufanya hivyo wanahisi ni lazima warudishe nguvu zao zote. Wamekosea sana. Nguvu hizo zimekwisha kabisa. Labda wazaliwe upya.
   
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Huyu mzee kwa kulia lia kila siku naye kazidi,sasa kama anajua kuna watu wana majumba huko Dubai na wapi mbona hawataji?blah blah kibao zisizo na msingi.Tunahitaji mtu jasiri ambaye atweza kuwafungulia mashtaka mafisadi na siyo kusema ukwasi walio nao.

  Fitina na uongo upi?kwamba yey siyo Fuska na yule binti siyo mchumba wake?hajaeleza ndani..

  Mtu ambaye anweka Fitina ni yeye mwenye we na Magazeti yake kwa kisingizio anakandika Ufisadi.Ndiyo imesaidia ila kuna amabo mengine anafanya kwa faida ya ugomvi wake na watu wengine!

   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  REGINALD MENGI SIO WA KUIGWA

  Inakuwaje unapompiga ngumi baba yako yeye anaamua kukurudishia hapo hapo anakuongezea mateke halafu anakimbilia kwenda kuchukuwa kitu akikate kichwa kabisa je huyu baba atakuwa anajenga familia bora ? kwanini asichukuwe nafasi yake ya baba abakie kuwa baba ?

  Katika ugumvi huo kwa sababu baba ameamua kwenda kuchukuwa panga ili amalize ugomvi huo kiurahisi aonekane mshindi je majirani na wapita njia watachukuliaje tukio hilo ?

  Na hivi ndivyo ilivyokuwa sasa hivi baada ya baadhi ya magazeti kuanzishwa na watu ambao Reginald mengi anawaita mafisadi katika baadhi ya magazeti yake ametaja mpaka majina ya watu hawa pamoja na magazeti wanayoyaongoza .

  Baada ya kuona hivi yeye kama baba akaamua kuwajibu kupitia magazeti yake kama Thisday ,Kulikoni na sasa hivi ameamua kufufua magazeti yake kama Taifa Letu na Sema Usikike kushambulia watu hawa inaosemekana ni mafisadi

  Angalia nafasi aliyonayo mengi katika jamii ya watanzania na watu wengine wa kimataifa nafasi aliyonayo katika baraza la habari na sehemu zingine nyingi katika nchi hii leo amefikia hali hiyo sijui hana washauri au washauri wake ndio wamemshauri hivyo hata hatujui kinachoendelea .

  Kutokana na jinsi anavyofanya sasa imetufanya tuanze kuwa na wasi wasi nae mkubwa sana na kupoteza imani nae kama mzalendo halisi wa nchi hii kwa jinsi anavyopenda kupeleka jamii shimoni yeye sio mzalendo tena anajua anachofanya .

  Sasa tunapokuwa na familia zetu na sisi huko mbeleni hatuwezi tena kuchukulia yeye kama mfano wa kuigwa hata kidogo yote aliyoyafanya yanafichwa na huu uchafu anaouendeleza sasa hivi kutumia vyombo vyake vya habari

  Hata hizi kampuni anazoendesha kama mtendaji mkuu kama The guardian sio brand zake halisi ni brand za nchi za ulaya kama ITV , Radio 1 huko nyuma vituo vyake vimeiba kazi za watu wengine toka nchi mbali mbali za kuzirusha hewani bila idhini yao
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  NImejaribu kukuelewa nimeshindwa Mkuu. Naomba uelezee zaidi ili nielewe unachokipinga hasa na nini kisichofaa kuigwa.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Feb 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  right.. na wale wa mafisadi wako wachache!
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ..kwani hajaoa na picha zipo...kamuoa lilian kimaro wa BRELA.....
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Feb 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  a. Utakuwa hujakomaa ukimchukulia Mengi kama baba yako au mfano wa maisha yako. Tafuta watu wa familia yako kama mfano.

  b. Ni wazi kuwa huna tatizo na uchafu mwingine unaoandikwa na watu wengine. Unachotaka kusema ni kuwa "huyo baba yako" ukianza kumpiga yeye akukodolee macho na kukuchekea ati kwa vile asikuoneshe mfano mbaya.

  c. Magazeti yote yanaandikishwa na serikali, kama serikali inaona magazeti au vyombo vya Mengi au mtu mwingine yeyote vinakiuka maadili ni wao wanajukumu la kuchukua hatua. Hadi hivi sasa serikali haijaona ubaya wowote. So tuwaache waendelee kugongana wapendavyo!
   
 16. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #16
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hata kama wana ndege hayamhusu ni za kwao mbona yeye anavyotumia brand za watu hatusemi ?? Radio 1 , itv si brand za watu wengine ? The gurdian si brand ya watu wengine ?? Kwanini asiwe mbunifu awe na vyake ??
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nani alifungisha ndoa?
   
 18. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nashindwa kujua mstakabali wetu kama taifa,tunaenda wapi hasa,hakuna hata mmoja anayetaka kuwajibika,zaidi ya kuwindana kama wanyama,hakika Taifa letu limekuwa kama shamba la wanyama,,,mwenye nguvu anamla asiye na nguvu,,,,it is the survival of the fittest,,,,,,
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hata wewe utaliwa wewe weka kichwa nje tu utaona
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Feb 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimekupata mzee, angalau wewe una motivation nyingine ya kusema hivyo. Sasa mnatuchanganya hapa PM anasema keshaoa, wewe unasema mchumba. Ina maana hao watu wengine wanayoyafanya huna tatizo nayo isipokuwa anachofanya Mengi.

  Kwanini usipinge pande zote mbili (au tatu) kutumia vyombo vya habari kuchafuana?
   
Loading...