Nchi hii ni ya ajabu sana. Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi tulitegea wapambane wananchi wapate huduma bora za afya- bima ya afya kwa kila mtu, elimu bora, miundo mbinu mizuri ya barabara, wanainchi wafundishwe kilimo bora na kuongeza thamani ya mazao yao n.k. Badala ya madiwani kupambania hayo wapo wanataka miji yetu iwe majiji- Tanga ni jiji, Mbeya ni jiji, Dodoma ni Jiji, Arushani jiji, Mwanza ni jiji na of course Dar. Sasa ni nini kimebadilika kwa mji kama Tanga kuitwa jiji. Au, Dodoma au Mbeya. Maisha yanazidi kuwa duni tu, hadhi ya jiji haibadili maisha ya mtu. Ni afadhali tufikirie mbinu za kuwatoa wananchi wetu kwenye umaskini kuliko kupambania miji yetu iitwe majiji