Moshi: Mwalimu mbaroni akituhumiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi kwa kumpiga mateke

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Utata umeibuka kuhusu kifo cha mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari iliyoko Pasua, Manispaa ya Moshi, Walter Ebenezer, anayedaiwa kushambuliwa kwa mateke kwenye mbavu na mwalimu wake kisha kupewa adhabu ya kupiga ‘push up’.

Kutokana na kifo hicho, ndugu wa mwanafunzi huyo wamejitokeza hadharani wakiliomba Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kufanya uchunguzi wa kitabibu kubaini sababu za kifo hicho.

Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo kabla ya kupoteza maisha Februari 19 mwaka huu kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) alikokuwa anapatiwa matibabu, alikuwa mwanafunzi wa bweni wa shule hiyo.

Akizungumzia tukio hilo jana, mama mdogo wa marehemu, Mkazi wa Sakina-Arusha, aliyejitambulisha kwa jina moja la Neema, alidai kuwa kabla mwanafunzi huyo hajafariki dunia, aliwaambia kwamba alipigwa na mwalimu wake mateke kwenye mbavu na aliambiwa apige push up kutokana na kosa ambalo hakuliweka wazi.

"Baba mzazi wa marehemu, alipigiwa simu akaambiwa akamchukue mtoto maana anaumwa sana. Alipokwenda shuleni kumchukua mtoto, alimleta Mount Meru kwa ajili ya matibabu.

Kili.JPG

Alipofikishwa Mount Meru, alipatiwa matibabu na aliwekewa oksijeni. Baadaye mtoto alipoteza maisha. Lakini tulikwenda kufuatilia polisi. Tulianzia Central Arusha (Kituo Kikuu cha Polisi) na baadaye tukaelekezwa twende Central ya Moshi mahali ambako tukio ndiko lilitokea.

"Tulimwelezea OCD Moshi (Mkuu wa Polisi wa Wilaya) tukio zima na akachukua gari na askari na wakaenda shuleni, hawakumpata mwalimu, wakaambiwa warudi siku iliyofuata.

"Niliwauliza polisi kama tunaruhusiwa kuuzika mwili, nikaambiwa 'hapana!', tunatakiwa kusubiri mpaka wafanye uchunguzi wao," alidai.

Hata hivyo, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliendelea kudai kuwa walipokwenda Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, waliambiwa wanatakiwa wauzike mwili huo.

"Tunashangaa tutazikaje wakati Central Moshi wametuzuia na ndio ambako tukio limetokea? Tunazikaje huo mwili, mbona wanafamilia tunachanganywa? Tunazikaje wakati hatujajua mwafaka wa ndugu yetu amekufakufaje? Tunahitaji haki, uchunguzi ufanyike," alisisitiza.

Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi (ACP) Simon Maigwa, alikiri jeshi hilo linamshikilia mmoja wa walimu wa shule hiyo (hakumtaja jina) kwa ajili ya uchunguzi.

"Tumefungua jalada la uchunguzi. Kwa sababu ni malalamiko, ni jukumu letu kumshikilia ili tujiridhishe. Timu yangu ya makachero imekwenda kufanya postmortem (uchunguzi wa kitabibu) ili tujiridhishe kwamba ni kweli aliuawa au alikuwa anaumwa?

"Tunachunguza lakini hatuwezi kusema moja kwa moja. Sasa kumshikilia ni jukumu letu, kwa sababu kuna malalamiko juu yake. Tunasubiri madaktari, watuambie kwamba chanzo cha kifo chake ni nini.

"Makachero wetu wamekwenda huko (Hospitali ya Mount Meru) kujiridhisha kwanza na hiyo taarifa, kama kweli ipo na kama ipo, basi washirikiane na ndugu ili 'ku-clear' (kumaliza) hiyo doubt (shaka). Bado uchunguzi unaendelea, tunamshikilia kwa ajili ya uchunguzi na sio kwa sababu ya mauaji," alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Walimu wenzangu hiki ni kizazi Cha lonyolonyo watoto walegevu mnoo,zamani walikua wanapigwa hawafi au hawaumwi siku hizi maradhi mengi wanafunzi Bado watoto mnoo katoto kanaanza shule na five years form four ana miaka 15 unavyompiga kama unapigana na mkubwa mwenzio jua utaleta athari tu

Mimi mwl ila nillishawahi enda shule kuongea na walimu juu ya mwanangu alikua anachapwa akawa asubuhi daily anaumwa hataki shule,ikabidi nisom saikolojia yake ktk kumuuliza nkajua anakimbia fimbo nkaenda kuongea na walimu nkawaambia mwanangu ana 7 yrs,std 3 yupo fimbo mnazompiga hazilingani na age yake hataki shule mtoto ,naomba aadhibiwe kulingana na umri wake Wala Sio darasa

Nashukuru since then hakukataa shule na hawakumchapa kiutu uzima
Sasa walimu tulee wanafunzi kama umri wao ulivyo Sio darasa lao tutaua na kufungwa daily. Fika shule timiza majukumu Yako,Rudi nyumbani, mshahara unapata kiherehere Cha nini

Watoto wa Sasa ni kizazi Cha nyoka watata mnoo tunajua ila maradhi mengi Sanaa,afu walevi,Malaya,wahuni n.k umempiga kakufia ,mmegawana majengo ya serikali. Kwani lini mtaskia nyie walimu wenzangu jamani

Mimi mbona mwl na Sina huo muda nanyoosha wanafunzi ila Sio Kwa kupiga mpk kuumiza mtoto ,familia zenu zinawategemea jamani acheni hizo mambo
 
Walimu wenzangu hiki ni kizazi Cha lonyolonyo watoto walegevu mnoo,zamani walikua wanapigwa hawafi au hawaumwi siku hizi maradhi mengi wanafunzi Bado watoto mnoo katoto kanaanza shule na five years form four ana miaka 15 unavyompiga kama unapigana na mkubwa mwenzio jua utaleta athari tu
Mimi mwl ila nillishawahi enda shule kuongea na walimu juu ya mwanangu alikua anachapwa akawa asubuhi daily anaumwa hataki shule,ikabidi nisom saikolojia yake ktk kumuuliza nkajua anakimbia fimbo nkaenda kuongea na walimu nkawaambia mwanangu ana 7 yrs,std 3 yupo fimbo mnazompiga hazilingani na age yake hataki shule mtoto ,naomba aadhibiwe kulingana na umri wake Wala Sio darasa
Nashukuru since then hakukataa shule na hawakumchapa kiutu uzima
Sasa walimu tulee wanafunzi kama umri wao ulivyo Sio darasa lao tutaua na kufungwa daily
Fika shule timiza majukumu Yako,Rudi nyumbani, mshahara unapata kiherehere Cha nini
Watoto wa Sasa ni kizazi Cha nyoka watata mnoo tunajua ila maradhi mengi Sanaa,afu walevi,Malaya,wahuni n.k umempiga kakufia ,mmegawana majengo ya serikali
Kwani lini mtaskia nyie walimu wenzangu jamani
Mimi mbona mwl na Sina huo muda nanyoosha wanafunzi ila Sio Kwa kupiga mpk kuumiza mtoto ,familia zenu zinawategemea jamani acheni hizo mambo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wakikuelewa nahama nchi
 
Mpwayungu village aione kwenye jalada
Huyo nae ni mngese tu, hayaoni yanayofanywa na Polisi? Mahabusu wangapi wanafia kwenye vituo vya Polisi yet hawaandiki hao maaskari kwa ubaya? Kwa kusema hivi siungi mkono mambo mabaya wanayofanya Walimu, ila napinga kitendo cha mpwayungu village 'kuwasiliba' Walimu pekee kana kwamba ndo kada pekee yenye mapungufu.
 
Back
Top Bottom