Kilimanjaro: Mwalimu ampiga Mwanafunzi hadi kifo

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
20230718_210249.jpg
Huko Kilimanjaro Mwalimu amempiga mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka saba mpaka kifo kwa kosa la kupiga kelele darasan 🥲

Kwenye picha huyo ni Mama yake Mzazi wa huyo mwanafunzi ameeleza kwamba Mwalimu

Alimpiga sana mwanafunzi huyo mpaka alijikojolea baada ya hali kuwa mbaya ya mwanafunzi alifariki dunia, Mwalimu amekimbia na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta huyo Mwalimu na kufanya uchunguzi wa shitaka hili.

#VibokoSioLazima

Credit: UTV Habari

---

Mwanafunzi wa darasa la kwanza, shule ya msingi Samanga, Wilaya, ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Sistus Aristid Kimario. (7) amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa ni kuchapwa viboko na mwalimu wake kwa kosa la kupiga kelele darasani.

Inadaiwa baada ya mwalimu huyo, James Urassa kutekeleza adhabu hiyo alitoroka kusikojulikana baada ya kubaini mwanafunzi huyo amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema tukio hilo limetokea Julai 17, mwaka huu, baada ya mwalimu huyo kumtandika viboko mwanafunzi huyo na kusababisha umauti wake.

"Jeshi la Polisi tunaendelea kumsaka mwalimu huyu kwa sababu baada ya kubaini mwanafunzi huyo amefariki amekimbia," alisema Kamanda Maigwa.

Alipotafutwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Charles Chavunike, alikiri kutokea kwa tukio hilo Julai 17, mwaka huu saa tatu asubuhi.

Mwalimu huyo alisema akiwa darasani aliona walimu wawili wa shule hiyo wakiwa wamembeba mwanafunzi huyo akitolewa darasani na alipowauliza nini kimetokea alijibiwa mwanafunzi kaanguka darasani

"Baada ya hapo niliita watoto wawili wa darasa la kwanza nikawahoji ni kitu gani kimetokea darasani, ndiyo wakanieleza mwalimu alimchapa mwenzao kwa sababu ya kupiga kelele darasani," alisema.

Alisema baada ya tukio hilo alilazimika kufuata taratibu zote na kutoa taarifa kwa viongozi wa wa kata na vyombo vingine vya dola.

Naye babu wa mwanafunzi huyo, Patricky Kachomba alise-ma mpaka anaondoka kwenda shule alikuwa haumwi popote.
 
Dah! Stress mbaya sana. Kila siku huwa ninawashauri walimu ku work under minimum stress, lakini hawasikii tu. Tumieni muda wenu mwingi kwenye kutatua changamoto zenu. Achaneni kabisa na haya mambo ya kuadhibu watoto wa watu. Fanya kazi, rudi nyumbani kalishe kuku wako/kasimamie duka lako/kakague shamba lako! nk. Acheni kabisa kujitesa na watoto wa watu!

Watoto wengine wana changamoto zao binafsi za kiafya! Ya nini kujiingiza katika matatizo? Mwalimu unahangaika na watoto wa wenzako, wa kwako anakuhangaikia nani?

Walimu ifikie wakati mbadilike kimtazamo, na pia kifikra. Dunia imebadilika.
 
Back
Top Bottom