Matinyi: Tahasusi mpya za dini shuleni, kinachofundishwa ni maarifa ya dini sio imani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akielezea sababu ya Serikali kujumuisha Tahasusi za masomo ya Dini katika ngazi ya Elimu ya Sekondari baada ya mwongozo kutolewa hivi karibuni kuhusu masomo hayo.

Je ! Watu wamepotezea hizi mada kuhusu tahasusi mpya 2024 ?

Nchi hii ina dini mbili tu?, je wenzetu wa Rastafarian, Shinto, buddha, Tao, Pagan et al nao wanapata wapi maarifa na elimu yao kama ilivyo kwa wengine?

Nadhani lengo na mipango ni ile ile ya kuifanya Tanganyika kuwa nchi ya ...
 
Niliuliza kuanzia mwanzo kwa nini siyo Religious studies? Sikujibiwa
 
  • Thanks
Reactions: K11
Hayo maarifa ni upuuzi mtupu na hayana tija kwa taifa linalotaka kukimbia kimaendeleo.
 
Lengo hapa ni kuweka uislam tu kwenye mfumo rasmi wa elimu wakati hiyo divinity imewekwa tu kama kubalansi dini kuu mbili zenye kuaminiwa na wengi ili hali hiyo divinity si ukristo bali ni abrakadabra fulani hivi isiyojulikana kwa wakristo kwa ujumla ni kitu gani.
 
kuweka hayo maarifa ya dini kwenye tahasusi.. ipo kwenye dira ya nchi..?
ama ilani ya chama chetu.?
 
Aendaeni miongozo ya dini yenu mpeleke kwenye mamlaka husika.
Matumizi mabaya ya hela ya mlipa Kodi. Uendeshaji wa nchi lazima uwe na usawa ukizingatia pia minority. Nyie lini mliandaa huo mwongozo unaotaka siye tuandae?
 
Matumizi mabaya ya hela ya mlipa Kodi. Uendeshaji wa nchi lazima uwe na usawa ukizingatia pia minority. Nyie lini mliandaa huo mwongozo unaotaka siye tuandae?
Mitaala ya masomo ya dini huwa inaandaliwa na kuwa ku submitted kwa mamlaka husika na wadau wa dini husika.
 
sisi WATANZANIA HATUNA JEMA KABISA! Watu wengi tumekuwa tukiomba tahasusi za dini ziingie kwenye mtaala wa elimu zimewekwa tena kelele zimeanza kweli hatuna JEMA!
mambo ya dini tutafundishana tunakoabudu na kuamini kuna Mungu huko. Kuingiza islamic na divinity ni upuuzi mtupu usiokubalika. Nijue hayo maarifa ili nivumbue nini?
 
Mitaala ya masomo ya dini huwa inaandaliwa na kuwa ku submitted kwa mamlaka husika na wadau wa dini husika.
Wewe unaona sawa resources za nchi kutumika kueneza ajenda za dini?
sisi WATANZANIA HATUNA JEMA KABISA! Watu wengi tumekuwa tukiomba tahasusi za dini ziingie kwenye mtaala wa elimu zimewekwa tena kelele zimeanza kweli hatuna JEMA!
Mmeomba na nani?
 
Back
Top Bottom