Mnyika's refusal of talking about his private life dissapoints Clouds FM

Mnyika's refusal of talking about his private life dissapoints Clouds FM

Mimi sifuatagi mikumbo. Ninapoona pana makosa nitakosoa. Ninapoona hapana haki nitatetea.

Kipindi cha Diva kinajulikana wazi. Na wageni wa hicho kipindi huwa wanaulizwa maswali yanayoendana na format ya kipindi.

Hiyo audio soundbite nimeisikiliza. Hakuna alichouliza Diva kilichokuwa nje ya mstari. Diva kauliza tu kama Mnyika ana rafiki wa kike. Hakuna ubaya wowote hapo.

Kwahiyo katika program nzima aliyoandaa huyo matangazaji wenu hilo swali la marital s status kwake ndio lilikuwa ndio mjadala wa kipindi kizima? hii ndio tabu wa kuajili strippers kuja kuongoza vitu professional wise.......huyu anataka kupigwa dudu tu hana lolote na Mnyika hana muda wa kuwaza ngono zembe!!
 
Kwa maelezo ya ripota wetu, Mnyika hakwenda kwa diva bali alivutiwa waya!

Sawa, hata kama alivutiwa waya ina maana hakujua anavutiwa waya kwa minajili gani? Hilo mimi nakataa. Hivi vipindi huwa vinatayarishwa....hawakurupukagi tu na kwenda hewani.
 
Mnyika hakutakiwa kwenda kwenye hicho kipindi; wanasiasa wanaojipeleka huko na kufunua mambo yao wanajiweka katika hali ya kufunuliwa zaidi. Ila hata hivyo nimependa majibu ya Mnyika ambayo ni very standard and well thought and reasoned.

Hakwenda (hakujipeleka) huko kwenye kipindi Mzee, huyu alipigiwa tu simu -- hakuwa na la kufanya. By the way, hivi huwa wakiwa wanakurekodi, unakuwa na taarifa hiyo? Au ile ukipokea simu tu tayari rekoda yake in-run?
 
For sure, Individual has the right to decide what to disclose or not . Individual privacy should be respected....period!. The root problem here is not Mr. Mnyika because his explanations were clear, but lack of focus and creativity of Radio program producer and presenter! Two things are Obvious here:
1: You know that Mnyika is a Politician, why did you contact him in the first place if you knew your session is about Love? Did you want to discuss political love?

2: Secondly, is it a MUST for everybody called by your presenter to discuss personal life? Why didn't you call Eric Shigongo who write love books? This is what i call lack of Focus and lack of creativity!

Radio presenters in Tanzania lack Vision, lack focus, lack creativity. I won't be surprised one day you call Obama to discuss Love...

Actually this is NOT Mnyika's problem, its RADIO Producer and Presenter's lack of vision.

LET POLITICS BE FOR POLITICIANS AND LOVE BE FOR LOVERS!

HAPA MSHAMBA NI DIVA MWENYEWE, PRODUCER WA KIPINDI NA CLOUDS FM! PERIOD!
elimu ndogo na uswahili swahili wa kibongo vimedumaza waandishi na watangazaji wa Tanzania matokeo kwa wasikilizaji wa hivyo vipindi ni kuzidi kudumaa kiakili na kuongezeka washamba na malimbukeni zaidi jijini Dsm!
 
Kwahiyo katika program nzima aliyoandaa huyo matangazaji wenu hilo swali la marital s status kwake ndio lilikuwa ndio mjadala wa kipindi kizima? hii ndio tabu wa kuajili strippers kuja kuongoza vitu professional wise.......huyu anataka kupigwa dudu tu hana lolote na Mnyika hana muda wa kuwaza ngono zembe!!

When people can't debate the facts, they avoid the issues and resort to personal attacks!!!
 
Hakwenda (hakujipeleka) huko kwenye kipindi Mzee, huyu alipigiwa tu simu -- hakuwa na la kufanya. By the way, hivi huwa wakiwa wanakurekodi, unakuwa na taarifa hiyo? Au ile ukipokea simu tu tayari rekoda yake in-run?

Kwa hiyo they randomly decided to call Mnyika?
 
Mnyika hakutakiwa kwenda kwenye hicho kipindi; wanasiasa wanaojipeleka huko na kufunua mambo yao wanajiweka katika hali ya kufunuliwa zaidi. Ila hata hivyo nimependa majibu ya Mnyika ambayo ni very standard and well thought and reasoned.

Kuna tatizo la Msingi ambalo wote hawalioni. Kama nilivosema tatizo hapa si Mnyika, bali Mtangazaji mwenyewe. Hebu Diva huyo atueleze , yeye kama 'Mtaalamu' wa masuala ya Mapenzi kwanza atuambie alivunja ungo lini? Nani alimtoa Bikira na amekuwa na wapenzi wangapi toka avunje ungo? Akijibu maswali haya kwa ukweli then Mnyika alikosea!
 
Haya maswali hata mwendesha kipindi cha taarabu hawezi kukujibu, ndio maana siku zote hata mtu kukataa kujibu swali lako nalo ni jibu vilevile!!
 
Dah kazi kweli kweli hapa...sasa labda kinachohitajika hapa ni kujua kama huyo bi Diva alimuandaa Mnyika i.e. alimtaarifu mapema kuwa tutakupigia simu na kufanya mahojiano na wewe wakati wa kipindi chake (hivi kinaitwaje tena??). kama hilo lingefanyika basi kusingetokea kashkash kama hiyo mpaka kumkatia mtu simu (by the way Diva that was so unethical in journalism--never do that again).

Prior to kipindi, Mnyika angejua kuwa nitaulizwa maswali haya na haya na angekuwa amejipanga jinsi ya kuyajibu.
 
Yes, hata mimi nakubaliana na wewe kuwa Mnyika asingeenda kabisa kwenye hicho kipindi. It's just not his thing. Nevertheless, he was a good sport.

Ila sauti yake wakati anamshangaa huyo mtangazaji imenisikitisha kidogo "kwa hiyo ndio mnakata"? akaambbiwa ndio. Halafu ukisikiliza utaona mdada alipoteza her cool na kurudia sauti yake ya uswahili kabla hajarudi tena na sauti yake inayokera! Kwa kweli hana tofauti sana na George Maratooo wa ITV...
 
way to go Diva!

Akija mwanasiasa yoyote akaleta siasa kwenye kipindi cha mapenzi, mkatie simu mbalini.

Mtu anajua fika kipindi ni cha aina gani, kisha anataka kujifanya yeye haongelei mapenzi.....kaenda kufanyaje sasa!
 
Kwa maelezo ya ripota wetu, Mnyika hakwenda kwa diva bali alivutiwa waya!

Eleweni kuwa watu hupewa taarifa mapema sana [hata kwa siku kadhaa wakati mwengine] kuwa watapigiwa simu kujiunga na kipindi, na ndio maana Diva akasema "kama nilivyokwambieni leo tutakuwa na J.J.Mnyika."

Na juu ya hivyo, mtu anapopigiwa simu kutoka studio, huwa anakuwa yupo kwenye line off air, akizungumza na watayarishaji wengine wa kipindi, kabla ya kurushwa hewani studio.

Kwa hiyo alijua vyema kinachoendelea
 
Hivi kama BBC wangekuwa wanawakatia watu simu kwa sababu wametoa majibu tofauti na walivyokuwa wanataka wangekuwa wapi?

Tumekuwa tukiona wanaohojiwa ndio wamekuwa wakikimbia lakini unapoona reporter ndio anakimbia kuna walakini mkubwa wa uwezo wake

PERSISTENCE ni sifa kuu ambayo Diva angetakiwa awe nayo
 
Una uhakika gani kuwa the BBC since its inception in 1922 hakujawahi kutokea mtu kukatiwa simu/ kuondolewa hewani?

Mimi kila siku nasikiliza talk radio na watu kukatiwa simu wala si jambo la ajabu.
 
Una uhakika gani kuwa the BBC since its inception in 1922 hakujawahi kutokea mtu kukatiwa simu/ kuondolewa hewani?

Mimi kila siku nasikiliza talk radio na watu kukatiwa simu wala si jambo la ajabu.
Ndio kuna watu wanakatiwa kutoka na wanachoongea mfano matusi au kupiliza muda na wanapewa woni kwamba watakatiwa simu.
 
Kwa hiyo hata mtu akiulizwa kama atagombea ubunge 2015 hakakataa kusema "Ndio" au "Hapana" atarajie kukatiwa simu na kuitwa mshamba
 
Ndio kuna watu wanakatiwa kutoka na wanachoongea mfano matusi au kupiliza muda na wanapewa woni kwamba watakatiwa simu.

Sasa ajabu ya mtu kukatiwa simu baada ya kukataa kuzungumza kulingana na muundo wa kipindi iko wapi?
 
Kwa hiyo hata mtu akiulizwa kama atagombea ubunge 2015 hakakataa kusema "Ndio" au "Hapana" atarajie kukatiwa simu na kuitwa mshamba

Inategemea na yuko kwenye kipindi gani na makubaliano yao yalikuwaje.....
 
Mnyika hakutakiwa kwenda kwenye hicho kipindi; wanasiasa wanaojipeleka huko na kufunua mambo yao wanajiweka katika hali ya kufunuliwa zaidi. Ila hata hivyo nimependa majibu ya Mnyika ambayo ni very standard and well thought and reasoned.

Inabidi nichangie mjadala huu japo machache kwa kuwa naona wakuu wengine mmeingia kwenye mjadala mzito kwa jambo ambalo ni dogo pengine kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi.

Mwanakijiji,

Asante kwa pongezi zako kuwa majibu niliyotoa. Hata hivyo, kauli kuwa 'sikutakiwa kwenda kwenye kipindi' ni potofu na inatoa hukumu ya ujumla bila kuchukua fursa ya kufahamu upande wa pili nini kilitokea. Ukweli ni kuwa sikwenda kwenye kipindi, na sikuwepo Clouds Fm juzi usiku kama ambavyo baadhi ya wachangiaji wengine wamejaribu kueleza.

Ukweli ni kwamba nilipigiwa simu wakati nikitoka kwenye masuala ya kesi ya uchaguzi Ubungo na mtangazaji husika, aliponitajia jina lake nikamtambua, akanieleza kuwa angependa kufanya interview nami kwa ajili ya Clouds Fm kesho yake yaani jana mchana kwa simu. Nikamweleza sina hakika kama nitakuwa na nafasi hivyo, nikamjulisha anitafute jana asubuhi ndio nimueleze ratiba yangu. Akasema hata hivyo hilo suala la kesi nalo ni story kwao hivyo angependa wanihoji juzi ile ile kwa njia ya simu.

Akakata simu yake binafsi na baada ya muda nikapigiwa na landline kwa sauti ya kiume kuwa ni producer wa kipindi na angependa kunihoji kwa ajili ya kipindi cha Amplifier na nikazungumza nao vizuri kuhusu suala la kesi, na naambiwa siku hiyo walitoa katika habari 10 za Amplifier. Baada ya kumaliza kuhojiana naye akanieleza kwamba kwanini badala ya jana, wasipige ndege wawili kwa jiwe moja kwa Diva naye kunihoji? Mpaka hapo sikuwa najua anataka kunihoji kuhusu nini hivyo nisingeweza kusema chochote. Kwangu si busara kukataa mwito ingawa unaweza kukataa uitiwalo, hivyo akapewa nafasi na swali nililomuuliza ni kuwa anataka kunihoji kuhusu nini? Akasema kuhusu mapenzi, nikamuuliza mapenzi yamefanya nini au kuhusu nini hasa?

Akasema nina swali moja dogo kwamba una mpenzi au la? Nikamwambia swali hilo siwezi kujibu redioni, kwa hiyo unamaanisha huwezi kufanya mahojiano kuhusu swali hilo, nikamwambia NDIO. Akasema basi haina shaka, sitakuuliza swali hilo, nitauliza swali lingine akimaanisha kutaka mtazamo wangu kuhusu masuala ya fedha katika mahusiano, nikamwambia kama unataka mtizamo wangu kama kiongozi katika jamii sawa lakini kama unataka mtizamo wangu kama mtu niliyekuwepo kwenye mahusiano au la sitajibu.

Akasema sawa na hivyo tuanze mahojiano na kuanza kurekodi: Kilichonishangaza ni kwamba moja kwa moja akaniuliza hilo swali aliloniuliza na sio swali lingine lolote, kama ambavyo wote mnaweza kusikia. Katika mazingira kama hayo, wewe ungefanyaje? Ukiwa tayari umeanza kurekodiwa. Mimi niliamua kujibu nilivyojibu, wakati naendelea kujibu, ghafla nikasikia tena tunakata simu, si kitu cha kawaida hivyo ilinibidi niulize kwa mshangao kupata uhakika, na alipothibitisha kama kweli wanakata; nikawajibu tu sawa haina shaka; unaweza kuwaza pia wewe ungejibu nini hasa.

Baada ya kumaliza kuzungumza tu, dereva akaniuliza mbona mahojiano hayo yamekwenda ndivyo sivyo? Nikamjibu inaonyesha kuwa aliyenihoji amekasirika kwa kuwa sijamjibu swali lake, lakini sikumjibu kwa kuwa nilishamweleza toka mwanzo kuwa nisingependa kufanya mahojiano kuhusu suala hilo kwa kuwa maisha yangu binafsi ni ya binafsi na maisha yangu ya umma ni ya umma.

Kwa hiyo ukiangalia mtiririko, baada ya majibu yangu sikutarajia kuwa mahojiano hayo yangerushwa hewani na kauli za mwisho kuanzia wakati namuuliza kuwa mnakata simu au la na kuendelea ni maneno ambayo kwenye vyombo vya habari huitwa off the record. Hata hivyo, chochote na yote yanaweza kuwekwa on the record na ningeshauri yawekwe wazi mawasiliano yote kuanzia mwanzo kama nilivyoyaeleza hapo juu ili wanaojadili wapate muktadha kamili.

Nasikitika kwamba imenilazimu kuandika, maandiko yangu haya yanaweza kutafsiriwa kuwa ni kuendeleza mjadala na pengine suala hili linaweza kwenda kwenye hatua nyingine ya kuanza kuandikwa magazetini. Lakini suala hili likitazamwa kwa mawanda mapana na kuwekwa kwenye mizani ya kimaadili litaishia tu kwenye celebrity forum!

Kwa hiyo baada ya maelezo hayo, mnaweza kuendelea kujadili kama mkipenda lakini kwa matashi yangu kuna mijadala mingine muhimu zaidi ya kitaifa ambayo ningependa kuingia na kuchangia hivyo nitawaacha muendelee kuchangia labda kama liibuke jambo lingine la lazima mimi kulitolea ufafanuzi.
 
Katika maeneo ambayo nimefanya rejea ya mazungumzo ieleweke kwamba nimezungumzia muktadha kwa kadiri ya ninayokumbuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom