Mnyika's refusal of talking about his private life dissapoints Clouds FM

Mnyika's refusal of talking about his private life dissapoints Clouds FM

Unajua nani alikuwa anamuhoji? Utaalamu/ uzoefu wake katika maswala ya kufanya mahojiano na watu mashuhuri/maarufu?.Unajua alianzia na maswali gani mpaka alipofikia Bill hakuona uvivu kulijibu?
Fikirisha ubongo kidogo

Hayo maswali unayoniuliza wewe unayo majibu yake?
 
Hawa wanasiasa washamba wangepewa kozi ya ujanja kidogo. Eti kipindi cha maswala ya mapenzi jamaa analeta misifa ya kijinga. Clouds safi sana kwa kumkatia simu.

He,wewe vipi? kwani ni lazima kueleza mambo yako personal kwenye public?
 
dc-shoes-gatsby-limited-sneakers-1.jpg

nakutumia mkwanja western union unichukulie haya makitu.....
Hivi hujawahi kuzimiwa simu wewe!!......
 
Jamani ndo maana watu wanama degree kwa hizo kazi za uandishi.kwa mtu ambae yupo deep na hiyo kazi anajua jinsi ya kumuingiza mtu kingi hata kama b4 hakuwa na mpango wa kuzungumzia private zake.hawezi kukata simu kwa jibu moja tu.diva ameidhallisha kazi ya uandishi,arudi darasani
 
Mtangazaji ambae hajakomaa hawezi kufanya kazi kikomavu. Kama jibu ya hilo swali ni muhimu sana kwake na ndicho pekee alichotaka kujua afanyie uchunguzi binafsi.
 
Amefanya vizuri tu maana maandiko yanatuambia watu wasifanye ngono mpaka ndoa labda Diva alitakiwa amuulize una mchumba na sio girl friend ambae kwenye maandiko hajulikani
 
Hawa wanasiasa washamba wangepewa kozi ya ujanja kidogo. Eti kipindi cha maswala ya mapenzi jamaa analeta misifa ya kijinga. Clouds safi sana kwa kumkatia simu.



Wewe unafil*a nini kwani wakimkatie Simu hao Clouds JJ anapoteza nn? Jamiiforum kweli imevamiwa,Mnyika aliwapigia hao Clouds au wao ndiyo walimpigia?
 
Watu wametukana kishenzi kwenye FB account yake. Hii issue itampotezea mashabiki sana.


Itampotezea Mashabiki wakware kama wewe ambao wanawaza kusuguliwa muda wote,kwa watu kama sisi ambao Maslahi ya Umma kwanza kutokumjibu "Diva" kuhusu maisha yake ya Mapenzi hakumpunguzii heshima kwetu zaidi sana inamwongezea!!

John Mnyika is one of the most intelligent people in Africa,at his age he has achieved a lot and has done a lot for ths country,I revere him and i trust in his wisdom,anajua nn ajibu,nn asijibu na alazimiki kuwapa maelezo Kenge kama nyinyi wa kituo cha redio ambao ni Makada tu wa Magamba!!
 
Kwa sababu redio ni biashara na wanasiasa ni public figures kwa hiyo wanauzika.

Yeye mwenye kipindi hali hasara hata mwanasiasa akienda pale akichemka [kama alivyofanya Zitto [see video attached]], au akimkatia simu kama alivyomfanyia Mnyika.

Kama mwanasiasa hataki kuuzwa kwenye vipindi vya mapenzi, asikubali mialiko. Hukubaliani na theme ya kipindi, usiende. Simple mbona




duuuuh,Zitto alichemka kuongea na huyo demu mtangazaji,kwanza tone ya huyo mwanamke ni ya kikahaba au ya mwanamke ambaye anaingiliwa,its just pathetic,Mnyika was wise to refuse to talk,that woman is just a hore!!
 
Last edited by a moderator:
When people can’t debate the facts, they avoid the issues and resort to personal attacks!!![/QUOTE]

and thats exactly what your self appointed ''diva'' chose to do, apparently she is so deeply self absorbed in her own world view that she Ignorantly expects every one of her radio guests to respond to her questions in accordance to her own playbook, She should have had a positive plan ''B'' in place, just in case her guest deviated from expected response. of course that could have been possible if she had any sence of intellect as most of us would expect of her, But you know she is From Radio Clouds and Can anybody expect anything better from such a radio!!!!!!!!!!!


Ha ha ha ha ha,Kizungu kilichonyooka na Point nzito,Big Up!! What would a sober-minded person expect frm Clouds?
 
Inabidi nichangie mjadala huu japo machache kwa kuwa naona wakuu wengine mmeingia kwenye mjadala mzito kwa jambo ambalo ni dogo pengine kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi.

Mwanakijiji,

Asante kwa pongezi zako kuwa majibu niliyotoa. Hata hivyo, kauli kuwa 'sikutakiwa kwenda kwenye kipindi' ni potofu na inatoa hukumu ya ujumla bila kuchukua fursa ya kufahamu upande wa pili nini kilitokea. Ukweli ni kuwa sikwenda kwenye kipindi, na sikuwepo Clouds Fm juzi usiku kama ambavyo baadhi ya wachangiaji wengine wamejaribu kueleza.

Ukweli ni kwamba nilipigiwa simu wakati nikitoka kwenye masuala ya kesi ya uchaguzi Ubungo na mtangazaji husika, aliponitajia jina lake nikamtambua, akanieleza kuwa angependa kufanya interview nami kwa ajili ya Clouds Fm kesho yake yaani jana mchana kwa simu. Nikamweleza sina hakika kama nitakuwa na nafasi hivyo, nikamjulisha anitafute jana asubuhi ndio nimueleze ratiba yangu. Akasema hata hivyo hilo suala la kesi nalo ni story kwao hivyo angependa wanihoji juzi ile ile kwa njia ya simu.

Akakata simu yake binafsi na baada ya muda nikapigiwa na landline kwa sauti ya kiume kuwa ni producer wa kipindi na angependa kunihoji kwa ajili ya kipindi cha Amplifier na nikazungumza nao vizuri kuhusu suala la kesi, na naambiwa siku hiyo walitoa katika habari 10 za Amplifier. Baada ya kumaliza kuhojiana naye akanieleza kwamba kwanini badala ya jana, wasipige ndege wawili kwa jiwe moja kwa Diva naye kunihoji? Mpaka hapo sikuwa najua anataka kunihoji kuhusu nini hivyo nisingeweza kusema chochote. Kwangu si busara kukataa mwito ingawa unaweza kukataa uitiwalo, hivyo akapewa nafasi na swali nililomuuliza ni kuwa anataka kunihoji kuhusu nini? Akasema kuhusu mapenzi, nikamuuliza mapenzi yamefanya nini au kuhusu nini hasa?

Akasema nina swali moja dogo kwamba una mpenzi au la? Nikamwambia swali hilo siwezi kujibu redioni, kwa hiyo unamaanisha huwezi kufanya mahojiano kuhusu swali hilo, nikamwambia NDIO. Akasema basi haina shaka, sitakuuliza swali hilo, nitauliza swali lingine akimaanisha kutaka mtazamo wangu kuhusu masuala ya fedha katika mahusiano, nikamwambia kama unataka mtizamo wangu kama kiongozi katika jamii sawa lakini kama unataka mtizamo wangu kama mtu niliyekuwepo kwenye mahusiano au la sitajibu.

Akasema sawa na hivyo tuanze mahojiano na kuanza kurekodi: Kilichonishangaza ni kwamba moja kwa moja akaniuliza hilo swali aliloniuliza na sio swali lingine lolote, kama ambavyo wote mnaweza kusikia. Katika mazingira kama hayo, wewe ungefanyaje? Ukiwa tayari umeanza kurekodiwa. Mimi niliamua kujibu nilivyojibu, wakati naendelea kujibu, ghafla nikasikia tena tunakata simu, si kitu cha kawaida hivyo ilinibidi niulize kwa mshangao kupata uhakika, na alipothibitisha kama kweli wanakata; nikawajibu tu sawa haina shaka; unaweza kuwaza pia wewe ungejibu nini hasa.

Baada ya kumaliza kuzungumza tu, dereva akaniuliza mbona mahojiano hayo yamekwenda ndivyo sivyo? Nikamjibu inaonyesha kuwa aliyenihoji amekasirika kwa kuwa sijamjibu swali lake, lakini sikumjibu kwa kuwa nilishamweleza toka mwanzo kuwa nisingependa kufanya mahojiano kuhusu suala hilo kwa kuwa maisha yangu binafsi ni ya binafsi na maisha yangu ya umma ni ya umma.

Kwa hiyo ukiangalia mtiririko, baada ya majibu yangu sikutarajia kuwa mahojiano hayo yangerushwa hewani na kauli za mwisho kuanzia wakati namuuliza kuwa mnakata simu au la na kuendelea ni maneno ambayo kwenye vyombo vya habari huitwa off the record. Hata hivyo, chochote na yote yanaweza kuwekwa on the record na ningeshauri yawekwe wazi mawasiliano yote kuanzia mwanzo kama nilivyoyaeleza hapo juu ili wanaojadili wapate muktadha kamili.

Nasikitika kwamba imenilazimu kuandika, maandiko yangu haya yanaweza kutafsiriwa kuwa ni kuendeleza mjadala na pengine suala hili linaweza kwenda kwenye hatua nyingine ya kuanza kuandikwa magazetini. Lakini suala hili likitazamwa kwa mawanda mapana na kuwekwa kwenye mizani ya kimaadili litaishia tu kwenye celebrity forum!

Kwa hiyo baada ya maelezo hayo, mnaweza kuendelea kujadili kama mkipenda lakini kwa matashi yangu kuna mijadala mingine muhimu zaidi ya kitaifa ambayo ningependa kuingia na kuchangia hivyo nitawaacha muendelee kuchangia labda kama liibuke jambo lingine la lazima mimi kulitolea ufafanuzi.

There you go my boy, thats why i love you. Radhia yuko wapi sasa kumtetea Diva wake na Clouds Fm?

Asha
 
Huyu Diva, baba yake nae ni seleb, juzi amepewa cheo kishaji, kama ishu ni hata Obama anahojiwaga,, amwite baba yake pia amhoji kama anacheat mama yake.
 
Labda huyo Diva anamtaka Mnyika kimapenzi!halafu huwezi ukamlazimisha m2 azungumzie maisha yake binafsi!
 
Diva ni CD kama wale wa pale buguruni, akanye mbele huko Nyambafu
 
katumia democracy yake!wewe unaemuona mshamba ndo nyie wale wa ndio bwana!! yes man yameshapitwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom