Akasema nina swali moja dogo kwamba una mpenzi au la? Nikamwambia swali hilo siwezi kujibu redioni, kwa hiyo unamaanisha huwezi kufanya mahojiano kuhusu swali hilo, nikamwambia NDIO. Akasema basi haina shaka, sitakuuliza swali hilo, nitauliza swali lingine akimaanisha kutaka mtazamo wangu kuhusu masuala ya fedha katika mahusiano, nikamwambia kama unataka mtizamo wangu kama kiongozi katika jamii sawa lakini kama unataka mtizamo wangu kama mtu niliyekuwepo kwenye mahusiano au la sitajibu.
Akasema sawa na hivyo tuanze mahojiano na kuanza kurekodi: Kilichonishangaza ni kwamba moja kwa moja akaniuliza hilo swali aliloniuliza na sio swali lingine lolote, kama ambavyo wote mnaweza kusikia. Katika mazingira kama hayo, wewe ungefanyaje? Ukiwa tayari umeanza kurekodiwa. Mimi niliamua kujibu nilivyojibu, wakati naendelea kujibu, ghafla nikasikia tena tunakata simu, si kitu cha kawaida hivyo ilinibidi niulize kwa mshangao kupata uhakika, na alipothibitisha kama kweli wanakata; nikawajibu tu sawa haina shaka; unaweza kuwaza pia wewe ungejibu nini hasa.