Mmoja wa Washindi walioipatia nchi jina la 'TANZANIA' alonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmoja wa Washindi walioipatia nchi jina la 'TANZANIA' alonga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyikanavome, Jun 17, 2011.

 1. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 442
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hii nimeipata kutoka wavuti.com nikaona niwajuze na wana JF wenzangu

  Hatimaye aliyeasisi jina la Tanzania aweka bayana

  Mwandishi wa blogu ya
  Kalulunga.blogsopt.com, Alphonce Tonny Kapelah kutoka Mtwara Leo ameona vyema aufahamishe umma juu ya mwasisi wa jina la Tanzania.

  Anasema...

  Nimeona niwafahamishe hili huenda likatusaidia hasa kwa hivi sasa wakati tukisherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tangayika, najua wengi wetu hatujui historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar maana tuliwakuta waasisi wetu wameishafanya zoezi hilo, tusilijadili sana kwa kuwa lengo lao lilikuwa zuri.

  Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la Tanzania pata historia ya namnaalivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A.

  Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kukutana na huyo ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania.

  Imekuwa kama Bahati nimekutana na Mtu huyu aliyebuni jina la Tanzania Mkoani Mtwara, sehemu ambayo tayari naiweka kwenye Historia yangu hata kesho nikiondokaMtwara nitaikumbuka Radio yangu Safari Radio.

  Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.

  Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944, Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T A DAR alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.

  Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGHAKHAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya hapo alikuja baadae kujiunga na Chuo cha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.

  Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar?

  Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku hizi Daily News, akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.

  Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukuaA kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na Akwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA, mfano EthiopIA, ZambIA ,NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.

  Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo…


  REPRESENTED BY THE MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM,TANZANIA TO MOHAMED IQBAL DAR IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY "REPUBLIC OF TANZANIA" DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964 I A WAKAL MINISTER FOR INFORMATION AND TOURISM  Barua hiyo pia ilisema...

  Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na wewe pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe Tanzania. Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane ile Zawadi ya sh. 200 iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya sh. 12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh.200. Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu.

  Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.

  Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye kuwa mshindi pekee wakati barua ilikuwa inaonyesha kulikuwa na washindi wengine 15 ambao nao walishinda?

  Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza, hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi na kumpatia zawadi yote ya sh.200/; pamoja na Ngao.

  Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema anachosikitika ni kuwa mchango wake bado Watanzania hawathamini mchango wake lakini yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu ndiyo tatizo hawataki kutambua mchango wake ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana.

  Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK, Dar– es-Salaam House, 18 TURNHOUSE ROAD, PHONE 44 121-747-9822

  Nimeona niwatumie hii wadau wangu ili tuweze kuongeza ufahamu na kama ulikuwa unalijua hili basi nimekukumbusha pia mambo yalivyokuwa miaka ya 1964.

  Alphonce Tonny Kapelah
  Radio Safari  source:
  Hatimaye aliyeasisi jina la Tanzania aweka bayana - Wavuti
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 27,500
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  Kwa nini umesema yeye tu wakati maelezo yanasema waligawana zawadi yeye akapata sh 12.50,pili huo ni mtazamo wake wa kuchagua jina,wale wengine 14 nao wana sababu iliyopelekea kuchagua jina TANZANIA ni makosa kusema jina hilo limetokana na hayo majina ma4,vipi wale 14?
   
 3. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,969
  Likes Received: 3,003
  Trophy Points: 280
  umesema walikuwa 15 ina maana wote walipendekeza majina kama yey............tujuze hao wengine walitumia vigezo gani kupata jina TANZANIA
   
 4. M

  Masuke JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,598
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hongera zake.
   
 5. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 442
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kama umesoma mpaka mwisho utaona alipewa tuzo nzima ya shilingi 200 baada ya wengine kutokujitokeza, na mmoja alijaribu kujitokeza akakosa sifa.
   
 6. S

  Siao Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You are also a thinker....

  Huhitaji elimu ya nyota kujua dini ya mleta hoja hii hapa... tz mbona bado safari ni ndefu tu naona... hata hivyo upande huo wa medali ulikuwa muhimu kujulikana, hata kama namna ya kuuletaujumbe ndo hivyo tena.... hata hivyo mambo huanza hivyo. Labda wanaotoa mada sasa sawasawa walianza hivi.
   
 7. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 800
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kote nimeelewa, hasa kuhusu IA, ila hapo kwenye RED kama sikosei ilikuwa by then inaitwa South/North Rhodesia, ingawa nayo inaishia na IA. Mkuu naomba ufafanuzi!
   
 8. MashaJF

  MashaJF JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani sijui kama kuna ukweli, je ni nani wa kututhibitishia ili tumpe sifa zake?
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi nimempigia simu leo Mzee Mohammed Iqbar, lakini kwa bahati ghafi yupo safarini kikazi jijini Dar ES salaam, na aliyepokea simu amejitambulisha kama Mrs Iqbar. Na akuweza kusema chochote kuhusiana na hii habari zaidi ya kunambia kuwa nipige tena simu baada ya miezi miwili Mzee Mohammed atakapokuwa amerudi.

  Nimeulizia contacts zake za uko Dar ES salaam, lakini nimeambiwa kuwa Mzee Mohammed huwa atembei na simu, na wala hana email address.

  Ila hii habari nilishawahi kuisoma zamani.
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,105
  Likes Received: 523
  Trophy Points: 280
  poa tu
   
 11. M

  Mutabora Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nahitaji kujipanga upya ili niweze kuchangia nahisi mleta hoja ana ajenda nyingine nyuma ya pazia.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,320
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Kifupi anataka kusema Tanzania ni Nchi ya AHMADIYA MUSLIM JAMAAT
   
 13. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,621
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  ndio maana wahindi wana nguvu sana hapa bongo kwa kuwa nchii hii ina majina ya miungu yao.
  Imelaaniwa nchi hii.
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,316
  Likes Received: 573
  Trophy Points: 280
  kwanini anasema hathaminiwi wakati alikula 200 kama zawadi? alitaka athaminiweje?
   
 15. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,917
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Aliyeleta hii mada namsoma kama ana falsafa ya udini.ni mtizamo wangu tu.hata hvyo kama ni kweli,haina majotro
   
 16. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,917
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Kumbe ndio maana tanzania ni maskini.
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hivi tunasheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika au Tanzania?
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 8,691
  Likes Received: 3,576
  Trophy Points: 280
  Hongera zake sana ila kwa tanzania ilivyo atasahaulika sana wanakumbukwa waliotoa pesa kuchapisha tshirt kuvaa uwanjani na kwneye majukwaa wanapesa tuzo
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,174
  Likes Received: 4,510
  Trophy Points: 280
  Mtu muhimu sana huyo
   
 20. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,850
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mmh i doubt
   
Loading...