Asili ya jina Tanzania na mwasisi wake: Mohammed Iqbal Dar

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,912
Jee ni kweli Mohamed Iqbal Dar, mwenye asili ya kihindi, aliyekuwa akiishi Tanga, mnamo mwaka 1964 ndiye aliipa nchi yetu jina zuri la "Tanzania".

Kama ni kweli huyu mtu yuko wapi kwa sasa?

Na serikali yetu inaweka kumbu-kumbu gani za kihistoria kwa huyu mtu kwa vizazi vijavyo? ili vipate kujuwa nani aliipa nchi hii jina lake.

Au mchango wake hauna maana yeyote, ni jina tuu, kwa hiyo potelea mbali?

Nadhani hata vizazi vya sasa, ambavyo havipo mbali 1964 hatuna uhakika na ndio maana tunauliza.

Naomba anaejuwa kuhusu hilo atuelimishe.

================
UPDATE:

October 22, 2012

UNAPOTAJA historia ya nchi Tanzania, ni dhahiri kwamba hutaacha kutaja majina ya wapigania uhuru na viongozi mbalimbali walioiongoza tangu enzi za ukoloni, hadi kupata uhuru.

Hata hivyo, katika kila historia ya taifa lolote iliyojengwa, kuna watu waliofanikisha historia hiyo, lakini kwa sababu moja au nyingine, michango ya baadhi yao imesahaulika na pengine kutotajwa kabisa kwenye historia hizo.

Wengi wa Watanzania tunafahamu kuwa jina la nchi yetu Tanzania, limetokana na majina ya nchi mbili zilizoungana na kuwa moja ambazo ni Tanganyika na Zanzibar. Hivi ndivyo tulivyofundishwa shuleni.

Wengine wanaamini kuwa Rais wa kwanza na muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyebuni jina la Tanzania.

Lakini ukweli ni kwamba, jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.

Ilikuwaje?

"Nilikuwa maktaba najisomea, nilishika gazeti la Daily News, wakati huo likiitwa The Standard, ndipo nikaona tangazo hilo," anaeleza Dar alivyopata hamasa na kuongeza:

"Siku hiyo hiyo, nikafanya majaribio ya kutafuta jina bila hata ya kuishirikisha familia yangu. Nilichuka karatasi na kalamu, lakini kabla sijaanza kufanya chochote, nilimwomba Mungu aniwezeshe kwa maana naamini Mungu, ndiye kila kitu wakati wa kufanya jambo lolote."

"Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili; Iqbal na Ahmadiya," anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.

Kupata jina Tanzania

Akisimulia alivyopata jina Tanzania, anasema kuwa ilimchukua dakika tano tu kufikiria na kulipata jina hilo.

"Nilichukua Tan kutoka kwenye Tanganyika na kuongeza Zan kutoka kwenye Zanzibar na kupata Tanzan, niliona halitimii vizuri,"anasimulia Dar.

Anabainisha kuwa baadaye alifikiria na kugundua kuwa majina mengi ya nchi za Afrika yanaishia na IA mfano akitoa mfano wa Ethiopia, Gambia, Tunisia, Nigeria, Algeria, Somalia, Zambia, Namibia na kwamba baada ya kubaini hilo aliamua kuongezea herufi hizo mbili na kupata jina Tanzania.

"Nilituma maombi yangu katika shindano hilo, bila kumwambia mtu yeyote nyumbani," anasema Dar.

Baada ya muda mfupi baba yake, mzee Tufail Ahmad Dar, alipokea barua kutoka Wizara ya Habari na Utalii (wakati huo), ambapo ndani yake kulikuwa na ujumbe wa pongezi ya kwamba kijana wake ameshinda katika shindano hilo.

"Wakati naandika, sikuwa na matumaini kama nitashinda kwa kuwa shindano hilo lilikua wazi kwa watu mbalimbali, hivyo sikuwa na tarajio lolote kama ningeshinda,

"Jioni wakati narudi nyumbani, baba mzazi alinifungulia mlango wakati si kawaida yake kwani mama ndiye alikuwa akinifungulia siku zote, hapo nikajua kuna kitu hakipo sawa. Lakini, nilikaribishwa na tabasamu la baba, pamoja na pongezi nyingi, nilifurahi sana," anaeleza.

Tuzo

Dar anasema kuwa kwa ushindi huo, alitunukiwa ngao pamoja na fedha taslimu Sh200 kama zawadi ya ubunifu wake.

Pamoja na kuibuka mshindi wa ubunifu huo na hadi leo jina la Tanzania alilolibuni yeye linaendelea kutumika, lakini Dar anadai kuwa mchango wake huo kwa taifa ni kama hautambuliwi na Serikali imemsahau katika kuandika historia ya taifa la Tanzania.

"Sijui kwa nini sitambuliwi tangu wakati huo? Hakuna chochote kinachoelezea uhusika wangu katika kupata jina la Tanzania na ukiwauliza watu, wengi watakwambia ilikuwa ni Nyerere aliyeleta jina Tanzania, hii inaumiza," anasema akilalamika.

Tanzania ya sasa

Baada ya miaka 13 tangu kufariki kwa Nyerere, Dar anasema kuwa Tanzania haimtendei haki mwasisi huyo wa Taifa, ambalo ni kisiwa cha amani.

"Ni kama imepita miaka mingi sana tangu kifo chake. Watanzania wamesahau kila kitu alichokiota Mwalimu Nyerere. Nakumbuka moja ya vita kubwa aliyopigana ni dhidi ya rushwa, yeye aliichuki rushwa lakini kwa sasa, rushwa imekua kama ndiyo tafsiri ya maisha ya Tanzania. Hakuna kitu kinachoweza kufanyika kwa urahisi hata kama ni haki ya mtu, bila kutoa rushwa," anasema.

Anaongeza kuwa: "Mwalimu Nyerere alikua ni rafiki ya baba yangu na walikua wakionana na kuongea, nakumbuka siku moja kulikuwa na sherehe nyumbani na kwa kuwa tulikuwa watoto, nilimhudumia chai Mwalimu.

"Nakumbuka Mwalimu aliwahi kumuuliza baba yangu; Lini Malaria itaisha nchini hii? Baba alimjibu kuwa, kamwe malaria haitaisha ikiwa hakutakuwa na kujitolea kwa kila mmoja wetu, bila kumtegea mwengine," anasema.

Katika kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Dar anaishauri Tanzania iendeleze misingi ya maisha ambayo Hayati Mwalimu Nyerere aliisimmamia, ikiwamo umoja na mashikamano, ili kuondoa tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri.

"Tunaona namna ambavyo matajiri wanendelea kuwa tajiri zaidi, wakati maskini wanazidi kudidimia. Kama kungekuwa na ushirikiano kati ya watu hawa wawili, tofauti kati yao ingekuwa ndogo au isingekuepo kabisa," anaeleza.

Anashauri pia kuwepo na sanamu za utambulisho ya Baba wa Taifa kila mahali, ili kulienzi jina lake liishi milele.

"Kwa ninavyomjua Mwalimu natamani jina lake liishi milele na litangazwe lijulikane dunia nzima," anasema.

Mohammed Iqbal Dar aliazaliwa mwaka 1944 jijini Tanga, ni mtoto wa tatu kati ya watoto saba wa Tufail Ahmad Dar.

Dar ni baba wa mtoto mmoja, ambapo kwa zaidi ya miaka 40 sasa amekuwa akiishi nchini Uingereza alikoenda kwa ajili ya kusoma kabla ya kuwa raia wa nchi hiyo.

Mbunifu huyo wa jina la Tanzania ni Mhandisi wa Masuala ya Redio, kazi anayoifanya nchini Uingereza, akieleza kuwa katika kuienzi nchi yake, nyumba yake iliyopo mjini Birmingham, ameipa jina la Dar es Salaam, ikiwakilisha ubini wake, pamoja na Jiji la Dar es Salaam
.
 
Jina Tanzania limetokana na Takanyika na Nzanzibar. Majina yeto haya yametoka kwa Wasambaa na si mtu yeyote ambaye anataka kudanganya kupata credit.
 
Jina Tanzania limetokana na Takanyika na Nzanzibar. Majina yeto haya yametoka kwa Wasambaa na si mtu yeyote ambaye anataka kudanganya kupata credit.

Una uhakika? kwani niliwahi kusoma kwenye gazeti moja la hapa Tanzania, bahati mbaya sikumbuki jina au lini, kuwa yalifanywa mashindano na watu wengi wakatuma majina waliyopendekeza na hili "Tanzania" ndio likashinda na inasemekana alishinda huyo muhindi.
 
You are both right

Jambo muhimu ni root ya jina TanZan. Hiyo ia ya mwisho mara nyingi humalizia majina ya nchi/sehemu kama Patagonia, Manchuria, Bavaria, Italia etc.

Katika siku ya muungano 1964 Marehemu Idris Abdul Wakil ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Utalii alipewa dhamana ya kutoa shindano la kutafuta jina la nchi, ndiyo inasemekana huyu bwana akatoa Tanzania likapitishwa, lakini ukisoma magazeti yaliyotokea kutoa siku za mapinduzi mpaka muungano nchi ilikuwa tayari inaitwa Tanzan, kwa hiyo mi sioni alichofanya sana zaidi ya kuongeza hiyo ia ambayo nayo siyo creative sana kwa sababu inajulikana kuwa hiyo suffix ya -ia inatumika dunia nzima kumaanisha nchi ya.

http://www.businesstimes.co.tz/kurasa.php?soma=art&habariNamba=59

http://www.businesstimes.co.tz/kurasa.php?soma=art&habariNamba=59
 
Aaaah kwa hiyo ni kweli huyu Jamaa, mwenye asili ya kihindi ndiye alishinda hayo mashindano na ndie aliyeipa hii nchi jina Tanzania? oopsss, history yetu inaonyesha hatuwezi kukwepa uhindi na uarabu uliokuwepo hapa kwetu, kwani hata Dar es Salaam nasikia ni kiarabu pure.
 
Mwaka 1964, wakati nipo darasa la 8, nilisoma gazeti la the Standard na kulikuwa Shindano hili la kulipa jina nchi yetu. Wakati huo nchi yetu ilikuwa inaitwa the United Republic of Tanganyika & Zanzibar. Wakati ule, shuleni tulikuwa tunasoma jiografia ya Australia na nakumbuka kisiwa cha Tasmania. Hii ilinipa hint ya jina la Tanzania. Mimi niliandika barua wizara ya Habari. Nakumbuka kupokea hundi ya Sh. 12.50 ikiwa ni share yangu ya kuipa jina Tanzania.

Maelezo katika barua ya Katibu Mkuu ilisema: Kwa sababu kulikuwa washindi 16, kwa hiyo hizo zawadi ya Sh. 200 itagawiwa miongoni mwa washindi. Pia, barua hiyo iliniambia kwamba jina hasa lililokubaliwa ni United Republic of Tanzania and sio Tanzania, kama nilivyoandika mimi.

Nakumbuka pia kwamba gazeti la September 1, 1964 au October 1, 1964 ilikuwa na headline, " From today, we are Tanzanians"

Huyo Mohamed Iqbal kama ni katika watu 16, basi anaweza kukubaliwa. Lakini kama anasema ni peke yake aliyechagua jina hili, basi ni mwongo. Best solution ni kwa Wizara ya Habari kupekua file zao na kujua ukweli. I am pleased to be part of history of Tanzania. Ikiwa wengi katika hao 16 walikuwa watu wazima mwaka 1964, basi wengi watakuwa wameshaaga dunia na itakuwa mushkeli kujitokeza. Mimi wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 13 lakini nilikuwa na bahati kusoma gazeti la kiingereza kwa sababu ya baba yangu, ambaye alikuwa anapenda sana kusoma magezeti.

Asili yangu ni kihindi na nilisoma Chuo cha Sokoine 1974. Sasa hivi nipo Marekani na imekuwa bahati tu kusoma forum hiyo kwa sababu ya mambo ya Lowasa.

Ahsante,
Mustafa Yusufali Pirmohamed
 
Mwaka 1964, wakati nipo darasa la 8, nilisoma gazeti la the Standard na kulikuwa Shindano hili la kulipa jina nchi yetu. Wakati huo nchi yetu ilikuwa inaitwa the United Republic of Tanganyika & Zanzibar. Wakati ule, shuleni tulikuwa tunasoma jiografia ya Australia na nakumbuka kisiwa cha Tasmania. Hii ilinipa hint ya jina la Tanzania. Mimi niliandika barua wizara ya Habari. Nakumbuka kupokea hundi ya Sh. 12.50 ikiwa ni share yangu ya kuipa jina Tanzania.

Maelezo katika barua ya Katibu Mkuu ilisema: Kwa sababu kulikuwa washindi 16, kwa hiyo hizo zawadi ya Sh. 200 itagawiwa miongoni mwa washindi. Pia, barua hiyo iliniambia kwamba jina hasa lililokubaliwa ni United Republic of Tanzania and sio Tanzania, kama nilivyoandika mimi.

Nakumbuka pia kwamba gazeti la September 1, 1964 au October 1, 1964 ilikuwa na headline, " From today, we are Tanzanians"

Huyo Mohamed Iqbal kama ni katika watu 16, basi anaweza kukubaliwa. Lakini kama anasema ni peke yake aliyechagua jina hili, basi ni mwongo. Best solution ni kwa Wizara ya Habari kupekua file zao na kujua ukweli. I am pleased to be part of history of Tanzania. Ikiwa wengi katika hao 16 walikuwa watu wazima mwaka 1964, basi wengi watakuwa wameshaaga dunia na itakuwa mushkeli kujitokeza. Mimi wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 13 lakini nilikuwa na bahati kusoma gazeti la kiingereza kwa sababu ya baba yangu, ambaye alikuwa anapenda sana kusoma magezeti.

Asili yangu ni kihindi na nilisoma Chuo cha Sokoine 1974. Sasa hivi nipo Marekani na imekuwa bahati tu kusoma forum hiyo kwa sababu ya mambo ya Lowasa.

Ahsante,
Mustafa Yusufali Pirmohamed

Inabidi nikuamini tu kutokana na yale uliyo andika. Nakushukuru!!

Karibu JF!

SteveD.
 
Hii nimeipata kutoka wavuti.com nikaona niwajuze na wana JF wenzangu

Hatimaye aliyeasisi jina la Tanzania aweka bayana

Mwandishi wa blogu ya kalulunga.blogsopt.com, Alphonce Tonny Kapelah kutoka Mtwara Leo ameona vyema aufahamishe umma juu ya mwasisi wa jina la Tanzania.

Anasema...

Nimeona niwafahamishe hili huenda likatusaidia hasa kwa hivi sasa wakati tukisherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tangayika, najua wengi wetu hatujui historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar maana tuliwakuta waasisi wetu wameishafanya zoezi hilo, tusilijadili sana kwa kuwa lengo lao lilikuwa zuri.

Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la Tanzania pata historia ya namnaalivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A.

Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kukutana na huyo ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania.

Imekuwa kama Bahati nimekutana na Mtu huyu aliyebuni jina la Tanzania Mkoani Mtwara, sehemu ambayo tayari naiweka kwenye Historia yangu hata kesho nikiondokaMtwara nitaikumbuka Radio yangu Safari Radio.

Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.

Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944, Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T A DAR alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.

Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGHAKHAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya hapo alikuja baadae kujiunga na Chuo cha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.

Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar?

Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku hizi Daily News, akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.

Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukuaA kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na Akwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA, mfano EthiopIA, ZambIA ,NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.

Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo…

REPRESENTED BY THE MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM, TANZANIA TO MOHAMED IQBAL DAR IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY "REPUBLIC OF TANZANIA" DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964 I A WAKAL MINISTER FOR INFORMATION AND TOURISM

Barua hiyo pia ilisema...

Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na wewe pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe Tanzania. Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane ile Zawadi ya sh. 200 iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya sh. 12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh.200. Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu.

Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.

Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye kuwa mshindi pekee wakati barua ilikuwa inaonyesha kulikuwa na washindi wengine 15 ambao nao walishinda?

Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza, hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi na kumpatia zawadi yote ya sh.200/; pamoja na Ngao.

Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema anachosikitika ni kuwa mchango wake bado Watanzania hawathamini mchango wake lakini yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu ndiyo tatizo hawataki kutambua mchango wake ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana.

Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK, Dar– es-Salaam House, 18 TURNHOUSE ROAD, PHONE 44 121-747-9822

Nimeona niwatumie hii wadau wangu ili tuweze kuongeza ufahamu na kama ulikuwa unalijua hili basi nimekukumbusha pia mambo yalivyokuwa miaka ya 1964.

Alphonce Tonny Kapelah
Radio Safari

Source: Hatimaye aliyeasisi jina la Tanzania aweka bayana - Wavuti
 
Kwa nini umesema yeye tu wakati maelezo yanasema waligawana zawadi yeye akapata sh 12.50,pili huo ni mtazamo wake wa kuchagua jina,wale wengine 14 nao wana sababu iliyopelekea kuchagua jina TANZANIA ni makosa kusema jina hilo limetokana na hayo majina ma4,vipi wale 14?
 
Umesema walikuwa 15 ina maana wote walipendekeza majina kama yeye, tujuze hao wengine walitumia vigezo gani kupata jina TANZANIA
 
Kama umesoma mpaka mwisho utaona alipewa tuzo nzima ya shilingi 200 baada ya wengine kutokujitokeza, na mmoja alijaribu kujitokeza akakosa sifa.
 
Kwa nini umesema yeye tu wakati maelezo yanasema waligawana zawadi yeye akapata sh 12.50,pili huo ni mtazamo wake wa kuchagua jina,wale wengine 14 nao wana sababu iliyopelekea kuchagua jina TANZANIA ni makosa kusema jina hilo limetokana na hayo majina ma4,vipi wale 14?

You are also a thinker

Huhitaji elimu ya nyota kujua dini ya mleta hoja hii hapa, tz mbona bado safari ni ndefu tu naona. Hata hivyo upande huo wa medali ulikuwa muhimu kujulikana, hata kama namna ya kuuletaujumbe ndo hivyo tena, hata hivyo mambo huanza hivyo. Labda wanaotoa mada sasa sawasawa walianza hivi.
 

Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukuaA kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na Akwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA, mfano EthiopIA,
ZambIA ,NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.
Kote nimeelewa, hasa kuhusu IA, ila hapo kwenye RED kama sikosei ilikuwa by then inaitwa South/North Rhodesia, ingawa nayo inaishia na IA. Mkuu naomba ufafanuzi!
 
Jamani sijui kama kuna ukweli, je ni nani wa kututhibitishia ili tumpe sifa zake?
 
Mimi nimempigia simu leo Mzee Mohammed Iqbar, lakini kwa bahati ghafi yupo safarini kikazi jijini Dar ES salaam, na aliyepokea simu amejitambulisha kama Mrs Iqbar. Na akuweza kusema chochote kuhusiana na hii habari zaidi ya kunambia kuwa nipige tena simu baada ya miezi miwili Mzee Mohammed atakapokuwa amerudi.

Nimeulizia contacts zake za uko Dar ES salaam, lakini nimeambiwa kuwa Mzee Mohammed huwa atembei na simu, na wala hana email address.

Ila hii habari nilishawahi kuisoma zamani.
 
Nahitaji kujipanga upya ili niweze kuchangia nahisi mleta hoja ana ajenda nyingine nyuma ya pazia.
 
You are also a thinker....

Huhitaji elimu ya nyota kujua dini ya mleta hoja hii hapa tz mbona bado safari ni ndefu tu naona. Hata hivyo upande huo wa medali ulikuwa muhimu kujulikana, hata kama namna ya kuuletaujumbe ndo hivyo tena. Hata hivyo mambo huanza hivyo. Labda wanaotoa mada sasa sawasawa walianza hivi.

Kifupi anataka kusema Tanzania ni Nchi ya AHMADIYA MUSLIM JAMAAT
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom