mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 16,053
- 35,955
Kama kuna kitu kizuri mzee wetu Ruksa alikifanya ilikuwa kumgomea mwalimu Nyerere kuondoa jina lake kwenye mchakato wa Urais 1985.
Ilikuwa hivi:
Mwalimu alikuwa na marafiki watatu kule zanzibar, Thabit Kombo, Salim A. Salim na Aboud Jumbe ambaye alikuja kulikoroga wakawa maadui kisa kutaka kuvunja muungano,
Ikapigwa figisu Aboud Jumbe akapokwa kadi yake ya CCM na kupoteza Urais,akarithiwa na Ali Hassan Mwinyi.
Sasa mwaka 1985 Nyerere alitaka kumrithisha nchi kijana wake Salim, alichofanya ni kupandikiza wagombea namluki wawili, Rashid Kawawa na Ali Hassan Mwinyi wachuane na Salim.
Mchakato ulipokaribia mwisho akamwambia Kawawa ajitoe,yule mzee wa watu alikuwa mtiifu sana kwa Mwalimu,akatii akajitoa.
Akamwendea Ali Hassan Mwinyi ili ajitoe,Mwinyi akagoma,majina yakabaki Mawili, Salim na Mwinyi,wazanzibar wakamwambia Mwalimu kuwa hawamtaki Salim yeye ni Hizbu na anajiona mwarabu zaidi, hajawahi kuyapongeza mapinduzi ya 1964 na inasemekana alishiriki mauaji ya Karume, wakasena chaguo lao ni Mwinyi,
Mwinyi akapita uchaguzi mkuu akapata ailimia 92.
Kwa nini nasema alifanya kitu kizuri, Salim na Nyerere akili zao zilikuwa moja wanasiasa wazuri lakini wajamaa sana, wanachukua ubeparu na matajiri ni kama akili za JPM.
Kipindi mwinyi anachukua nchi,ilikuwa kawaida kuona tako la mti mzima kutokana na suruali kuchanika kwa ukosefu wa nguo, sabuni sigara,sukari,bia,kiberiti,mafuta ya taa, ilikuwa ni anasa,na ungekutwa navyo kuliko kiwango kilichowekwa ni jela na ungepewa kesi ya kuhujumu uchumi.
Ukitaka kununua gari lazima uombe kibali,hata petrol lazima ununue kwa kibali, uchaguzi wa 1985 kampeni zake zilianza october 14 badala ya october 7 kutokana na uhaba wa mafuta nchini. Mwinyi baada ya kushika nchi alibadili kila kitu cha Nyerere, nchi ikafunguka mabilionea wapya wakazaliwa bidhaa zikajaa madukani,... kwa mara ya kwanza kombe la dunia tukaliona live tukiwa sebuleni kwetu, kuvaa viraka ikawa ni ulofa,wasanii wa njw wakaanza kumiminika nchini, Bongoman na chakachaka walipikuja nchini kiingilio ilikuwa laki moja .laki moja ndio, nilikuwa mdogo ila mengi nayakumbuka na mengine niliambiwa na wazee wangu
Itaendelea...