Wafadhili wamejenga Msikiti kwenye Eneo la shule ya sekondari inayomilikwa na serikali. Mkurugenzi wa Halmashauri ameuvunja

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,873
6,283
Wafadhili wa Waislamu wamejenga msikiti kwenye eneo la shule ya sekondari ya serikali inayoitwa Talawanda iliyopo katika wilaya ya Chalinze.

Mkurugenzi wa wilaya ya chalinze ameuvunja. sababu eneo ni la shule ya serikali.

Mkurugenzi wa Halmashauri aliyeuvunja ni Muislamu pia. nawaza ungevunjwa kwa amri ya mtu wa dini nyingine ingekuaje?

 
Kuna watu wanajitafutia laana kilazima....mkurugenzi ana udini sana.

Ila atakipata anachokitafuta hapa duniani na huko akhera
Kwa hiyo kwa vile ni nyumba ya ibada ijengwe tu hata katikati ya uwanja wa shule? Au kanisa lijengwe tu hata kwenye uwanja wa jeshi na liachwe tu? Huo ujinga hata Makka au Vatican hautakubaliwa kabisa, wafia dini ni watu wa kukaa nao kwa tahadhari kuliko hata majambazi,jambazi ataathiri mtu au watu wachache tu, ila extremist wanaathiri jamii nzima,akili.
 
Shule nyingi mpaka vyuoni hutenga maeneo kwa ajili ya wanafunzi wa kiislam na kikristo kufanya ibada zao.

Muislam anatakiwa aswali mara tano kwa siku. Asubuhi,adhuhuri (saa 7 mchana), Alasiri (saa 10 ),maghrib (baada ya jua kuzama) na isha (baada ya usiku kuingia). Sasa hao walimu wasije kuleta tena malalamiko pindi wanafunzi wa kiislam wakitoka nje ya eneo la shule kwenda kutafuta misikiti ya kuswalia.
 
Back
Top Bottom