Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

madereva wapimwe vilevi kabla ya kuanza safari, bangi, madawa ya kulevya n.k.
Poleni ndungu zangu mlifikwa na maswahibu haya. Mungu awatie nguvu
 
Duuuh!.....inasikitisha sana. yaani binadamu tunapukutika kwa hajari kama wanyama wa porini!
RIP wote waliopoteza roho zao kwenye hajari hii.
 
Askari wa barabarani mbeya, morogoro ni wazembe kupita kiasi tunaotumia hii barabara huwa tunaona huwezi kuona au kukuta basi lipo speed kali Iringa. Kila siku trafic wanauza sura na kubishana na wamiliki wa mabasi kwenye tv mara vizibiti mwendo mara kamera.. Poleni sana wafiwa na majeruhi.

Ndugu,ni kama umesoma mawazo yangu. Siku chache zilizopita nimesafiri kwenda Mbeya kwa basi.Kwa sasa mabasi yote yaendayo Mbeya,Malawi au Zambia yanakimbia sana mikoa ya pwani,Morogoro na Mbeya. Mkoa wa Iringa wote huwa wanatembea hata ukiwa na baiskeli unawapita. Na madereva huwa wanapigiana simu kuelezana polisi gani(kwa majina)wamekaa sehemu gani. Nadhani pia abiria waanze kuwapiga na kuwachoma moto madereva waendao kasi kama tufanyavyo kwa wezi mitaani. Itasaidia.
 
Kuna haja ya kuongeza tochi za ma-polisi barabarani; na basi yote yafungwe Spidi-gavana kwa lazima ilo lisiwe ombi.
 
Bado hatujifunzi hata kidogo.............Poleni sana Watanzania
 
Ndugu,ni kama umesoma mawazo yangu. Siku chache zilizopita nimesafiri kwenda Mbeya kwa basi.Kwa sasa mabasi yote yaendayo Mbeya,Malawi au Zambia yanakimbia sana mikoa ya pwani,Morogoro na Mbeya. Mkoa wa Iringa wote huwa wanatembea hata ukiwa na baiskeli unawapita. Na madereva huwa wanapigiana simu kuelezana polisi gani(kwa majina)wamekaa sehemu gani. Nadhani pia abiria waanze kuwapiga na kuwachoma moto madereva waendao kasi kama tufanyavyo kwa wezi mitaani. Itasaidia.

... Kumbe inawezekana kudhibiti mwendo wa wapuuzi hawa wachache wanaomaliza ndugu zetu kama ambavyo askari wa Iringa wamedhibitisha! kwa hiyo hawa wengine wanatufanyia makusudi tu...!

Ndugu,mimi ni dereva tena wa siku nyingi tu,nimeshapinduka na gari mara nne. Mara 2 nilikuwa peke yangu kwenye gari,mara 1 nilikuwa na mwenzangu lakini mimi nilikuwa naendesha na mara 1 nilikuwa nimepanda basi la abiria. Kuna tofauti kati ya CHANZO CHA AJALI na CHANZO CHA MAAFA MAKUBWA YALIYOPATIKANA BAADA YA AJALI KUTOKEA. Tairi inaweza kupasuka wakati wowote ukiwa unaendesha gari au hata kama gari imesimama. Pipe ya brake inaweza kupasuka au kuchomoka kwenye maungio yake wakati wowote dereva akiwa barabarani. Lakini kitakachoamua watu wafe kiasi gani na majeruhi wawe wangapi ukiacha na kudra za mungu ni speed ambayo dereva alikuwa akitembea. Soma research zote zinazoelezea ajali za barabarani utaona kuwa chanzo namba MOJA cha maafa makubwa ya barabarani ni SPEED,namba 2 ni UBOVU/HITILAFU ZA VYOMBO VYA USAFIRI na namba 3 ni UBOVU WA MIUNDOMBINU(in our case BARABARA)

Nakubaliana na wewe mkuu. Nilishawahi kupanda basi. Basi lilikuwa kwenye mwendo wa kawaida kwa sababu barabara ilikuwa ya changarawe. Tairi ya mbele upande wa dreva ikapasuka lakini hakuna hata mmoja aliyeumia. Naamini kama basi lingekuwa kwenye speed kali, nisingekuwa naandika hapa.

RIP marehemu.
 
Poleni sana wafiwa na Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi~AMEN. Ukijua ndugu, jamaa au rafiki yako wa karibu anasafiri kwa barabara Tanzania unajawa na wasiwasi mkubwa mpaka atakapokufahamisha kwamba amefika salama maana Barabara zetu ni chinja chinja na si ajabu zinaongoza duniani kwa kuua watu wengi sana au zitakuwemo katika tatu za juu na hii inasababishwa zaidi na Serikali mbovu na dhaifu ambayo haijali kabisa uhai wa Wananchi wake.
 
Kuna haja ya kuongeza tochi za ma-polisi barabarani; na basi yote yafungwe Spidi-gavana kwa lazima ilo lisiwe ombi.

Mkuu sidhani kama hiyo itasaidia. Mbona speed governor zilikuwepo na ajali bado zikatokea? Polisi nao wanaangalia sana pesa. Nafikiri hapa abiria inabidi washike hatamu. Kama gari inakimbia mno basi wamwambie dereva apunguze. Nilishapanda basi moja, dereva alikuwa anakimbiza mwenzake asimkute. Ilibidi tumwambie apunguze speed. Konda akadai eti wanaendesha kwa speed ili wameet targets walizopewa na mmiliki wa basi. Bado tukamtolea nje. Wakasema kama ndio hivyo basi itabidi wasisimame kwenye kituo ili tupate chai. Bado tukasizitiza kuwa chai tutakunywa na speed lazima ipungue. Mbona walikubali. Ila tatizo wako abiria wengine sijui wanajidai wana haraka zao za kibiashara. Wanaudhi kweli. Kwa hiyo the only way to fix this problem ni abiria wenyewe kushika hatamu. That is it.
 
Ajali haina kinga. 80 kph inaua na si mwendo mdogo kama tunavyofikiria. tz hatufuati sheria na ndo tatizo. watu hawafungi mikanda, dereva anakuwa mmoja kwa route nzima na wakati hapaswi kuendesha zaidi ya saa 8. akiwa anasafiri 12 asbh ina maana ameamka 11 plus kujiandaa nk. kama huyu amepata ajali 4 usiku then piga hesabu zako upate idadi ya masaa. na utakuta wakati mwingine alitoka njiani akagonga mawe au kisiki ndiyo tairi likapasuka na si lilipasuka ndo akaacha njia. wenzetu wanazingatia hayo. ukiendesha masaa kadhaa unapaswa kupumzika. na parking zipo. magari yote ya masafa yana meter na chat zinazoratibu safari. ukiendesha zaidi ya muda hata kama hujachoka utapata kasheshe na hutorudia. hapa kwetu ni tofauti. ruksa. tutalaumu madereva but kuna chanzo. serikali ilaumiwe. madereva wa mabasi ni vibarua. they get their bread only when they drive. so, hata kama amechoka atadrive ili ale. ukiweka helper means unagawana nae posho. itabidi ukomae tu. chanzo cha haya si leseni au driverz ila ni mfumo mzima wa serikali kutokufuata misingi ya kazi husika na kupindisha sheria kwa wahusika. poleni wafiwa.
 
Speed limit za hizo barabara za kwenda kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine ni ngapi?

Look at me now...naulizia mambo ya speed limit bongo! I must be out of my mind.
 
Poleni sana wafiwa na mungu awasaidie majeruhi wapone haraka, mimi mara zote huwa siamini mwendo kasi ni chanzo cha ajali nyingi zinazotokea hapa nchini, kampuni ya sumri ni kati ya kampuni bora kabisa ya usafirishaji nchini nategemea watashiriki kikamilifu katika kusaidia wafiwa na majeruhi wote

toa upupu wako hapa, watu wamekufa wewe unasifiwa kampuni! Simple minded people bwana!
 
Ndugu,mimi ni dereva tena wa siku nyingi tu,nimeshapinduka na gari mara nne. Mara 2 nilikuwa peke yangu kwenye gari,mara 1 nilikuwa na mwenzangu lakini mimi nilikuwa naendesha na mara 1 nilikuwa nimepanda basi la abiria. Kuna tofauti kati ya CHANZO CHA AJALI na CHANZO CHA MAAFA MAKUBWA YALIYOPATIKANA BAADA YA AJALI KUTOKEA. Tairi inaweza kupasuka wakati wowote ukiwa unaendesha gari au hata kama gari imesimama. Pipe ya brake inaweza kupasuka au kuchomoka kwenye maungio yake wakati wowote dereva akiwa barabarani. Lakini kitakachoamua watu wafe kiasi gani na majeruhi wawe wangapi ukiacha na kudra za mungu ni speed ambayo dereva alikuwa akitembea. Soma research zote zinazoelezea ajali za barabarani utaona kuwa chanzo namba MOJA cha maafa makubwa ya barabarani ni SPEED,namba 2 ni UBOVU/HITILAFU ZA VYOMBO VYA USAFIRI na namba 3 ni UBOVU WA MIUNDOMBINU(in our case BARABARA)

Naunga mkono 100% kwa vile ni kweli
 
muda wenyewe mbaya kweli,saa 4 usiku!tatizo la sumry na hood na sumry ni 'ligi' za kijinga jinga,wanaenda mwendokasi kama wapo kwenye rally.ajali haiepukiki,ila angalau kampuni ya hood wamejiwekea utaratibu kila wakifika moro,lazima gari iingizwe garage kufanyiwa uchunguzi na matengenezo mbali mbali kama matairi,breki n.k!
kila kona ajaliajaliajali inasikitisha vibaya sana lakini hatuna jinsi! Mungu ndiye mwamuzi!jumlisha na mabasi ya kichina mabovumabovu,jamani
 
Poleni sana wafiwa na mungu awasaidie majeruhi wapone haraka, mimi mara zote huwa siamini mwendo kasi ni chanzo cha ajali nyingi zinazotokea hapa nchini, kampuni ya sumri ni kati ya kampuni bora kabisa ya usafirishaji nchini nategemea watashiriki kikamilifu katika kusaidia wafiwa na majeruhi wote

Ndugu yangu labda hujui tu,lakini kwa taarifa yako kampuni hii ya Sumry ndio inaongoza kwa ajali kwa wastani ajali moja kila week.Nilikuwa mbeya last week pale stand ya Mbeya abiria wa mabasi ya Sumry wanaitwa Mbuzi wa Kafara...Nilishangaa na kuogopa sana.
 
ina maana soln.ya hizi ajali imeshindikana jamani!mbona tutakwisha.poleni wafiwa
 
Basi la kampuni ya Sumry likitokea Arusha kuelekea Mbeya, limepata ajali maeneo ya Igawa, kilometa 140 kutoka mji wa Mbeya. Basi hilo likiwa mwendo mkali, tairi la mbele lilipasuka na kupelekea kupinduka kwake. Watu 13 wamepoteza maisha yao papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya.

Habari zaidi zinasema waliokufa wameshafikia 15

NAFSI YANGU INANIUMA SAANA.JAMAN WANA JF UNAPOKUWA NDANI YA BASI NA UKAONA MWENDO NI MKALI SANA JARIBU KUWAELIMISHA ABIRIA WENZAKO ILI UPATE NGUVU YA KUMZONGA DEREVA IKIWEZEKANA APIGWE HATA VIBAO ILI APUNGUZE MWENDO.NDIO APIGWE SABABU USITEGEMEE HATA SIKU MOJA KWAMBA UKILALAMIKA KWA ASKARI WA USALAMA BARABARANI UTAPATA MSAADA,HAO WAKISHAPEWA ELFU MBILI HAWAULIZI CHOCHOTE.PIA MADEREVA WANA LIGI AMBAZO WASHABIKI WAKE WAKUBWA NI WATU WA STENDI NA BAADH YA ABIRIA.ANGEFIKA MAPEMA UTASIKIA WANASEMA DEREVA NI NOMA....MATAJIRI LAZIMA WAWE WAKALI SANA.KUNA TAJIRI MMOJA WA TABORA ANAITWA NBS CLASSIC HUYU HAPENDI MZAHA NA MALI YAKE HATA KIDOGO,USAFIRI WAKE NI WA UHAKIKA SANA.MADEREVA WOTE WAMEPEWA MUDA WA KUONDOKA NA KUFIKA.IKITOKEA DEREVA KAFIKA MAPEMA HUWA ANATAKIWA AJIELEZE KWA KINA SANA....HAPENDI KUMUONA DEREVA ANAYEKIMBIA ILI MFIKE MAPEMA.MATAJIRI WENGI WANAPOONA GARI IMEFIKA MAPEMA WANACHEKELEA BADALA YA KUHUZUNIKA.
Rip marehem wote,
Majeruhi MUNGU awape nguvu mapema.
 
Ninakubaliana kabisa na wote waliosema sababu ya maafa makubwa katika ajali za mabasi ni mwendo mkali na pia kutozingatia sheria za barabarni. Mimi nilisafiri kwa basi kutoka Mji mmoja wa kaskazinn na basi la Abood. Hadi mwisho wa safari Mungu alituepusha ajali mbaya zaidi ya tatu. Nilimwita kondakta nikamweleza kuwa sisi abiria hatuna haraka hivyo amweleze derva wake aache kukimbiza gari. Lakini habari hii wala hakumfikishia dereva na cha kushangaa abiria wengine wote hawakuonyesha kuguswa na spidi ya dereva. Wakati wa kurudi niliamua kutumia gari binafsi na siku hiyo nilikuta ajali tatu, moja ya hizo ndio ilikuwa imetokea basi matairi yako juu na watu ndio walikuwa wanachomoza. Mimi niaona abiria ni lazima waelimishwe ili waweze kuwadhibiti madereva kama wanaendesha mwendo wa kasi. Lastly, I pray for those who lost their loved ones in this avoidable accident.
 
Kuna haja ya kuongeza tochi za ma-polisi barabarani; na basi yote yafungwe Spidi-gavana kwa lazima ilo lisiwe ombi.

mbona nasikia tochi siku hizi zinanunuliwa? Kwamba anateuliwa wa kutoa fungu kwa siku hiyo kisha anaambiwa location za tochi zote. Ye anatangulia ili kudhibitisha na anawaambia wenzake. Hata njiani utasikia makonda wakipigiana na kuulizana nani kanunua tochi, kisha wanampigia...
 
Back
Top Bottom