Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

EEH Mungu wangu,walaze marehemu wote mahali pema peponi,nchi yetu imepata laana ya nini kila siku watu ni chinja chinja tuu ,mpaka lini jamani
 
Route ya Mbeya-Arusha Sumry hawezi ni bora amwachie Hood.
 
Kuna umuhimu wa haya magari ya sumry kufungiwa....kama kumbukumbu zangu ziko sahihi kuna ile ajali ya barabara ya kwenda mtwara, kule songea kama sikosei na sasa arusha-mbeya na ajari zote hizo watu 10+ walifariki, tatizo ni ubovu wa magari au uzembe wa madreva au rushwa za traffic wanaochhukua hela na 'kusamehe' ubovu wa magari
 
Nasikia na Rose Muhando kafariki wenye taarifa mtujuze kwa uhakika zaidi
 
RIP our fellow citizens. Muhimu sasa kwa Sheria ya Road Traffic Act ibadilishwe
hasa ktk kipengele cha adhabu badala ya kifungo cha miezi michache au faini isiyozidi
50,000 sasa siwe kifungo cha miaka kumi au maisha na fain iwe kubwa kwa dreva atakaeua kizembe,
Pili kampuni ziwape mikata ya ajira na mishahara mizuri kuwaondolea stress wawapo barabarani
itamfanya dreva aheshimu kazi yake na kujali maisha ya watu kwani wengi hawana mikataba
na hajui hatma ya kibarua chake wanaendesha tu magari,Tatu kila kampuni ihakikishe inaajiri
madreva waliofuzu mafunzo kupitia chuo cha usafirishaji au kusomea Veta kama kozi,
Nne mabasi ya abiria yakaguliwe kila mwezi kuangalia ubora wake..PCCB wangejitoa kusafiri
na haya magari kila siku kwa kupeana zamu kama mojawapo ya kazi yao
hii ingesiaida pia kukomesha vitendo vya rushwa kwa Trafic kwani wangefanya kazi ya ukaguzi na usalama.
Huo ni mtizamo wangu kwani Tunazidi kuangamia kila kukicha.
 
Askari wa barabarani mbeya, morogoro ni wazembe kupita kiasi tunaotumia hii barabara huwa tunaona huwezi kuona au kukuta basi lipo speed kali Iringa. Kila siku trafic wanauza sura na kubishana na wamiliki wa mabasi kwenye tv mara vizibiti mwendo mara kamera.. Poleni sana wafiwa na majeruhi.
 
kati yahao waliopoteza maisha je

ni watoto wangapi watabakia mayatima? ni wanawake wangapi watabakia wajane? ni nguvu kazi ngapi zimepotea??

Mungu zipokee roho zao!!
 
Basi la kampuni ya Sumry likitokea Arusha kuelekea Mbeya, limepata ajali maeneo ya Igawa, kilometa 140 kutoka mji wa Mbeya. Basi hilo likiwa mwendo mkali, tairi la mbele lilipasuka na kupelekea kupinduka kwake. Watu 13 wamepoteza maisha yao papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya.

Habari zaidi zinasema waliokufa wameshafikia 15[/QUnOTE]Hawa Sumry wana dhamira gani na maisha ya watu hii ni ajali ya 3 sasa ndani ya muda mfupi..
 
Iam giving my deepest condolence to those who have lost their beloved ones. Let almight God give them the heart of patience at this difficult period. Amen
 
jana usiku gari hili lilinipita pale ifunda.......likiwa na mwendo mkali sana na yanafukuzana na hood..........
 
Kwa alieangalia taarifa ya habari ya juzi Ijumaa TBC 1, basi la Sumry lilijaza abiria kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya waliosimama kuwa wengi kuliko waliokaa, abiria wakatoa taarifa polis na kweli gari lilisimamishwa, cha ajabu askar aliangalia tu na kuruhusu gari kuendelea na safar, leo yametokea maafa kwa gari hilo hilo tena, kwa nini hii kampun isifutiwe leseni?????

Hapana mi naona kusiwepo na Trafic,kwa sababu uwepo wao hausaidii kitu,kazi yao kubwa ni kubanana na daladala tu,mabasi makubwa hawana habari nayo kabisa.
 
... kampuni ya sumri ni kati ya kampuni bora kabisa ya usafirishaji nchini nategemea watashiriki kikamilifu katika kusaidia wafiwa na majeruhi wote
Nani kakuambia atawasaidia? Mwarabu mshenzi sana yule, iliwahi kutokea ajali kama hiyo, akamfunga jela kondakta eti kwa kuwa TV iliyokuwamo kwenye basi imepotea! Sasa wewe ajali inatokea, anaanza kufungua kesi ya upotevu wa vitu vidogo vidogo kama TV anaacha kuangalia wafu na majeruhi, leo hii ndio amsaidie nani? Huyu jamaa anatoa watu kafara sana tu!
 
Ajali zote za Scandnavia hazijawahi kuua watu zaidi ya watano kwa gari moja!
 
Inasikitisha kuona ajali zinazidi kila kuchwapo, na nyingi zikichangiwa na uzembe wa madereva kutokujali sheria za barabarani. Napenda kuwataarifu sumatra kukagua leseni itapunguza kwa kiasi kidogo tu kupunguza ajali hizi, kwa sababu mara madereva hawa waendapo kutahiniwa kwa ajili ya kupata leseni huwa wako fresh na maanisha hawajachakachua akili zao kwa vilevi mbalimbali kama vile pombe, bangi , mihadarati n.k.
Ni ushauri wangu kwa serikali kufanya zoezi la kushtukiza mara kwa mara kwa madereva hawa kupimwa vilevi aidha wanapotoka stendi au kuweka vituo katikati ya route ya barabara. vifaa vya kisasa vipo ambavyo havichukui zaidi ya dk 3 kupata majibu. nimefanya kazi kwenye migodi tofauti wamefanikiwa kudhibiti ajali ndani ya migodi kwa utaratibu huo, Majibu ya kilevi kama pombe unayapata ndani ya sekunde 3 kwa kupuliza, bangi na madawa kwa kupima mkojo ndani ya dk 2 unapata majibu. vilevi vinafanya mtu yyt kuwa na maamuzi yasiyo sahihi na ujasiri usiokuwa yakinifu. mwisho nitoe pole kwa watanzania walioadhiriwa kwa namna moja au nyigine kwa ajali hizi.
serikali msione uchungu kununua vifaa hivi vitatusaidia kupunguza ajali na kuokoa maisha ya kitanzia
 
Back
Top Bottom