Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, hawajarie roho ya uvumilivu na ujasiri wote waliopoteza ndugu zao.
 
inasikitisha sana du! moja wa mashuhuda wanasema basi iliovateki kwanye mwinuko.
Ushauri wangu kwa serikali siyo kupitia leseni upya ila kuwe na utaratibu wa kupima madereva pombe, bangi na madawa ya kulevya kabla ya kuanza safari. Hilo linawezekana na litapunguza ajali
Well said!!
 
Aiseeee!!!
RIP kwa waliopoteza maisha na pole nyingi kwa wengine wote ambao ajali inawahusu kwa namna moja ama nyingine!
 
Naomba mwenye taarifa kuhusu ajali za mabasi ya abiria huko Shinyanga atujuze.Nimesikia imesomwa kwenye taarifa ya saa 2 jioni ya leo ITV, lakini sikuweza kuiona kwani nilikuwa mbali na TV.
 
Mungu awaponye majeruhi, na pole kwa ndugu wa marehemu, sijui hawa madereva huwa wanapandwa na wazimu gani jamani. Gari zo
 
Inasikitisha sana watu kupoteza maisha kwa ghafla.Nawaombe majeruhi wasipate ulemavu wa kudumu, wapone haraka waendelee na harakati za maisha.Mungu awafariji wafiwa wote waliopata taarifa za ghafla za kuodokewa na ndugu zao.Huenda wangine waliopoteza maisha walikuwa ndio tegemeo la familia, Mungu awape familia hizo upeo wa haraka wa namna ya kuendesha maisha yao baada ya kuondokewa na waliowategemea
 
WATU 15 wakiwemo watoto wawili, askari polisi mmoja wa

jijini Mwanza wamepoteza maisha na wengine 67 kujeruhiwa

vibaya katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya

Sheraton lenye namba T 268 AJC na basi la Bunda Expres

namba T 810 BDW baada ya kugongana uso kwa uso eneo la

Kijiji cha Chibingo Wilaya ya Geita mkoani Mwanza.

Ajari hiyo ambayo imetokea jana mjini hapa majira ya saa

tatu asubuhi eneo la barabara kuu ya Mwanza-Bukoba

imehusisha mabasi mawili pamoja na roli la mizigo aina

ya Fusso lenye namba za usajili T 823 BDV baada ya basi

la Sheraton lililokuwa likitoka Ushirombo Shinyanga

kwenda Mwanza, kutaka kulipita lori lililokuwa likipanda

kilima cha Chibingo.

Taarifa zinaeleza kuwa kabla ya kulipita gari hilo

lilikutana uso kwa uso na basi la Bunda lililokuwa

likitoka mkoani Mwanza kuelekea Karagwe Mkoa wa Kagera

na ndipo ajali hiyo ilipotokea.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo

imesababishwa na mwendo kasi wa madereva wa mabasi hayo

huku yule wa basi la Sheraton akitupiwa lawama kwa

kushindwa kufuata sheria za barabarani kutokana na

kutaka kulipita gali lililokuwa kwenye kilima bila

kuhofia atari yoyote eneo hilo.

“Tulikuwa tukitokea Shinyanga kwenda Mwanza na basi la

Sheraton tulipofika Kijiji cha Chibingo dereva wetu

alijalibu kulipita gari la mizigo, lakini alishindwa

kulimudu gari kisha kugongana uso kwa uso na basi la

Bunda hali iliyosababisha vifo…huu ni ukiukaji wa

sheria za barabarani,” alisema, Yunusu Mathias.

Mmmoja wa majeruhi, Johnas Kalokola ambaye ni mwanafunzi

wa Sekondari ya Ihungo Bukoba, alisema dereva wa Bunda

alijitahidi kulikwepa basi la Sheraton kwa kunusuru

maisha ya abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Karagwe,

lakini kutokana na mwendo kasi wa mabasi hayo

yaligongana na baadhi ya abilia kupoteza maisha, viungo

vya mwili na mali zao.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita, Dk.

Abdallah Dihenga amethibitisha kupokea miili 15 na

majeruhi zaidi ya 60 na kuongeza kati yao watu sita

wamepelekwa katika hospital ya rufaa ya Bugando Mwanza

baada ya hali zao kuwa mbaya.

Alisema madaktari wanaendelea kuwahudumia majeruhi hao

na hali zao zinaendelea vizuri baada ya wengine saba

kutibiwa na kuruhusiwa, huku akiwataka ndugu, jamaa na

marafiki kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kutambua

miili ya marehemu ambao wamehifadhiwa chumba cha maiti

hospitalini hapo.

Kutokana na ajali hiyo mamia ya wananchi wamefulika

katika eneo la tukio wakisaidia kutoa miili ya marehemu

na majeruhi katika magari yaliyo gongana uso kwa uso

licha ya zoezi hilo kuwa gumu kutokana na ukosefu wa

vifaa vya kutoklea huduma ya kwanza .

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Philemon shelutete na Mbunge wa

Jimbo la Busanda, Lolensia Bukwimba ambao wamefika eneo

la tukio na kueleza kusikitishwa na ajali hiyo na

kutamka ni janga la kitaifa, hivyo kuwataka Watanzania

kuomboleza juu ya vifo v ya wananchi hao.

Hata hivyo Shelutete amewataka wamiliki wa magari ya

abiria kuajiri madereva wenye ujuzi wa kutosha kwa lengo

la kupunguza ajali na kudai iwapo madereva hao

wangezingatia sheria za usalama ajali hiyo isinge tokea.

Hii ni kwa hisani ya Ajali ya kutisha, 15 wafa, 67 wajeruhiwa | TheHabari
Jamani hebu tupeni updates mpya kwa hali hii tutakufa mpaka lini kwa ajali???
 
mi kinachonipa uchungu zaidi ni kauli za viongozi, mf huyo anaposema wamiliki waajiri madereva wazuri ana maanisha nini? Afu ni hatima ya hao waliokufa? Hii inaonesha ni kwa jins gani tunachukulia vifo vya watu kawaida, imekuwa wimbo kila siku lakin hakuna mabadiliko, hawa madereva huwa wanawahi wapi? Kwa nini wasijifunze kupitia matukio ya mbeleni? Yani haina hata miez 2 haijapita tngu 2wapoteze akina Issa Kijoti chanzo kikiwa ni spid lakin bado madereva hawajifunzi. Mi naona ni bora tutembee kwa miguu yetu... Cdhani kama cc kwa cc 2tagongana. Inasikitisha sana.
 
Madhara ya vyombo vya moto ni hatari sana kwa maisha ya watumiaji wake.
Tunasema haya leo tukiitazama ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi mawili na lori iliyotokea katika wilayani Geita jana asubuhi. Hadi jana jioni watu 16 walikuwa wamethibitika kufa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika janga hilo la kusikitisha.
Tunachukua fursa hii kuwapa pole wote waliofiwa na ndugu au jamaa katika ajali hiyo, tunawaomba wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao.
Kadhalika, tunawapa pole majeruhi wote wa ajali hii, tunawatakia uponaji wa haraka ili wasimame tena na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo yao na familia zao, lakini pia katika ujenzi wa taifa.
Kwa hakika wimbi la ajali limekuwa kama ni jambo la kawaida mno katika barabara zetu zote kubwa nchini, mfululizo wa ajali zinazokatiza maisha ya mamia kama si maefu kila mwaka zimekuwa zikiendelea kana kwamba hakuna njia ya kubadili hali hii.
Kwa bahati mbaya sana, kila ajali inapohusisha basi la abiria utasikia kwamba chanzo cha ajali ni uzembe, ama wa dereva au uimara wa chombo anachoendesha, lakini pengine kutokana na shinikizo la abiria au kutimiza hesabu ya siku ya mwenye chombo.
Sehemu nyingine tumesikia kwamba askari wa usalama barabarani wenye wajibu wa kudhibiti vyombo vya usafiri barabarani, nao wamekuwa na sehemu yao katika ongezeko la ajali hizi; ni nadra sana kwa askari hawa kufanya ukaguzi wa kina wa vyombo vya usafiri vilivyoko barabarani, ama kutokana na kazi hiyo kuwa kubwa mno huku idadi ya askari ikiwa ndogo, au kwa sababu tu ya kubweteka.
Kwa habati mbaya sana gari bovu kabisa linaweza kuwa barabarani kwa sababu tu dereva wake amewawezesha trafiki, tumeshuhudia magari mengi yakifia njiani, lakini mengine jinsi yanavyoonekana unajiuliza mara mbili kama trafiki kweli wako barabarani na wako makini katika kutimiza wajibu wao kwa kiwango gani.
Kwa mfano matukio ya malori kujaza mizigo kupita kiasi, kuharibika na kuachwa katikati ya barabara bila ishara yoyote ya hadhari kwa watumiaji wengine wa barabara, ni matukio ambayo yanafanyika mbele ya macho ya trafiki, lakini wanayaacha kana kwamba ndivyo sheria za usalama barabarani zinataka mambo yawe.
Tungependa kusema kwamba katika zama za sasa za mtandao wa kompyuta ni rahisi na inawezekana sana vyombo vyote vya usafiri, hasa vya abiria vikaingizwa kwenye mtandao ambao unaweza kuvifuatilia juu ya mwenendo wao vikiwa barabarani; kwa kufanya hivyo kwa mfano, itakuwa ni rahisi sana kujua nani anakwenda kwa mwendo gani na kisha hatua za hadhari kuchuliliwa kabla ya ajali kutokea.
Tunafikiri wakati sasa umefika wa kutumia maendeleo haya ya tekonolojia kutatua matatizo muhimu ya kijamii kama haya ya ajali za kila siku ambazo zimekuwa zikikatiza maisha ya wapendwa wetu, kusababisha familia hasara kubwa, lakini pia likipunguza nguvu kazi tegemeo kwa taifa hili.
Ni kwa maana hiyo, tunasema sasa tunahitaji ubunifu katika kukabiliana na ongezeko la ajali hizi.
 
tatizo rais wetu anaamini kuwa kila mtu anaweza kutekeleza majukumu yake bila kusimamiwa au kuadhibiwa.......aibu kila siku watu wanakufa aibu ......hakuna ajali tanzania.....tafsiri ya ajali ni kitu kisichoweza kuzuilika ........hizo crash za bongo zinazuilika kwa asilimia 100% tatizo wasimamizi wa barabara wamekuwa corrupt lakini mkwele halioni hilo......fukuza watu kazi?? Kagame ni mfano wa rais wa kuigwa nchi inakwenda mungu rudi tuokoe tanzania
 
Basi la kampuni ya Sumry likitokea Arusha kuelekea Mbeya, limepata ajali maeneo ya Igawa, kilometa 140 kutoka mji wa Mbeya. Basi hilo likiwa mwendo mkali, tairi la mbele lilipasuka na kupelekea kupinduka kwake. Watu 13 wamepoteza maisha yao papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya.

Habari zaidi zinasema waliokufa wameshafikia 15
 
Inasikitisha sana. Inasikitisha kwa sababu watu wamepoteza maisha yao lakini pia inasikitisha kwa sababu ni kama vile Watanzania hatujifunzi.

Sijui hizi ajali hadi ziue watu kiasi gani ndo tupate ufunuo kuwa aha kumbe zinatumaliza hivi! Ukiangalia mabasi mengi ya abiria Tanzania ni makuukuu mno. Ingekuwa kwenye nchi zilizoendelea yangekuwa yameshapigwa marufuku kuwa barabarani na kubeba abiria.

Sasa jumlisha huo ukuukuu na mwendo kasi ambao madereva huendesha unachopata ni majanga kama haya. Lakini licha ya ukuukuu wa hayo mabasi kinachosababisha ajali zaidi ni mwendo kasi usio hata na maana. Kwa ujumla watu Tanzania hawana ustaarabu kabisa wa barabarani. Wanaendesha kama vile hawajali maisha yao.

Aaah ngoja niishie hapa maana nisije kuambiwa huo ndo utamaduni wa Mtanzania na mimi najifanya najua sana. Pole zao waliofiwa na walioumia.
 
Nimeambiwa na mmoja wa kondakta wa Sumry kwamba watu 17 walikufa papo hapo na majeruhi waliobaki wapo kwenye hali mbaya. Maiti wapo Hospital ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha ajali ilikuwa ni tairi la mbele kupasuka lakini maafa makubwa yametokana na mwendokasi wa dereva. Gari ilipinduka na kutambaa kwa mgongo matairi yakiwa juu mwendo wa mita kama 500.

Dereva alikata roho papo hapo.Kama gari ingekuwa mwendo mdogo maafa yasingekuwa makubwa kiasi hicho hata kama tairi ilipasuka. Inasikitisha sana roho za watu wasio na hatia kuondolewa kikatili kila siku.

Sijui kama tuna chombo makini cha kusimamia usalama barabarani.
 
Sijui kama tuna chombo makini cha kusimamia usalama barabarani.

Hicho chombo cha kusimamia kitoke wapi? Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Kilichopo sasa hivi ni ghasia na vurugu mechi tu. Halafu cha kushangaza sasa ni kama vile hatujali au hatuoni ubaya wowote ule na yanayoendelea.

Ajali ndiyo hutokea. Hilo silikatai. Lakini ninaamini kabisa kuwa nyingi ya hizi ajali zinazuilika. Ila kwa vile inaonekana kama hatuoni ubaya wowote na jinsi mambo yalivyo, acha tu zitumalize.
 
Kwa alieangalia taarifa ya habari ya juzi Ijumaa TBC 1, basi la Sumry lilijaza abiria kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya waliosimama kuwa wengi kuliko waliokaa, abiria wakatoa taarifa polis na kweli gari lilisimamishwa, cha ajabu askar aliangalia tu na kuruhusu gari kuendelea na safar, leo yametokea maafa kwa gari hilo hilo tena, kwa nini hii kampun isifutiwe leseni?????
 
Back
Top Bottom