watanzania wenzangu poleni tena kwa kuondokewa na wapendwa wetu takribani kumi na nne waliokuwa wanasafiri na basi la sumry kutoka arusha kwendam mbeya usiku wa juzi. kama vile tumezoea vifo hivi bado hatujifunzi kuwa ajali hizi zina mkono wa binadamu na wala siyo makusudi ya Mwenyezi Mungu.
leo nimesoma magazeti yakinukuu salam za rambi rambi alizopelekewa mkuu wa mkoa wa mbeya na rais wetu bwana JK. jk amesikitishwa sana na ajali hizo na tena amewaomba wafiwa wawe watulivu. tofauti na ajali nyingine za nyuma ambazo huwa anawaonya madereva kuwa makini hii hakufanya hivo. pengine wengine mtawaza kuwa rais wetu amechoshwa na ajali za kila mara, lakini ukweli jk anaujua yeye mwenyewe, na huu ndo ukweli;
- mnamo wiki chache zilizopita, jeshi la polisi lilionya kuwa sumry waache kuendesha magari mabovu njiani ambayo magurudumu yake yameisha, lakini onyo hilo halikutekelezwa.
- abiria waliopona katika ajali ile, wanaeleza jinsi dereva alivyokuwa anaendesha kwa mwendo kasi huku akibujia mirungi, na kila walipomwonya hakuwasikia, sikio la kufa halisikia dawa
- kila kituo cha polisi walikopiata, basi lilikuwa linakamatwa na polisi lakini dereva na kondakta R.i.p walikuwa wakiitwa nyuma ya basi na kumalizana na polisi.
- ingawa miaka ya nyuma safari za mabasi zilikuwa zinaishia saa nne usiku, sheria hii iliondolewa na jshi la poisi kwa amri za mamlaka ya juu, hasa kutokana na mabasi ya sumrny na hood kumilikiwa na wanasiasa mafisadi wa nchi hii.
kwa hiyo jk kama tulivhomzoea, rais pekee katika sayari hii, mwenye majeshi, mahakama., na executive powers ambaye anagwaya kwa mafisadi wanaonyelelea nafasi yake, ambao sasa wako mlangoni kusambaratisha chama chake na kumfanya gorbachev wa afrika mashariki hawezi kuona haya kwa sababu:
mabasi ya summry yanamilikiwa na mama zakhia mehji, huyu ndo yule mama aliyeshirikiana na fisadi namba wani marehemu bilali wakakomba akaunti zote za EPA, sasa wanawafunga akina maranda wakati rafikia zake akina rostam na kagoda bado anasita kuwaleta pale kisutu
kampuni hiyo ya sumry ilikuwa inaingiza magari nchini na kuyasajili kama pikipiki kukwepa ushuru, mama meghji nafahamu sana hili, walikamata machache pale mbeya, laikini wale maofisa wa TRA waliokamata yale magari wanajua kilichowatokea.
askari waliokataza haya magari yasitembee, hawana uwezo wa kufua dafu mbele ya jk kupitia kwa mama meghji mweka hazina mpya wa ccm, ambaye ni mmiliki wa sumry asiyetaka kununua matairii ya mabsi yake bali kuchuna nauli ya watanzania, waendelee kufa wakati yeye akinyanyua mkono na kusema ccm juu!! ju!!! zaidi.
ni wazi kuwa hawa wote ni mafisadi, NI WAKATI MUAFAKA WA KUANDAA NA KUSHIRIKI SIKU YA HASIRA DSM! NA SIKU YA HASIRA TANZANIA, TUNA KILA SABABU. TUTOE HASIRA ZETU KWA PAMOJA NA KWA PAMOJA TUSHINDA UDHALIMU HUU.