Mliooa mnastahili pongezi

Yaani nikifikiria hii kitu nachoka aiseee.
Navuta pumzi kwanza
 
Mjomba unataka kumkabidhi mtu maisha yako? Wanaume tunakabidhiwaga maisha ya wake zetu na watoto wetu tuyaangalie lakini kamwe mwanaume hatafuti mtu ampe maisha yake alelewe.
kwa hiyo mume ni mfugaji wa binaadam!?
 
Asante kwa kutupongeza,ni maandiko ya Mungu ndio yanatuongoza mkuu ,Mwanzo 2:24(Kwahiyo mwanamume atamuacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja),kwahiyo unakuwa huna hofu,chako kinakuwa chake na chake kinakuwa chako..
 
Asante kwa kutupongeza,ni maandiko ya Mungu ndio yanatuongoza mkuu ,Mwanzo 2:24(Kwahiyo mwanamume atamuacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja),kwahiyo unakuwa huna hofu,chako kinakuwa chake na chake kinakuwa chako..
Amen...
 

Congrats to her jamani! Ni kweli kabisa kila Mtu Ana namna yake na njia yake ya kupita ktk safari hii ya maisha,kuangalia wenzio Kwaweza sababisha ukaona Giza totoro mbele na haimaanishi kushindwa Kwa mwenzio ndiyo kushindwa kwako!cha muhimu ni kuamini na kusonga mbele!
 
Mungu ni mwaminifu kwa kweli nimeamka salama tayari kwa mchakamchaka wa wiki nzima!!!!

Vipi wewe hali yako
Basi ni vizuri kama wiki yako imeanza poa, bila shaka kila kilichopangwa kimeenda vizuri.

Hali yangu si mbaya bibie!
 
Mimi kama mwenyekiti wa mabachelor katika kata ndogondogo za jijini, natoa rai kwa wanachama wote wajitokeze kumuombea huyu mwenzetu.
Maana mara nyingi wanaosemaga hivi, huwa wapo karibu kutumbukia kwenye hukohuko kwa ndoa. Karibu atapotea ndugu yetu.
Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…