Mlinzi wa shule alinilaani, nami nimekuwa mlinzi

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,646
35,979
Ilikuwa 2012 nikiwa kidato cha tano katika shule moja ya serikali hapa nchini. Ile shule ilikuwa ya boarding. Siku moja wakati natoka kwenye kipindi cha dini saa 2 usiku nilipopita getini na wenzangu 2 tukielekea mabwenini nikamuuliza mlinzi maswali ambayo yalimkwaza. Moja ya maswali hayo nilimuuliza analipwa sh.ngapi?

Aisee dunia duara, nami sasa ni mlinzi. Naweza kumtafuta yule mtu nimwombe msamaha. Sina hali ngumu sana ya maisha ila naichukia sana hii kazi. Nalipwa kama 800k hivi, nimeajiriwa permanent na taasisi moja hivi ya serikali tangu 2015.

Mwaka huu namaliza shahada yangu ya kwanza but daaah naona hii kazi inaendelea kuniganda. Wife na ndugu zangu wengi hawajui kuwa mimi ni mlinzi.

Nimejenga kijumba kidogo kwa mkopo, yaani daaah naificha sana title yangu.
 
wapi alipokulaani sasa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamjamwelewa mleta mada, kwa uelewa wangu na kaliba yangu, mletamada ameajiliwa katika moja ya vyombo vya ulinzi. Jukumu kubwa la vyombo hivi ni ulinzi ( kushika mninga). Hivyo yeye atakua ametambua kua tofauti yake na yule mlinzi wa shuleni kwao ni upande wa maslahi tu.
Buddah kabidhi kombati uingie kwenye ulinzi kama wa yule mlinzi wa shuleni kwenu ndio utakapokuja gundua kua ndoto yako itatimia vipi. Acha mitero na uganga wa ajabu pia ulikuwa kiapo mwenyewe.
 
Acha kutudanganya Mkuu Hakuna mlinzi anaelipwa zaidi ya Laki nane kama unavyosema
Labda utuambie unalinda nini ??

I'm on that good kush and alcohol
Labda hujanielewa.
Nimesema mshahara uko chini ya laki nane but nikikusanya na malipo mengine inakuja hiyo 800k na visenti kidogo.
Sema tu salary slip hazionyeshi title ningekutumia pm uione.
Muulize mtu wa hazina yeyote atakuambia.
Kuna wazee hapa walinzi wanakula ndefu zaidi ya hapo.
 
Kila mtu ni mlinzi katika hali moja au nyingine. Mie nina mifugo nyumbani kwangu yaani mbwa akibweka tu naangalia CCTV camera kujiridhisha kama hamna wezi. Yaani kila siku lazima niamke mara nne au tano kuangalia picha la nje

Imekuwa mateso sana kwangu. Nalala usingizi wa mang'amung'amu maana nilishawahi kuibiwa broilers kibao niakaona isiwe tabu niweke CCTV. Ni mateso
 
Pole aisee my fellow guard
 
Back
Top Bottom