Mlinzi wa shule alinilaani, nami nimekuwa mlinzi

hao walinzi wa taasisi maalumu,hatuwahesabu kama walinzi hawako kundi hilo.

tanapa,takukuru,bot,bandari.kote huku kuna walinzi ila ni maafisa ulinzi wa taasisi husika,wanalipwa pesa nzuri tu.

wala huwezi hisi umelaanika kwa kwa kufanya kazi hapo,labda amekuwa supervisor wa guardaworld.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeishi familia ya bandari... unadhani kwanini sikuwataja bandari na nimewataja TANESCO?! Jibu ni hili: Bandari walikuwa wanatumia askari na sio walinzi... mwanzoni walikuwa wanatumia askari wa kawaida (wakiitwa askari wa bandari), na baadae waakawa wanatumia askari wao wenyewe tukiwaita kwa utani Askari Katuni!!

Hali kadhalika TANAPA wanatumia askari! Kinyume chake, TANESCO walikuwa wanatumia walinzi!

All in all, hata mleta mada amesema wazi kwamba yeye ni mlinzi kwenye taasisi, na kwahiyo mjadala ni kuhusu walinzi kwenye taasisi na sio hawa wanaokodishwa kutoka security firms.
 
Hamjamwelewa mleta mada, kwa uelewa wangu na kaliba yangu, mletamada ameajiliwa katika moja ya vyombo vya ulinzi. Jukumu kubwa la vyombo hivi ni ulinzi ( kushika mninga). Hivyo yeye atakua ametambua kua tofauti yake na yule mlinzi wa shuleni kwao ni upande wa maslahi tu.
Buddah kabidhi kombati uingie kwenye ulinzi kama wa yule mlinzi wa shuleni kwenu ndio utakapokuja gundua kua ndoto yako itatimia vipi. Acha mitero na uganga wa ajabu pia ulikuwa kiapo mwenyewe.
kweli poti
 
Ilikuwa 2012 nikiwa kidato cha tano katika shule moja ya serikali hapa nchini. Ile shule ilikuwa ya boarding. Siku moja wakati natoka kwenye kipindi cha dini saa 2 usiku nilipopita getini na wenzangu 2 tukielekea mabwenini nikamuuliza mlinzi maswali ambayo yalimkwaza. Moja ya maswali hayo nilimuuliza analipwa sh.ngapi?

Aisee dunia duara, nami sasa ni mlinzi. Naweza kumtafuta yule mtu nimwombe msamaha. Sina hali ngumu sana ya maisha ila naichukia sana hii kazi. Nalipwa kama 800k hivi, nimeajiriwa permanent na taasisi moja hivi ya serikali tangu 2015.

Mwaka huu namaliza shahada yangu ya kwanza but daaah naona hii kazi inaendelea kuniganda. Wife na ndugu zangu wengi hawajui kuwa mimi ni mlinzi.

Nimejenga kijumba kidogo kwa mkopo, yaani daaah naificha sana title yangu.
Ww ulifanya usaili wa police DPA mwaka 2015, barua yako ya maombi uliandika ukasaini kabisa pale chini, "WAKO MTIIFU" leo hii unawananga police, korosho ww
 
Back
Top Bottom