Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Umenikumbusha Mashiku;hiyo gari ilikuwa inakimbia sana,Musoma Mwamza;hadi kinywaji maarufu pale magamaga(Nyakato-Musoma)kikabatizwa jina hilo
 
watu mmeulizwa kitonga na sekenke upi mkali mnaanza kutaja milima mingine ovyooooooo!
 
yap sekenke ya zamani ilikuwa nouma kwasasa hakuna tatizo
 
Sekenke ndo ufananishe na Kitonga? Are you serious? Hata wakati huo uusemao bado Kitango ni hatarishi mara 100 kuliko Sekenke.Saranda ni kawaida sana pale!
Unaijua Sekenke ya miaka ya 85? mimi milima yote nimeiona sasa hivi Sekenke wachina walivyojenga barabara waliuzunguka mlima.

Wakati ule wa Kamata.
 
kama unataka safari njoo rukwa uende bonde la ziwa rukwa ukutane na kitu cha kona ya mkasi na kaburi wazi,acha Mungu aitwe Mungu mkuu.
 
Milima ipo Nyanda za Juu Kusini...hii ya Kanda ya Ziwa ni cha mtoto sana!
 
senkenke hamna kitu kwa sasa wala kitonga hamna kitu
kwa anae safiri barabara ya kutoka Mbeya-Chunya.kuna mlima unatisha unaitwa #KAWETELE . huu unapa uwanza hadi kumaliza una KM 55. kwenye kilele cha juu kabisa ni sawa na nusu ya mlima kilimanjaro. kona zipo zakutisha na unaweza kupata kizunguzungu kama wewe ni dereva. kibaya zaid kuna sehemu upo kwenye kona kali alafu hujui barabara inakata kushoto au kulia.
Japokuwa Mchina amerekebisha ila bado ni kubaya mno. haswa kipindi cha usiku kunakuwa na ukungu mkali sana

Pale kuna kibao kabisa kimeandikwa ndiyo the highest point in all trank roads in Tanzania!
 
Kwa wale watu wa kusafiri safiri sana,

Kati ya mlima Sekenge uliopo Singida, mlima ulioua abiria kibao kwa ajali zake, yaani mkifika na basi mnasali kwanza. Enzi zile mkifika na basi abiria wanashuka na kutangulia kwa miguu then basi linakuja na mizigo na dereva; na mlima Kitonga wa Iringa wenye kona kibao, upi unatisha sana kwa madereva?

Ahahahaha mkuu umebadirika sana aisee hiyo Id ilizoeleka sana humu ndani kwa kupost utumbo.... Nakumbka wakat nasoma Kigonsera nimepita sana Kitonga, kwenye kona kali ukiangalia chini ni mbali alafu kuna magar unayaona ambayo yalishawahi kupata ajali, kuna dada mmoja nilisafir nae siku moja kiti kimoja hatujuani wala nn, alipofika hapo Kitonga nikashangaa ghafla kanikumbatia kwa uoga maana yy alikuwa kakaa dirishani Ahahahaha! nilifurahia sana nikatamani dereva awe anapanda na kushuka hapo hapo Kitonga. ....
 
kwa sasa hamtakiwi kuufananisha mlima kitonga na senkenke.

Labda kwa maeneo niliyozunguka mpaka sasa angalau uufananishe mlima kitonga na kawetele {barabara ya kwenda chunya kutoka mbeya mjini}, senkenke imebaki historia.
 
Kwa wale watu wa kusafiri safiri sana,

Kati ya mlima Sekenge uliopo Singida, mlima ulioua abiria kibao kwa ajali zake, yaani mkifika na basi mnasali kwanza. Enzi zile mkifika na basi abiria wanashuka na kutangulia kwa miguu then basi linakuja na mizigo na dereva; na mlima Kitonga wa Iringa wenye kona kibao, upi unatisha sana kwa madereva?

mlima sekenke sio mkali bali zamani sekenke ilikuwa mbaya na wala sio mkali kutokana na barabara bt now sekenke hautishi na wala sio mrefu sana... Thus kitonga unatisha kutokana na kona nyingi ....hayo ndio maoni yangu
 
Kwa wale watu wa kusafiri safiri sana,

Kati ya mlima Sekenge uliopo Singida, mlima ulioua abiria kibao kwa ajali zake, yaani mkifika na basi mnasali kwanza. Enzi zile mkifika na basi abiria wanashuka na kutangulia kwa miguu then basi linakuja na mizigo na dereva; na mlima Kitonga wa Iringa wenye kona kibao, upi unatisha sana kwa madereva?

Itategemea unazungumzia nyakati zipi
kwa mfano
kwa sasa sekenke kuna lami
Pia Kitonga zamani ilikuwa ni vumbi na ni single lane gari zinategemea radio call kupigwa ndio iruhusiwe kupanda au kushuka.
 
Ni kweli kitonga zaidi, ila ajabu ni kwamba magari yanaanguka zaidi sekenke kuliko kitonga!! Hasa ukifika ile kona ya mwisho kabla ya darajani pale kama unatokea misigiri huku.. Kila wiki pale maroli yanaisha.
 
Ahahahaha mkuu umebadirika sana aisee hiyo Id ilizoeleka sana humu ndani kwa kupost utumbo.... Nakumbka wakat nasoma Kigonsera nimepita sana Kitonga, kwenye kona kali ukiangalia chini ni mbali alafu kuna magar unayaona ambayo yalishawahi kupata ajali, kuna dada mmoja nilisafir nae siku moja kiti kimoja hatujuani wala nn, alipofika hapo Kitonga nikashangaa ghafla kanikumbatia kwa uoga maana yy alikuwa kakaa dirishani Ahahahaha! nilifurahia sana nikatamani dereva awe anapanda na kushuka hapo hapo Kitonga. ....
Ha ha ha haa.. Mkuu hukuchukua namba???
 
Kwa Tanzania mlima umebaki Ngara K9 (k nine)
Pamoja na NYaishozi.Kwa kila Gari inayopanda lazima iimbe sauti ya kwanza hasa malori.
Scania lazima uweke corolla.
 
Back
Top Bottom