Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

kwani lazima useme ulikua unaenda mahenge kufanya nini? hizo ndo sifa zenyewe. unalala na makaratasi kudadadensa

hahaha! umekosea ungemwambia mlienda kufanya nin halafu uone atakavyo tiririka uongo kama mhaya!
 
Mlima inayotisha Tanzania ni pamoja na kitonga one and two, lushoto, chamanyan Morogoro, na mwingine upo muleba, hii ya senkenge sikuhizi cha mtoto kwasababu ilihamishwa toka senkenge ya kwanza.

Ya Muleba km unaenda Rubya kupitia kamachumu,huo nao unatisha.
 
Sijawahi kupita sekenke ila nimepita Kitonga ule mlima shida yake ni malori yanayoharibika ovyo barabarani na hivyo kuweka possibility za kutokea ajali.
 
Wale wadau wa kimara kupitia chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) kule nyuma kuna ka mlima tishio, yaani zingeongezeka kona mbili tu, Sekenke ingekua cha mtoto.
 
Stamina ana mstari wake unasema"huu mlima kitonga we Lerner ucje kwa spidi" kitonga balaa
 
senkenke hamna kitu kwa sasa wala kitonga hamna kitu
kwa anae safiri barabara ya kutoka Mbeya-Chunya.kuna mlima unatisha unaitwa #KAWETELE . huu unapa uwanza hadi kumaliza una KM 55. kwenye kilele cha juu kabisa ni sawa na nusu ya mlima kilimanjaro. kona zipo zakutisha na unaweza kupata kizunguzungu kama wewe ni dereva. kibaya zaid kuna sehemu upo kwenye kona kali alafu hujui barabara inakata kushoto au kulia.
Japokuwa Mchina amerekebisha ila bado ni kubaya mno. haswa kipindi cha usiku kunakuwa na ukungu mkali sana
 
Namshukuru aliyeanzisha hii mada, imenifanya niende mbali zaidi, hebu ona hii video ya huyu dereva wa kike akiendesha "fuso" kwenye mlima kwenye barabara hatari zaidi. Nikiota video hii lazima nidondoke kutoka kitandani, au niweke godoro chini sakafuni....
https://www.youtube.com/watch?v=G4PVeqj2Nqg
 
Kitonga naifananisha na mlima chiweta wa Malawi
 
Panda same milimani afu ushukie njia ya Makanya!! kitonga cha mtoto saana, hiyo ya makanya balaa mtu uko ndani ya gari afu unatafuta sehemu ndani ya gari ujishike humo ,
 
Duh!hiyo bolivia's road of death haifai hata kidogo nimeiona si mchezo
 
Back
Top Bottom