Camera za Usalama kufungwa Mlima Kitonga ili kudhibiti ajali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1692008582568.png

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama Barabarani ya Mkoa huo, wapo mbioni kuanza utekelezaji wa mpango kabambe wa kuweka camera za kisasa kwenye maeneo korofi kwenye barabara kuu inayounganisha Mkoa huo na Mikoa mingine na kwa kuanzia camera hizo zitafungwa eneo la Majinja Wilayani Mufindi na Mlima Kitonga Wilayani Kilolo ili kupunguza ajali za barabarani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas @salimasas amesema hayo wakati kamati yake ikiongozwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ilipotembelea maeneo kadhaa ambayo ni korofi na yanayoongoza kwa kusababisha ajali nyingi Iringa.

Asas amesema uwekwaji wa camera hizo utasaidia kupunguza ajali barabarani kwasababu zitakuwa zinafanya saa 24 na zikifungwa Polisi katika Ofisi ya RPC, RTO na OCD watakuwa wanaona LIVE kila kinachoendelea Kitonga na kote zilikofungwa, pia amesema Madereva wakijua eneo lina camera watazingatia sheria za usalama barabarani.

Katika ziara hiyo ya siku mbili Kamati hiyo imetembelea Nyang’oro, Mlima Kitonga na eneo la Majinja ambalo lilipewa jina hilo kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Kampuni ya Majinja Express lililogongana na lori la mizigo na kusababisha vifo vya Watu 50 na wengine 23 kujeruhiwa March 11, 2015.
 
Hii ni Blah Blah ya politicians, Kitonga inahitaji kufanyiwa maboresho kuliko camera, kwanza ukitokea juu ya mlima pale walipo machinga wa nyanya ,panua ile sehemu na kuweka kituo cha lazima kwa heavy vehicles zote above 10T to stop, hii itasaidia kupunguza momentum ya vehicles hizi;,tujenge two arrester kwa vehicles zitakazo lose breaks ili ziweze kuelekezwa huko;lami ile iliopo ifumuliwe na kujengwa upya (kama walivyofanya Inyala pass),barabara ipanuliwe kwa kuchonga zaidi zile blind corners;malori yote yanapokua pale Kitonga pass LAZIMA ile 8s rule ya following distance ifuatwe;,small vehicles ziruhusiwe to overtake pale driver anapoona its safe to do so.
 
Shida ya Kitonga sio Camera kuna vitu vya muhimu zaidi ya camera. 1, Kwanz akupanua njia toka chini mapaka juu na kuweka sehemu za kupaki magari kwa dharura. 2, Kuweka vioo maalum vya kwenye kona kuwa msaada kwaajili ya upishano wa magari nyakati zote, rejea njia ya Chirundu mpakani mwa Zambia na Zimbabwe. Sehemu zote zenye kona kali zifanyiwe upanuzi wa kutosheleza magari kupita bila ya shida.
 
Yes mkuu vikiwekwa vioo vikubwa kwenye blind corners vitasaidia sana, yes ile pass ya kutokea Zimbabwe kuelekea zambia karibu na chirundu OSBP, panatisha, pia ya kutokea chirundu border kuelekea kafue, welldone zambia wameondoa all check points kati ya Lusaka na livingstone town, Dar to Moro kuna check points zaidi ya 15 za ulaji!
 
Mkuu Arovera haya yalioandikwa kwenye comment ni kweli?
 
Fikiria uko nyuma ya lori linalotembea 5km/hr! Utamaliza ule mwinuko baada ya muda gani?

Dawa sio kufunga kamera bali kuweka mazingira rafiki slow movers watembee bila kuwachelewesha wenye haraka zao.

Panua barabara au weka barabara mbadala. Simple!
 
Ndio jibu nimepita mara kibao kwenda Mbeya. Ilikuwa zamani ajali sio sasa
Watu 50 wamekufa juzi kwenye ajali ya basi la Majinjah mzee unamlisha matango pori kwa confidence kabisa. Nadhani wewe ndio haufuatilii media za bongo mkuu.

Last month kuna basi ilianguka tena ikafunga barabara luckily hakukuwa na vifo.

So huu mjadala wa Kamatu ya Ulinzi na Usalama umetokana na matukio kadhaa yaliyofululiza.
 
Watendaji wa Serikali ni ovyo kabisa sana.
Mimi kama mimi naona suluhuhisho la Ajali za Mara kwa Mara pale kitonga na iyo Zambia Road Yote ni Udogo wa Barabara. Sasa Wanatakiwa Wafanye Ujenzi wa Barabara Njia Nne tokea Morogoro Mpaka Tunduma. Hilo ndo suluhisho Muhimu na Zuri kabisaaa.
 
Yes mkuu vikiwekwa vioo vikubwa kwenye blind corners vitasaidia sana, yes ile pass ya kutokea Zimbabwe kuelekea zambia karibu na chirundu OSBP, panatisha, pia ya kutokea chirundu border kuelekea kafue, welldone zambia wameondoa all check points kati ya Lusaka na livingstone town, Dar to Moro kuna check points zaidi ya 15 za ulaji!
Mkuu kweli mtupu shida sijui hawa viongozi wetu kwanini wanajitia upofu na kuto kukubali kufundishika, ni vitu vya kitaalamu na wanavisoma ktk masomo yao ya Engineer na usalama Bara barani , ila kwetu imekuwa kama dhambi kuiga mazuri yenye kuleta tija kwa maendeleo ya Taifa.
 
Back
Top Bottom