Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Mlima Kitonga vs Mlima Sekenke, upi mkali?

Nimeona hatari ya lushoto,kitonga nimepita zaidi ya Mara mia,songea njombe nimepita kwa kawaida,sekenke sijawahi.

Ila mwisho was yote Balaa liko njia ya Chunya,nasikia ndio barabara iliyojengwa juu kabisa juu ya usawa wa
IMG-20170723-WA0013.jpg
bahari kwa Tanzania,Usiku hunipitishi njia ile
 
yote cha mtoto,kuna kitu inaitwa kaburi wazi na kona ya mkasi.toka sumbawanga kwenda ziwa rukwa.we acha tuu.nashangaa hata serikali kutopeleka hili eneo kwenye maajabu 8 ya dunia
Nimewahi sikia kuhusu hilo. Nasikia Waziri Mkuu aliopt kutotumia usafiri wa barabara tena kupitia hapo mahala hapo.
 
Sekenke hamna kitu mzee kwanza unaweza ukapita hapo usijue kama umepita Sekenke labda huko zamani lakini ya leo inazidiwa hata na zile Kona za mtera.

Barabara ambazo huwa napita nasema hapa sijui tena ukiwa umeongozana na Lori lenye mzigo kama alivyosema hapo juu mdau ni pale mtera, kitonga na kule Songea kwa barabara nilizopita hapo ndo nashikilia roho nikipita.
 
Yote hiyo haijafikia ukali wa Kona za mkoa za Chunya.
Barabara ipo kileleni
Huku korongo na huku korongo
Siyo Kona za Kitonga Wala Nyang'olo zinazoikaribia uhatari Kona za Mkoa.
 
Nimeona hatari ya lushoto,kitonga nimepita zaidi ya Mara mia,songea njombe nimepita kwa kawaida,sekenke sijawahi.

Ila mwisho was yote Balaa liko njia ya Chunya,nasikia ndio barabara iliyojengwa juu kabisa juu ya usawa wa View attachment 549894bahari kwa Tanzania,Usiku hunipitishi njia ile
Zile movies za fast and furious franchise ilifaa wangeshoot huku
Panafaa kabisa
 
Mlima Kitonga hapanaa umetia fora ila mlima Sekenke shida yake ni kona kali mto mmoja una madaraja saba just imagine
 
Kwa wale watu wa kusafiri safiri sana,

Kati ya mlima Sekenge uliopo Singida, mlima ulioua abiria kibao kwa ajali zake, yaani mkifika na basi mnasali kwanza. Enzi zile mkifika na basi abiria wanashuka na kutangulia kwa miguu then basi linakuja na mizigo na dereva; na mlima Kitonga wa Iringa wenye kona kibao, upi unatisha sana kwa madereva?
Ile sekenke ya zamani,ulikuwa mlima hatari sana
 
Kwa wale watu wa kusafiri safiri sana,

Kati ya mlima Sekenge uliopo Singida, mlima ulioua abiria kibao kwa ajali zake, yaani mkifika na basi mnasali kwanza. Enzi zile mkifika na basi abiria wanashuka na kutangulia kwa miguu then basi linakuja na mizigo na dereva; na mlima Kitonga wa Iringa wenye kona kibao, upi unatisha sana kwa madereva?
mimi siijui kitonga wala sekeseknke ila nachojua Mlima Ndororo wa kule Mahenge ni mlima mkali kuliko milima yote sema tu wapogoro wanashindwa kujielezea wakavutia watalii kwenda kushangaa ule mlima
 
siku hiz sekenke hakuna mlima ni barabara tu ya kawaida ila kitonga nomaaa,enzi zle tunaenda mza kupita singida na mashiku bus service ni balaa mkuu,
Mashiku Bus Service, enzi za kupandia barabara ya Msimbazi. Unatoka Dar saa 12 asubuhi, mnaingia Singida saa 5 usiku, na mnalala hadi saa 11 alfajiri ndio safari ianze tena kwa hofu ya kutekwa usiku. Barabara zenyewe ilikuwa ni vumbi tupu.
Kutoka Kahama saa 12 Alfajiri na kufika Bahi saa 4 usiku na inabidi kulala uondoke saa 12 alfajiri.
Kuepuka hizi adha ndipo ikawa tunapitia Kenya kuja Dar au kwenda Mwanza enzi za TAWFIQ na TAKRIM
 
mimi siijui kitonga wala sekeseknke ila nachojua Mlima Ndororo wa kule Mahenge ni mlima mkali kuliko milima yote sema tu wapogoro wanashindwa kujielezea wakavutia watalii kwenda kushangaa ule mlima
Ndororo nimeipanda mwaka 1997 mpaka 2000 kwa kutumia landrover 109 zilizojaa mizigo halafu abiria tunaning'inia kwenye mabomba. Nyakati za masika ilikuwa tunashuka kule chini mlima unapoanzia, then tunapandisha kwa miguu hadi juu huku gari ikipanda na mizigo.
 
🫡

Ova
 
Back
Top Bottom