Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando apata ajali ya gari

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,142
2,000
MKUU wa wilaya ya Morogoro, Albert Msando amepata ajali maeneo ya Dakawa mkoani Morogoro baada ya gari aliyokuwa amepanda kugongana uso kwa uso na gari jingine dogo.

Ajali hiyo imetokea wakati mkuu huyo wa Wilaya akiwa kwenye msafara wa ziara ya waziri Mkuu uliokuwa unatoka Dakawa kuelekea Morogoro mjini leo Jumamosi, Agosti 14, 2021.

Mkuu wa wilaya pamoja na dereva wake wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
===
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Albert Msando amepata ajali ya barabarani katika eneo la Dakawa nje kidogo ya Morogoro.

Ajali hiyo ilitokana na gari aliyokuwa amepanda Msando kugongana uso kwa uso na gari nyingine.

Mkuu huyo wa wilaya na dereva wake wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Pia, Soma=> DC Msando na DC mwenzake wahamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini wako stable!


1628965793221.png
IMG-20210815-WA0007.jpg
IMG-20210815-WA0000.jpg
IMG-20210815-WA0004.jpg
 

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
924
1,000
Atapona TU, mwambie tozo za miamala zitagharim matibabu yake asijali, pia kuhusu Hilo gari, tozo itanunua jipya

Huyo dereva wa gari jingine, aombe afe TU vinginevyo atasota gerezani
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
14,113
2,000
Pole sana kaka yangu Albert, dereva wako na wengine

Mungu awanusuru na lolote baya na awape familia yako utulivu

Uko kwenye maombi yetu
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,311
2,000
Maeneo haya ndipo alipopatia ajali hayati waziri mkuu Edward Moringe Sokoine hiyo barabara imenyooka kama rula na hakuna matuta ijapokuwa wapo trafiki wanaojificha pembeni mwa barabara kuvizia wenye mwendo kasi

Pole DC Abert Msando-Esq, pamoja na majeruhi wengine
 

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,845
2,000
Mbona hakuna gari ya Mkuu wa Wilaya kati ya hizo mbili? Au lake lilikuwa bovu akaamua kupanda hilo la DFPA?

Na ilikuwaje msafara wa Waziri Mkuu usisafishiwe njia?
Itakua gari lake lilitumika na ugeni, hapa tatizo/kesi lipo kwa OCD na RPC kwa uongozaji mbaya wa msafara au Taasisi iliyomuazima gari DC dereva aliyepewa majukumu hana weledi wa kazi za msafara. Kama Mkuu huyo wa Taasisi pia aliombwa aruhusu gari aendeshe dereva mwenye uzoefu akagoma imekula kwake.

Kwa kifupi hapo kuna mtu atasimama kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom