Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi awasamehe waliofukuzwa JKT, watakiwa kurudi jeshini

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa vijana 853 kati ya 854 (mmoja alifariki) waliofukuzwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Aprili 2021 kwa makosa ya kinidhamu.

Jenerali Mabeyo ameagiza vijana hao warejeshwe katika kambi za JKT tayari kuanza mafunzo.

"Vijana wa JKT 853 waliosamehewa wapokelewe ifikapo March 12, 2022 na watakapokelewa katika Kambi moja tu, kambi namba 841 ya JKT ipo Mafinga Iringa.

"Katika msafara wa mamba na kenge watajipenyeza, niwaombe Vijana ambao hawahusiki na msamaha huu wasijipenyeze, Vijana hawa 853 orodha yao yote imeandaliwa na tumefanya utafiti mpaka kwenye ngazi zao za Familia, hata makundi yao ya damu kwa kila mmoja limeorodheshwa kwa hiyo udanganyifu hautojitokeza utapimwa kwa jina picha na damu yako," amesema Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ).

Pia, soma:

1). JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi
 
Hatua nzuri sana! Afande Mabeyo ameonyesha ukomavu wa kiongozi! Mungu akuongezee maisha marefu Afande CDF! maisha ya vijana hawa yanabeba maisha ya watu wengi sana!

naomba ikikupendeza uwarudishe makomando wengi ambao pia walitolewa kwa makosa ambayo hayaliathiri jeshi letu!

mie naamini walifunzwa kwa gharama kubwa za sisi walipa kodi! ni vijana wetu hawatakiwi kurandaranda mitaani kama machinga kwa waliyopitia katika mafunzo!
 
Hii hatari maana wengi wamebebwa na wanasiasa wakubwa
Watoto wa masikini wataendelea kuwa watazamaji
 
Hivi hawa vijana ni kwa mujibu wa sheria au ni permanent...?
 
Mungu ampe maisha marefu huyu mzee mwenzagu huyu, huwa inafikirisha sana kuona mtu anafukuzwa kazi pasipo hata kupewa onyo na mara nyingi viongozi wenye roho za korosho kama hizo huwa wana majuto mengi sana na wengi wao huwa vichaa enzi za uzee.

Binadamu mwenye akili timamu na anayetambua nini maana ya maisha huwezi mkuta anafurahia kumfukuzisha mtu kazi.

Pongezi za dhati zimuendee huyu mzee huwenda hata wale walinzi wa mbowe watarudishwa kambini kuendelea na majukumu yao ya kawaida
 
Safi sana Mabeyo haiwezekani asamehewe gaidi mbowe alafu vijana wazalendo waliojenga ukuta wa Mererani na Ikulu ya Dodoma waachwe wakiteseka mitaani
Kwani ukitoa maneno ya busara utapungukiwa nn. Hivi hizo chuki mnazopanda mnapata faida gani nyie kima?
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa vijana 853 kati ya 854 (mmoja alifariki) waliofukuzwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Aprili 2021 kwa makosa ya kinidhamu.

Jenerali Mabeyo ameagiza vijana hao warejeshwe katika kambi za JKT tayari kuanza mafunzo.

"Vijana wa JKT 853 waliosamehewa wapokelewe ifikapo March 12, 2022 na watakapokelewa katika Kambi moja tu, kambi namba 841 ya JKT ipo Mafinga Iringa.

"Katika msafara wa mamba na kenge watajipenyeza, niwaombe Vijana ambao hawahusiki na msamaha huu wasijipenyeze, Vijana hawa 853 orodha yao yote imeandaliwa na tumefanya utafiti mpaka kwenye ngazi zao za Familia, hata makundi yao ya damu kwa kila mmoja limeorodheshwa kwa hiyo udanganyifu hautojitokeza utapimwa kwa jina picha na damu yako," amesema Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ).

Pia, soma:

1). JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi
Sawa afande!! Leo nimeamini unayaishi maisha yako sawa na dini yako ya Mkristo Mkatoliki. Huu ni Mwezi wa toba (Kwaresma). Kwa hatua hiyo utakuwa umejisogeza karibu kabisa na Mungu wako. Mwenyezi Mungu akupe kadri ya moyo wako unavyo tamani.
 
Back
Top Bottom