Mkutano wa Mwakyembe na Hoja za Mgongano wa Maslahi

- ...........- Ujumbe wangu kwa Wa-Tanzania wenzangu ni kwamba tusidharau mwiba kwa sababu huwezi kupigana na adui ambaye hujui mbinu zake, adui tunayepigana naye hapa ni too sophisticated kuliko wengi tunavyoamini na kumuelewa, tunamuongelea kama vile ni mtu mjinga mjinga tu mwenye hela basi!, shutuma nyingi tunazomrushia ni za kisiasa tu badala ya kisheria.............William.

Malecela,

thats very true my brother......right now we should think of what willbe his next move...........baada ya kutuchanganya changanya.........very unfortunate....wengi wetu tumeingia kwenye mtego wake.......huku tukifikiri tunatetea fikra zetu.......dah....
 
Kwa nini Rostam alalamikie ubaguzi?.......it tells me a lot of things behind
 
Kwa nini Rostam alalamikie ubaguzi?.......it tells me a lot of things behind

Kweli there is more said without saying, kwanini ubaguzi tu. What should we think is behind all this.

Ameacha kujibu tuhuma zote zile alizo tupiwa siku hile, all he saw was ubaguzi. Sijui zile allegations zingine hazina umuhimu au ukweli.
 
Last edited:
Mtanzania,
.Wapi Sitta amesema hivyo? Hayo ni maneno ya Mwambalaswa, kuna sehemu nyingine nimesoma wameandika Sitta anasema hajasema hivyo. Niliposoma kuhusu mahojiano ya Spika hajaongelea kabisa kuhusu nani ana/hana kosa.


Huyo Mwambalaswa anasema eti hakuna conflict of interest kwa yeye kuwa member wa board ya directors, kuwa mjumbe kwenye kamati ya madini na nishati na kuwa na kampuni ya kufua umeme?

Kamati ya madini na nishati inapojadili TANESCO, inajadili mambo yaliyoamuliwa au kupitishwa na board ya TANESCO. Sasa yeye huko atakuwa anajijadili mwenyewe?
Mkandara, tuachane na ya Mwakyembe, je hata Mwambalaswa hakuna conflict of interest?
Kwa mimi huyu ndio balaa kabisa, inatakiwa aachie TANESCO
Mkuu wangu kwanza nitarudia maneno yangu kuwa kila siku unapofikiria jambo ili kutafuta ufumbuzi au hata jawabu lake ni bora sana utazame WATU na MAZINGIRA yake...

Hivi nyie wenzangu mnaitazama vipi hii Conflict of interest nje ya system nzima!.. jamani serikali haiongozwi na kijiwe ama fikra za kijiweni ila ni system nzima iliyoundwa chini ya katiba inayosimamia maamuzi yote..

Ni katika mwongozo huu ndipo unapoweza kuweka madai yanayohusiana na shinikizo kwa mfano mimi Muislaam na unapotaka kunihukumu kuhusiana na wake zaidi ya mmoja ni lazima ufikirie kama Muislaam ili nami nikuelewe makosa yangu lakini kama utaleta za kuleta kwa fikra za Kikristu tutakesha!.. Ni lazima tutumie kitabu kimoja kinacholinda haki hizo..

Sasa muundo wa System yetu.. Mbunge ni Waziri, Mzsimamizi mkuu wa wizara zetu (Waziri mkuu) ni Mbunge wa wilaya fulani hivyo hivyo utaenda hadi idara, wilaya au kata zetu utawakuta ni watu hawa hawa wakishika nafasi zote zinazohusiana na maamuzi mengi acha mbali kushauri tu..
Kwa fikra za haraka haraka utasema waziri mkuu akiwa Mkerewe bila shaka ataipendelea Ukerewe na neno Kupendelea likazua malalamiko ya Conflct of interest kwa sababu waziri huyo atahitaji kura za wananchi wake uchaguzi ujao..Rais ni mwenyekiti wa CCM na wagombea wote ni wenyeviti wa kamati zenye maamuzi makubwa kuhusiana na vyama husika wakati wao wana interest zinazoingiliana na vyeo ama wenyeviti..

Na kama nilivyosema Madaktari Muhimbili wote wana Zahanati zao nje na mara zote huku refer kwenda kutibiwa ktk Zahanati zao..Na pengine inawezekana kuwa mtu huna Ugonjwa ukaambiwa unaumwa kwa sababu daktari ana own biashara ambayo ni lazima ijiendeshe..

Mawaziri wetu wengi tu wana Hospital, shule, NGO's na inawezekana kabisa matokeo ya shule hizi yakawa mazuri zaidi kwa sababu ya waziri huyo ku own shule hiyo.. tena basi unakuta mtu huyu ni waziri wa Elimu..

Kwa hiyo, fikra kama hizi mkuu wangu haziwezi kujenga nchi ya Kibepari..Ni fkra finyu kwa mapana ya Ubepari kwani hizi ni fikra za Ujamaa (Ucommunist) ambapo hakuna mtu anayeweza kuaminiwa..

Kwa bahati mbaya Tanzania ni moja ya nchi ambazo hazitakiwi kuamini mtu kwani sisi wote mazishi..Kila unalofikiria haliwezekani linawezekana Tanzania, hivyo kama kweli Mwakyembe ana Conflict of Interest ktk fikra za kuwepo ktk kamati hii basi bila shaka Conflict hiyo ipo kila sehemu....

Binafsi maadam Mwakyembe hakuwa na interest yoyote ktk mradi huu wa dharura na mapendekezo ya kamati yake yote yamekuwa (lenga) kwa maslahi ya Taifa na hakika yametuwezesha sisi Kufahamu mengi machafu yanayotendeka nchini pamoja na kwamba yaliathiri baraza zima la mawaziri..hakuna faida yoyote kwa Mwakyembe zaidi ya sifa...

Ni matokeo ambayo Watanzania wengi tuliyasubiri sana na kila siku JK alisema tulete ushahidi.. ushahidi ukapatikana! What more do we want!..
 
Ni alasiri nzuri kabisa chini ya jua hili katikati jiji hili la DSM, niko ofisini mwangu kama mwanachama wa JF nasoma na kuchangia maada mbali mbali, mara nasikia hodi ya uwoga inapigwa, nika-respond kuwa ingia, mgeni huyu hakusikia mpaka pale nilipoenda kufungua mwenyewe. Napokewa na sura ya mashaka mashaka na kijana,mwanafunzi wa chuo fulani cha uandishi wa habari jijini. Nasogeza kompyuta yangu pembeni, ili nimsikilize kikamilifu anasemaje, nimeamua namsomesha fani hii.Nimejiajiri kama mhandisi.

Karibu! Nikaanza kusema, asante mzee akaitikia (acha nijitambulishe kama mwanaJF)
Kijana:Shikamoo mzee!
Mwana JF: Marahaba kijana,
Mwana JF: Karibu kijana, masomo yanasemaje??Kijana: naendelea vyema mzee, samahani nimekuja kuchukua muda wako, najua uko bize sana mzee, ndio maana nimeingia kwa woga, secretary sijamuona sio kawaida mzee, is everything ok here??

Mwana JF: Usihofu, nimekuwa nikipumzika, japo ni saa za kazi, umeme umekatika ghafla, sekretari akataka apige simu akagundua nayo imekatwa japo tumelipa bili, kwa hiyo ameenda kufuatilia haya yote, hatuna umeme kabisa, generator nimenunua wiki iliyopita limekufa, linaonekana lilikuwa feki, japo zuri, so unaniona hapa nilikuwa nasoma soma magazeti yetu kutumia umeme wa betri wa kwenye laptop yangu, vipi kuna tatizo.

Kijana: Pole mzee , kilichonileta hapa, da! Kama hali yenyewe ni hii ningejua ningekuja si nyingine, mzee kwa kifupi nimechanganyikiwa, mzee kuna mambo yananiumiza sana, nimeona nije nisikie unasemaje.

Mwana JF: ( najitengeneza vizuri kwenye kochi) endelea kijana usihofu, vipi ni kitu gani hasa, maana sio kawaida hii, I am getting nervous,umeharibu sehemu??

Kijana: hapana!
MwanaJF: Mhh,! Tell me,

Kijana: Mzee pengine, nitakuudhi!, tatizo langu ni kutaka kukuuliza maswali ya kisiasa hapa nchini, hii pia ni sehemu ya project yangu, ywa mwaka huu wa pili. Nimeonelea niulize watu wa kila fani , wakubwa kwa wadogo, nikaona si vibaya nije kwako mzee wangu nikuulize kuhusu mustakabali wa taifa letu, siasa zetu na mambo mengine mengi.

MwanaJF: (Nikaamka kwenda kuchukua vinywaji kwenye kafriji kangu nikazishika shika kungalia ubaridi). Unatumia soda gani?
Kijana: Yoyote mzee,

Mwana JF:afadhali zina ubaridi,karibu pepsi

Kijana: Asante sana!
Mwana JF: Kijana, unataka kuongelea mambo makubwa sana, siasa?? Leta habari unaanzia wapi?? Ni topic pana sana hii kijana wangu! Mh! Uliza maswali yako, naona umeandika kabisa!

Kijana: Ndiyo nimeandika mzee, lakini yanaweza yakabadilika, mzee unaamini ndani ya CCM kuna viongozi wasafi??

Mwana JF: Kijana mpaka unauliza swali hili, kuna maswali unajiuliza,kwa kifupi nakuambia kwa kujiamini kuwa hakuna! Hata mmoja! Hakuna!!

Kijana: (akiniangalia kwa mshangao), mzee maneno mazito haya, kwa nini unafikiria hivi, una proof??

Mwana JF: Kijana nina wasiwasi umechagua topic ngumu sana!
Tumewapa miaka 40 ya kuongoza, kila kukicha afadhali ya jana, CCM hawa ndio walioifikisha Tanzania yetu hapa, tuna watu, tuna maliasili, tuna sheria na katiba, ila mara zote tunakosa viongozi safi, waliojitoa, wanamfikiria mtanzania wa Masaki na yule wa nzega Tabora. Tuna kila sababu ya kuendelea , kila sababu

Kijana: Kwa hiyo? Si…..

Mwana JF: Subiri! Kijana kila kitu kina kipimo chake na muda, huwa tunapewa probation period miezi 3 hili kuwa approved kuendelea na kazi! Kuna contracts na project zote zinaelezea mwanzo wa jambo fulani na mwisho wake,

MwanaJF: what is contract??

Kijana: mhh, is…..

MwanaJF: A contract is an exchange of promises kwa kifupi, kuna contract za aina nyingi, mpaka Oral or unwritten contract. Kijana, unapotoa fedha dukani upate soda how are sure utapewa soda?? Je akikupa kitu kingine utakubali?

Kijana: Hapana

Kijana: Unataka kusema nini??
MwanaJF: Wanakuja kila baada ya miaka 5, wanaomba kura, wanaapa kwa kutumia vitabu vitakatifu, kuilinda katiba, na kutetea wananchi na kusaidia watanzania!
Kijana: Naanza kuelewa kidogo

MwanaJF: wanateuana, wanapeana vyeo, wanakura rushwa, ufisadi kila kona kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa kwa mkuu wa nchi!, wanalindana, kila kukicha maigizo, CCM hii hii ndiyo imetufanya tuwe maskini, kuna watu wanaishi kama Obama nchi hii, kuna watu wanakosa milo 3 kwa siku! Kuna watu wanasafirisha magari kwa ndege nchi hii, kuna watu wanajifungua njiani kwa kukosa ambulance! Kuna watanzania wanasoma shule za kiingereza tangu utotoni, wakati wko wengine wanasoma shule zisizo na waalimu tangu utotoni!
Kijana: (anashusha pumzi) mzee sasa kwa hiyo unatak..

MwanaJF: Ndiyo , Leo hii kuna watu wanataka watuaminishe kuwa akinawatu kama akina Mwakyembe ni wasafi, akina Kilango ni wasafi na wengine kama hao, kisa kwa sababu wanapinga waziwazi ufisadi, huku wakila na kupanga mipango na hao hao mafisadi,majina yao iliyapite kuchaguliwa yanapitishwa na hao hao mafisadi! wakiomba kura wanataka kupitishwa na mafisadi. CCM imeoza kiasi ambacho mtu yeyote anayeelewa dhana ya usafi hatakiwi kubaki humo! Hata kwa sababu yeyote itakayoonekana ni nzuri! Kwa kifupi hakuna kitu watakachofanya ndani ya CCM kisipitie mikononi mwa mafisadi huu ndio ukweli kijana! Hupo??

Kijana: (akiwa mnyonge) nakusikia mzee!

MwanaJF: Najua huna raha, kazi yangu leo ni kukuweka sawa, ili unapoandika article zako ziwe realistic, na zitoke moyoni, lazima uwaze katika big and different directions!

Kijana: endelea mzee;

MwanaJF: CCM haijaanza leo, wabunge machachari hawajaanza leo, kufunguliwa mashtaka viongozi hakujaanza leo, kwa kifupi hamna jipya, watu ni walewale wamekulia kwenye system na sheria zilezile, kubebana kulekule, kuna wabunge walitikisa nchi hii tangua hata wakati baba wa taifa yuko hai! Ulikuwa mtoto pengine!
Kijana: Tutawezaje sasa kuondoa hii CCM??

MwanaJF: Lazima tufuate kanuni za msingi, unapopiga dawa kuua wadudu ndani ya chumba, huchagui wadudu! Unapiga dawa chumba kizima, wadudu walio na nguvu huwa wanaishi, hawa viongozi wa CCM wanaoonekana wasafi hata kama CCM wataondoka kwenye majimbo yao watasimama tu wataishi watakuwa wabunge kwa chama chochote kile!

Kijana: Mzee unataka kusema hawa watu waondoke CCM ili kuthibitisha usafi wao??

MwanaJF: Umenipata haswaa!, maamuzi ya bungeni, hata siku moja huwa hawatofautiani, wanakuwa pamoja, kwa kifupi kuna vyama viwili nchini?
Kijana: vipi hivyo tena?

MwanaJF: CCM A, na CCM B, CCM A-mafisadi, na CCM B, wasio mafisadi.lakini CCM A+CCM B =CCM! Ni walewale! Ebu ona Lowassa baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu CCM ana cheo gani?? Kwa nini?? Au Mwakyemebe lengo la kuacha kufundisha chuo kwenda kwenye siasa lengo ni nini?? Si pesa?? Au?? Funguka macho! Umeshawaona wabunge hawa wasafi wanakataa pesa za posho bungeni, wakati hospitali ya kisarawe na Bumbuli hazina dawa??
Kijana: Interesting!

MwanaJF: Kwa hiyo mijadala ya nchi hii iko ndani ya CCM wasafi na wachafu, lakini jumla yake ni walewale! Vyama vingine vimezikwa hata vile ambavyo wananchi tungepaswa tujitahidi kuviinua tuwape nchi, tuone sera mpya, na nguvu mpya za kweli, lakini vimeuliwa! Hakuna chama cha siasa kitakachoshika nchi hii mbali ya CCM kama vita yetu tutapigana kama sasa hivi!
(Mara mlango unagongwa hodi, ni secretari)


Sekretari:Boss nimerudi, TTCL walikata simu bahati mbaya!

MwanaJF: Na umeme?

Sekretari: Tanesco wamesema hawataleta mpaka keshokutwa,

MwanaJF: haya, tumezoaea sasa! Asante, wahi nyumbani sasa, nina mazungumzo mazito
Kijana: kuhusu Rostam unasemaje mzee?
MwanaJF: (akimwangalia kijana usoni kwa makini) naona unataka kunafanya kosa la wengi hapa Tanzania.

Kijana: kwa nini
MwanaJF: Ok, kafanya nini??
Kijana: si fisadi??
MwanaJF: kafisadi nini??
Kijana: Kagoda, Richmond, na vitu kibao!
MwanaJF: Kwani yuko jela??
Kijana: Hapana
MwanaJF: Kwa nini? Kama mtu ni fisadi, vithibitishi mnavyo, kwa nini hayuko jela??
Kijana: inabidi uamke, Rostam siyo fisadi kwa lugha ya haraka haraka. Kama angekuwa hivyo angeenda jela tangu tulipoanza kusikia taarifa hizi!

Kijana: unataka ksuema nini tena mzee!

MwanaJF: Kijana katika vita yeyote ile lazima ujue mbinu ya kushinda!, kuandika kwenye magazeti na kumjua kuwa fulani ni fisadi hakuuondoi ufisadi, hata kumpeleka jela kiongozi pasi yeye kuturudishia fedha zetu , hakumsaidii mtanzania wa kawaida! Kusema huyu mtu fisadi, hakutuletei maendela wala tija yeyote, nikwambie kitu??
Kijana: sema

MwanaJF: jamii ya Tanzania imekata tamaa, au imeficha uwezo wao kwenye habari za udaku, kwa sababu tumezoea udaku udaku, jamii yeyote maskini huwa inashiba sana taarifa za kusikia au kupewa moyo, kisaikolojia habari ya kuwa Rostam ni fisadi inawafurahisha wengi, japo haiwaondoi katika matatizo yao! Kwa kifupi akili yeyote fupi iliyodumaa ni ile isiyofikiria kiini cha tatizo inafikiria tatizo wanaloliona, unaufahamu mti nadhani, u mgomba

Kijana: Ndiyo;
mwanaJF: Ukikata majani au matawi, hayataota tena??

Kijana: yataota!

MwanaJF hivi hauoni kuwa , Rostam ni katawi kadogo tu kati ya li jimti likubwa linaloitwa CCM ??

Kijana (anacheka)

MwanaJF: Usicheke, havichekeshi hivi vitu, ni miaka sasa tumesikia Rostam fisadi, mahakama, zipo, rais yupo, wabunge na wanasheria wapo, kila sababu ipo! Kwa nini haendi jela??

Kijana: sijui

MwanaJF: Huoni kuongelea kuhusu Rostam ni kupoteza muda?? Kwa nini tusiwabane hawa viongozi watoa hesabu ya uwajibikaji wo katika hili?? Huoni kijana kuwa kumsema Rostam kwenye magazeti ni swa na kumchoma moto kibaka kariakoo?? Kwa nini tunaona ni hatari kuua kwa mawe, na sio kundika kwa peni??

Kijana: sijui!

MwanaJF: Au ni ile akili finyu ya baadhi ya watanzania ya kuwagawa wezi, kuwa mtu wa serikali akiiba hela ya umma elfu 10 ni afadhali kuliko wa milioni moja?? Kwa nini tusikae chini na kuona ufisadi ji janga la kitaifa ?? hatuoni kunogelea kuhusu Rostam ni kulimit mawazo na uwezo wetu?? Kwani akiondoka Rostam mafisadi hawapo tena?? Rostam anafanya ufisadi na nani?? Peke yake?? How?? Kwa nini tusione tunawajibika moja kwamoja kuzuia tatizo kama ili lisitokee tena, tung'oe mzizi huu na mzizi huu ni CCM na serikali yake??

Kijana: kwa hi..
MwanaJF: Umeshawahi kwenda kwa waganga w kienyeji??

Kijana: huwa nawasikia!
MwanaJF: Basi ,ni sawa na waganga wa kienyeji kutoa shetani mdogo kwenye mwili wa mtu, kwa nguvu ya shetani mkubwa! Ambaye ni hatari mara milioni ya kale kadogo!!! CCM ni shetani likubwa, linajitahidi, liwashtueshtue vishetani vidogo, ambavyo ni fisadi! Ili kuwafurahisha watu, tena mara nyingi , haya majini huwa yanarudia tena mtu yuleyule!!



Kijana: Oho!
MwanaJF: Uwezo wetu ni mkubwa kuliko kumsema Rostam au Mwakyembe, uwezo wetu ni mkubwa unatisha, japo watanzania wengi wameprove ni wazuri kuongea na kuandika, uwaambie tuandamane, hawataki, wengine waambie hata kupiga kura hawataki! Nikuchekeshe!
Kijana: Mhh! ( akiwa haandiki tena)
MwanaJF: Viongozi wengi tuliowaita mafisadi, wamachaguliwa na sisi wenyewe akiwamo huyu Rostam! Waliopatikana na hatia, walipokelewa kama mashujaa! Kana kwamba vita hii tunapigana sisi wenyewe! Kuna tatizo sehemu na tusipogundua tutaandika weee mpaka tukome!

Kijana: Nani wa kuwapeleka hawa wachafu jela?? Nani atawashtaki, ni yule mama mjamzito mwenye kipato cha elfu 2 kwa mwezi?? Au ni yule mmachinga anayeuza vitu tandale, nani wa kumpeleka Rostam na wenzake mahakamani??

MwanaJF: Umeuliza swali, juzi Mwakyembe alisema yeye ni mwansheria, mwanahabari, ana makampuni mengi tu, kwa kifupifedha anayo, maana mahakamani huendi bila pesa! Tena akasema Rostama ni mchafu! Kumbe naye anajua, ila naye anamsubiri fulani ampeleke Rostam mahakamani!!! Kama mbunge anaujua uachafu wa mbunge mwenzake basi anaujua kwa mapana kuliko tunavyodhani! Kwa nini asiwe wa kwanza kutushirikisha tupeleke mafisadi mahakamani??

Kijana? Ndani ya CCM kwa taratibu zao sio rahisi mzee!MwanaJF: Good! Then yu are simply saying, tuwaondoea CCM, kama nilivyosema mwanzoni??

Kijana: ndiyo, sasa kwanini alisema vile??

MwanaJF: alikuwa na haki ya kujitetea, kwani hoja za maslahi hapa haziingiliani na swala lake, watu wamechemsha, hoja yangu ni kuwa hakutakiwa kusema Rostan anaoga maji machafu! Kwani yeye ni mchafu , ni sawa na rais kuwapa muda mafisadi wa madawa ya kulevya, bandarini n.k?? kweli umpe mwizi muda?? Mtu aliyeiba fedha za maskini wa nchi hii??
Kijana: duh! Ni kweli

MwanaJF: Kama Rostam anaoga maji machafu Mwakyembe anaishi kwenye dampo!

Kijana: (anachukua peni haraka) mh!, unasemaje mzee??

MwanaJF: Kama Rostam anaoga maji machafu Mwakyembe anaishi kwenye dampo!CCM ni dampo, ni jalala, anayeishi humo hani-convince kuwa naye ni msafi hata kama atasema msafi hata kama nitamwona msafi, lakini yuko sehemu chafu, anakula, anaongea, anapanga mipango na hawa wachafu! Huyu naye by no means ni mchafu!Tusafishe Tanzania

Kijana: Mzee maneno haya siwezi magumu!
MwanJF: Ni kwa sababu mawazo yetu tumeyaweka upande mmoja, mtu yeyote atakayesema kinyume na Mawazo ya wengi ataonekana mbaya, nikimsema vibaya mwakyembe ntapigwa hata mawe hata kama nitasema sahihi! Kila kitu kina mahali pake, siwezi nikacheza mdundiko kanisani wala siwezi kuimba nyimbo za bikira Maria msikitini. Huwezi kuhubiri usafi ndani ya CCM!

Kijana: mzee asante sana, maneno mazito haya
MwanaJF: Unajua hatari ya kuishi dampo?? Taratibu wadudu wataingia mwilini, hata kama utajitahidi kujisafisha na kuwa msafi, why risk?? Kwanini uiishi kabisa sehemu safi ukafanya mambo yako kwa raha? Kuliko kuwa double standard?? Unafikiri kwenye ile press connferene ya Mwakyembe opponent wake angekuwa mweusi angesema maneno yale??? Kwa nini tumuone Rostam ni mwarabu wakati ni raia wa Tanzania na jela imewekwa kwa ajili ya wote wavunjao sheria??
Kijana: mzee inatosha nimeshapata vya kuandika

MwanaJF: habari ndiyo hiyo hata kama utatukanwa!, ila message sent

Kijana: asante sana mzee, neno la mwisho mzee
MwanaJF: Tuko nyuma ya kila anayeitakia mema Tanzania, walio safi ndani ya CCM, waondoke wajaribu Mrema alsihajaribu, tena wakati Nyerere yuko hai miaka 15 iliyopita!!! Kama wasafi na wachapa kazi popote mtakapoenda mtapokewa ! CCM ilishashindwa siku nyingi! Tuone tufanye nini kwa kuwaza mbali na kuwa upeo mkubwa sio kila kukicha kuwasema watu ambao wanatakiwa kuwa jela au wathibitike kuwa sio wachafu!. Vyama vya upinzani vijipange, sio sawa na vinavyofanya sasa! Vibadilike!
Kijana asante sana mzee kwa kuchukua muda wako
MwanaJF: karibu, so title ya project yako itakuwaje??

Kijana: KAMA ROSTAM ANAOGA MAJI TAKA, MWAKYEMBE ANAISHI KWENYE DAMPO!(CCM-A,CCM-B??)
MwanaJF: Mhh, mi simo, je wakipinga watu hiyo title??

Kijana : wakipinga kwa hoja sina tatizo haya ni maelezo na mawazo ya mtu

MwanaJF: Sasa ni saa 11, jioni unaenda wapi, kwako ubungo??
Kijana: ndiyo mzee:

MwanJF: Itabidi twende wote huwa nakaa mpaka saa 2 usiku kukwepa foleni, leo hata sina umeme hata nikikaa mpaka saa 2 sitakuwa nafnaya kitu, twende pamoja
Kijana: kweli foleni iboa sana!

MwanaJF: Nayo ni Rostam??
Kijana: NO!
(Wote wanacheka na kuondoka)
 
Kijana: Mzee kwa hiyo RA yupo kwenye dampo na 'anakoga' maji taka?

Asante mkuu kwa ubunifu!
 
Kama Rostam anaoga maji machafu Mwakyembe anaishi kwenye dampo!CCM ni dampo, ni jalala, anayeishi humo hani-convince kuwa naye ni msafi hata kama atasema msafi hata kama nitamwona msafi, lakini yuko sehemu chafu, anakula, anaongea, anapanga mipango na hawa wachafu! Huyu naye by no means ni mchafu!Tusafishe Tanzania

Haya chadema mmepewa msemo wa bure hapa! Hizi lugha zikiongelewa mara kwa mara zitawatoa watu nyumbani sikuya kupiga kura wakiwa na hasira. mambo ya "yes we can " huku bado sana hivyo
 

Mwana JF: Usihofu, nimekuwa nikipumzika, japo ni saa za kazi, umeme umekatika ghafla, sekretari akataka apige simu akagundua nayo imekatwa japo tumelipa bili, kwa hiyo ameenda kufuatilia haya yote, hatuna umeme kabisa, generator nimenunua wiki iliyopita limekufa, linaonekana lilikuwa feki, japo zuri, so unaniona hapa nilikuwa nasoma soma magazeti yetu kutumia umeme wa betri wa kwenye laptop yangu, vipi kuna tatizo.

  1. Umeme wa mgao kila siku,
  2. Maji kwa magaloni,
  3. Barabara chache zilizopo hazipitiki kwa msongamano,
  4. Njaa mikoani imeongezeka,
  5. Bandari imegeuzwa kitegauchumi cha maswahiba wasioweza kazi, n.k, n.k.
Huu ni mwaka wa 4 tokea JK awe raisi. List ya matatizo iliyokuwepo alipokuwa waziri inaongezeka urefu akiikodolea macho kama vile hayaoni, bila kutatua lolote.

Hivi kweli Kikwete anaweza kutueleza ni lipi alilofanya kuikwamua nchi kutoka kwenye haya matatizo tokea akalie kiti cha uraisi??
 
Kwi kwi kwi!!! yaani nimecheka leo sina mbavu. Kumbe JF tuna waandishi!

Mkuu, umepigilia msumari kweli kweli!
 
duu jamaa anatisha, mara nyingi makala ndefu kama hizi huwa sina muda wa kuzisoma lakini leo nimejikuta namaliza kusoma kutokana na utamu wake kiasi unakuwa kama unaona jinsi hawa watu wanavyo fanya interview safi sana nimependa hii big up to you..
 
Waberoya,

Kwa kweli hapo umeandika. Hongera sana. Pamoja na kwamba umeiita utopia mimi nadhani hiyo ni zaidi ya utopia. Ni makala iliyonifanya nicheke na kufikiri. Safi sana
 
Duu Weborya!! this is hilarious kind of thinking, nimeisoma yote, nimejifunza kitu...asante sana ROSTAM ANAOGA MAJI TAKA, MWAKYEMBE ANAISHI KWENYE DAMPO

Nadhani hata Muungwana JK anajitahidi kuoga maji ya taka na watanzania tuko kwenye Dampo hatujifunzi kwa ndugu zetu wa Madagascar!
 
Unajua habari zingine unaweza kufikiri unafanya utani, kumbe ikawa na effect kubwa kwa jamii.

Hii article pamoja na kuandikwa kiutani, ina fundisho kubwa mno. Ukiwafikishia vijana wa mitaani, inaweza kuwa na thamani kuliko mikutano 10 ya vyama vya siasa.

Mimi nimeirudia kama mara tano. Inabidi watu kujua mapema, kwenda kuishi dampo 2010 au kuendelea kupiga box.
 
Hapa Waberoya umetoa somo kubwa kwa Watanzania kwa njia ya kipekee.Hatuwezi kuwaamini watu walio ndani ya chama kilicho kichafu.

Ninapopata kigugumizi ni pale ambapo hawa wenzetu ambao wao ni safi lakini hawaungwi mkono na wapiga kura hata kama usafi wao unang'aa kama jua!Je,Jamii imelewa mvinyo gani?

Ni kitu gani ambacho Watanzania hatukielewi hivi kwamba kinatufanya tuendelee na CCM daima??
 
Ni kweli RA ni mbaguzi,hataki watanzania weusi waushike uchumi wa Tanzania anataka wahindi ndio washike uchumi wa TZ.
 
Nimeamini kama watanzania wangekuwa wote JF Tanzania sasahivi ingebadilika kama Madagasca tukawaoondoa viongozi wasio waadilifu tukamweka mwadilifu hatakama ni kuli,tumechoka kuhujumiwa kwa kauli za hadaa et nguvu mpya,ari mpya na kasi mpya kumbe kibwagizo hiki kilikuwa cha EL alipoondaka tu sijaisikia tena.Hatutaki maneno ya uchumi wa TZ unapaa tunataka mifano halisi ya uchumi wa Watanzania kuanzia vijijini unakua na kila mtanzania anapata mahitaji yake muhimu ili aweze kuishi.
 
Kama kuna mtu amekuwa akufuatilia kwa makini uandishi na maoni ya Mhariri wa Tanzania daima, utagundua kuwa kwa siku za karibuni amekuwa akitetea sana Dowans na RA. Nahisi kilichombadirisha Zitto Kabwe ndicho kilichimgeuza Mhariri. Nimeamini hakuna kinachoweza kushindana na nguvu ya pesa. Mungu ibariki Tanzaniana watu wake
 
Back
Top Bottom