Victoire
JF-Expert Member
- Jul 4, 2008
- 24,146
- 56,610
kumbuka wazee wa RA walikuja kama wakoloni!so mjukuu anaendelenza lengo lililowaleta huku!Hivi babake Obama alienda lini USA? Watu waliohamia Tanzania 1852 Mtikila anawaona ni wageni?
kumbuka wazee wa RA walikuja kama wakoloni!so mjukuu anaendelenza lengo lililowaleta huku!Hivi babake Obama alienda lini USA? Watu waliohamia Tanzania 1852 Mtikila anawaona ni wageni?
Ukweli ni kuwa RA ni FISADI, period. Yes ni hard working, kwenye UFISADI.
Dr ni , well, mwana CCM ila yes na yeye amesema maneno ya KIKABURU, kwa hiyo na yeye ni KABURU na inabidi awithdraw hizo statement zake kama anataka kuchukuliwa kama serious leader.
Hizi siasa za KIKABURU za "uzawa", yes zitapata support kubwa kwani tunacheza na numbers, lakini hazisaidii nchi hata siku moja. Ukaburu mbaya kule Afrika Kusini na ni Mbaya hata leo kwa Tanzania yetu. Tukemee haya kwa nguvu zote, tusijidanganye hata siku moja!
mi nashangaa watu wanaompigia kura mtu ambaye hana hata uchungu na maisha yao. hivi RA wanampa kura za nini? hivi watu wa huko igunga wakoje? napenda siku moja niwaone.
kuhusu dowans, RA anajua hasara itakayopatikana asipouza ile mitambo, hivyo anang'ang'aniza kwa nguvu zake zote, akitumia magazeti na mitandao yake yote, ili alimradi apate kitu isiwe hasara kubwa kakwe. anatapatapa. Watanzania tusimpe nafasi, akitapatapa asijeinuka, tumbane palepale chini hasi atoe kamasi. moto wa mafisadi umeshawashwa. hata watu wakifa, upo mioyoni mwa watz wengi. kama hamuamini subirini kipindi cha uchaguzi mwakani mtaona,patawaka moto.
Spika inabidi aelewe kuwa wabunge wana haki zote za kiraia, na kama wanataka kuongelea mambo yao nje ya bunge wanaweza.
Spika hana wajibu wala mamlaka ya kuwashurutisha wabunge jinsi ya kuongea nje ya bunge, almuradi hawavunji kanuni za bunge.Nafahamu kuwa hawavunji.
Kama kuna watu wanaoweza kuwashurutisha wabunge hawa jinsi gani ya kuongea basi ni chama chao, CCM. CCM wameshafanya hivyo.
Chombo chochote kinachoingilia jinsi gani wabunge hawa wajieleze kinavunja misingi muhimu ya demokrasia, ikiwamo uhuru wa kujieleza.
Hata kama si yake ila ana connection au maslahi na ile mitambo!hujiulizi kwa nini magazeti yake yanatetea sana pia campuni hii ya Dowans kutumia aniani yake ya CAsPIAN. Richmond/downs!haihitaji kuwa Isaac Newton kujua kuwa RA ana uhusiano na Dowanskuna ushahidi kuwa ile mitambo yake? au?
Hata kama si yake ila ana connection au maslahi na ile mitambo!hujiulizi kwa nini magazeti yake yanatetea sana pia campuni hii ya Dowans kutumia aniani yake ya CAsPIAN. Richmond/downs!haihitaji kuwa Isaac Newton kujua kuwa RA ana uhusiano na Dowans
kumbuka wazee wa RA walikuja kama wakoloni!so mjukuu anaendelenza lengo lililowaleta huku!
Mimi nimesikiliza mahojiano ya Dr. Mwakyembe na waandishi wa habari kama ilivyowekwa hapa JF (Shukran Invisible kwa hilo). Katika mahojiano yote, sijasikia kauli yoyote ambayo Dr. Mwakyembe alisema inayomfanya awe kaburu.
Alichosema Dr. Mwakyembe (ambacho wala hakina mjadala, kwa kuwa ni kweli) ni kwamba mara nyingi taasisi zetu hapa nchini, hujali zaidi watu wa nje na kuwapa kipaumbele kuliko waTanzania wa kawaida. Alitoa mfano wa jinsi Bank zetu zinavyotoa mikopo kwa urahisi zaidi kwa wazungu, wahindi, waarabu n.k. na kuwapa shida sana waTanzania wengine wa kawaida kupata mikopo hiyo. Kwa mtazamo wangu ni kwamba, kauli kama hizi si za kibaguzi. Ubaguzi unatokana na kauli za kutaka watu wa rangi/jinsia/kabila/imani/itikadi au vinginevyo kupewa kipaumbele zaidi ya wengine. Dr. Mwakyembe angekuwa mbaguzi kama angesema ni vyema waTanzania wapewe kipaumbele zaidi ya watu wengine wasio na asili ya Tanzania (hakusema hivyo, bali alionyesha masikitiko yake kutokana na ubaguzi unaoonekana kuwepo dhidi ya waTanzania). Ubaguzi hauwezi kuwepo kwa kutoa malalamiko ya ubaguzi unaofanywa. Ubaguzi unakuwepo kwa kuanzisha ubaguzi usiokuwepo dhidi ya tabaka fulani.
Sidhani kama kuna mtu hapa anaeweza kukanusha ukweli kuwa imefikia kwamba kampuni za watu binafsi (waTanzania wa kawaida) kuamua kuajiri au kuuza share zao kwa watu wa nje ili tu waweze kupata sauti na attention inayohitajika katika maombi na mambo mengine wanayotaka kuyafanya ili kukuza biashara zao. Vingenevyo, biashara zao haziwezi kufika popote.
Hii ni kasumba iliyojengeka ndani ya fikra za waafrika wengi. Kasumba kuwa Mwafrika hawezi bila kusaidiwa na mtu mwingine wa nje ya Afrika kwa kuwa hajui au hana utaalamu au uaminifu unaotosha kupewa kipaumbele anachohitaji kuendesha shughuli zake.
Kuna habari kwamba Mtikila na leo atazungumza na waandishi wa habari kuzungumzia kuwasema wengine na huenda akawasema wale wanaopingana na Rostam kwa maana leo huenda akamsaidia Rostam. Huyo ndiye Mtikila, hebu tusubiri
Recta,
Kauli inayosemwa ilikuwa ya kibaguzi ni ile ya "wengine wana passport tatu tatu, sisi ni wazawa/wazalendo hatuna kwa kwenda na tutafia hapa hapa" Sija quote exactly ila ilikuwa karibu na hiyo.
Hivi Dr. Hayajui ya Ballali? Mweusi mwenzetu yule na katuibia na kuishia visiwani huko.
Hayajui ya Chenge, mweusi mwenzetu huyo na visenti vyake kwenye visiwa.
Sidhani kama Dr. ana ushahidi kwamba Rostam ana passports tatu, kilikuwa kijembe cha kisiasa ambacho kinalenga kwenye ubaguzi.
alikuwa na hoja nzuri sana katika kujitetetea kuhusu yeye kuwa ni shareholder wa ile kampuni ya umeme, lakini aliharibu kabisa ladha ya hotuba yake alipoanza kuingiza mambo ya uzalendo na kujiona yeye, kwa kuwa ni mweusi na kazaliwa Mbeya, kwamba ni mtanzania wa maana zaidi kuliko wengine, supposingly wale wenye asili ya asia. This was rubbish and it completely killed his good message.
lakini aliharibu kabisa ladha ya hotuba yake alipoanza kuingiza mambo ya uzalendo na kujiona yeye, kwa kuwa ni mweusi na kazaliwa Mbeya, kwamba ni mtanzania wa maana zaidi kuliko wengine, supposingly wale wenye asili ya asia. This was rubbish and it completely killed his good message.
Hivi babake Obama alienda lini USA? Watu waliohamia Tanzania 1852 Mtikila anawaona ni wageni?
Mtikila ni call box, akija Mangugu akaweka coin itasema, akija Panjun akaweka rupia ataimba, akaja Kunguru akaweka noti, atatukana, akaja Mwangananga akaweka fedha ataimba kwaya na kadhalika. Alitumika mwaka 1995, 2000, 2005 na sasa anarudi tena. Enyi Wadanganyika SAA YA UKOMBOZI NI SASA!!!!!!
...shutuma nyingi tunazomrushia ni za kisiasa tu badala ya kisheria.
- Sasa ifike mahali tutafute hoja nzito za kisheria meaning legal facts za kumbana....
Wito wangu kwa viongozi wetu wa sisi wanyonge huku upande wa pili, please mjitayarishe na muwe makini, tafuteni ushauri wa nje ya ma-box yenu, wachujeni kwa makini mnaojihusisha nao, tafuteni ukweli wa kisheria against adui kwa sababu huyu adui sio lelemama....... Msisahau kwamba siasa bado ni mchezo mchafu sana unaowezwa kuchezwa vizuri zaidi na wanasiasa wachafu....