Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Anayeshindana na Chadema ajue anashindana na nguvu za Mungu!
Siku zote Mungu hajawahi kushindwa na msukule
 
Wakuu,taarifa za kusikitisha ni kwamba Mkutano wa Dr.slaa umevunjika Kasulu,amepigwa mawee na vijana wasiojulikana akiwa Jukwaani,Polisi wanapiga mabomu ya Machozi Muda huu kutawanya watu,haijulikani Slaa ameumizwa kiasi gani lakini polisi wamewahi kumuokoa na kumtorosha kusikojulikana.
hali ni tete wakuu,naomba Munipe muda wa kuwawekea Picha hapa.
Pia awali Mkutano ukiwa unaendelea,Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa CHADEMA alitangaza kuwa Matamko na mambo mengine yote ya kumtibulia Dr.slaa yanaratibiwa na Kijana Habib Mchange na Diwani mmoja wa Mwanza(Hakutaja jina).

MODS naamini mnawatu KASULU,wapigieni simu MUDA huu,Mpigieni Tumaini Makene mjue Ukweli huu.naomba muiache Post watu wachangie
​

Usiwe unasema vitu ambavyo huna uhakika navyo. Slaa hajapigwa mawe, hajatoroshwa na polisi. Nilikuwepo uwanjani, mawe yalikuwa yanarushwa na waliokuwa na mabango, wengi wao ni wafuasi wa ccm kwani wanaonekana kwenye vikao na mikutano ya ccm hapa wilayani wakiwa wamevaa safe ya ccm. Wengine ni watumishi wa serikali wanafahamika. Slaa alipoondoka alionekana na mawe yaliendelea kurushwa. Andikeni vitu vya ukweli. Kuna polisi kapigwa jiwe kidevuni na mkononi anavuja damu
 
Nimekumbuka ubeti wa Marehem Bi. Kidude; "usitukane wakunga na uzazi ungalipo"!

Leo nakuuliza Dr.W.Slaa, kiko wapi? si hao hao ndio pilisisiem?
 
Last edited by a moderator:
Habari ni za kweli kapigwa mawe inasadikika kw vijana walikuwa wafuasi wa ccm au waliandaliwa na ccm kwani wkt mawe yanatupwa polisi hawachukua hatua mpaka baadae walipoamua kupiga mabomu ya machozi.
Mtaweweseka sana na CCM. ukweli ni kuwa Dr Slaa ni adui wa wanakigoma kutokana na kusimamia Zitto kuonyofolewa Vyeo vyake
 
Kama kweli Dr. Slaa hapendi vurugu, basi aahirishe mkutano uliopangwa kufanyika Mwandiga - nyumbani kwa akina Zitto

Itakuwa ni ujuha na kiburi cha ajabu kwenda huko. Nina uhakika anaweza kuhisi nini kitatokea baada ya matukio ya Kasulu mjini. Kama hujui kusoma, hata picha huelewi??
 
Chadema hakifugi wahsaliti, na nina kuhakikishia wote watangoka....

mlimtuma SLAA kuja kutest zari Kigoma na Kahama ilikuwa zuga tu-kwasababu mnajua SLAA KIGOMA alipata 40% wakat KLMNR alipata 5% hivyo msingependa kuipoteza Kigoma-sasa ujumbe wetu ni huo NO ZITTO =NO CHADEMA KIGOMA
 
Wanajamvu na Mods,

Habari hii imetiwa chumvi zaidi nakuwa ni UONGO mkubwa,

Mkutano haukuvunjika kama huyu masalia anavyowadanganya,

Mkutano umeisha salama kabisa kama ilivyo mikutano ya vituo vingine kwenye ziara hii,

Mods ili mjiridhishe mpigieni simu Dr Slaa awape ukweli huenda ndio mtaamini,
 
Upo usemi usemao usitukane mkunga na uzazi ungalipo. Leo doctor Slaa ameponea mikononi mwa polisi ambao mara zote amekuwa akiwa kejeli kwa maneno yake ya dharau, amelazimika kuahirisha mkutano under polisi escorts. Pole babu ubishi ni utumwa utamuacha Mashumbushi wako kwa ujeuri wako.
 
Habari ni za kweli kapigwa mawe inasadikika kw vijana walikuwa wafuasi wa ccm au waliandaliwa na ccm kwani wkt mawe yanatupwa polisi hawachukua hatua mpaka baadae walipoamua kupiga mabomu ya machozi.

So wakati vijana wa CCM walipokuwa wanampiga mawe,wafuasi wa Chadema nao wakawa kimya tu wakishuhudia mawe yakirushwa?something is wrong somewhere..
 
Huyu Slaa ni mtu gani asiyesoma alama za nyakati? Mi nadhani hawa chadema hasa hawa viongoxi 2 wa juu akili zao ni kama za zero. Watu kama haw ndo waongoze tz yani mbw naye awe pale ikulu? Kweli nyie wa tz mnaona kuna mtu mle, raisi kwa chadema sacosi hamna. Kea sasa wamebaki wenye akili zisizo na uwexo yani nishida ndani ya Sacosi.

Unasubiliwa pale kisuma kafanye kazi yako, siasa waachie wenyewe
 
Ziara za Dr. Slaa huko Kahama na Kigoma ziliwahishwa sana. Wangesubiri mpaka maamuzi ya hatima ya hao walioambiwa wajieleze...

Tulijadili wiki iliyopita kuhusu safari hii, na tulio wengi tulisema si vema kwa sasa, na pengine viongozi kitaifa wangebaki kwanza na shughuli za kitaifa maifisini na hawa wa kanda wafanye hiyo mikutano.

Viongozi wa Chadema lisemwalo lipo, kwamba pengine ushupavu unaweza kusababisha matukio kama haya, kudharau tahadhari za kiintelijensia si mwafaka katika masuala ya ushindani wa kisiasa.

Baada ya tukio la kuwaondoka katika uongozi baadhi ya viongozi wa Chadema kitaifa kisha uongozi wa kitaifa kutembelea maeneo ambayo ni ya waathirika ni mapema mno kama ulivyosema.

Viongozi Chadema jaribuni kuwa wasikivu kwa ushauri mzuri mnaupewa, binafsi nilikuwa nashangazwa na msafara huu wa Dr. Slaa kwenda Kigoma kwa kipindi hiki wakati bado kesi ingalipo na hali haijatulia.

Kujiamini mno wakati mwingine huweza kusababisha mitafaruku na matukio kama haya.
 
Mkutano umeisha salama licha ya jaribio la vijana wenye mabamgo kutaka kuvuruga,

Polisi walitaka kutumia nguvu kuwakamata vijana hao lakini Dr Slaa akawaomba wawache na wasogeebele watoe madukuduku yao,

Hakuna uvunjifu wa mkutano, umeisha salama kabisa!

teh teh teh teh kesho wapi??
 
Alikuwa anapima kina cha bahari kwa ujiti. Alitaka kujiamini watu wanamkubali na kuamua kuanzia kulekule ambako walisema asifike. Aendelee na ziara yake kama anaona bado anakubalika.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
"Usitukane wakunga uzazi ungalipo". Bi kidude.

Dr slaa ona police leo ndio wamekuokoa.
 
Usiwe unasema vitu ambavyo huna uhakika navyo. Slaa hajapigwa mawe, hajatoroshwa na polisi. Nilikuwepo uwanjani, mawe yalikuwa yanarushwa na waliokuwa na mabango, wengi wao ni wafuasi wa ccm kwani wanaonekana kwenye vikao na mikutano ya ccm hapa wilayani wakiwa wamevaa safe ya ccm. Wengine ni watumishi wa serikali wanafahamika. Slaa alipoondoka alionekana na mawe yaliendelea kurushwa. Andikeni vitu vya ukweli. Kuna polisi kapigwa jiwe kidevuni na mkononi anavuja damu
Mkuu bado zamu yako kuchapwa siasa za kilaghai haya ndiyo madhara yake nabado mtagongwa sana mawe acheni demokrasia ichukue nafasi yake.
 
Back
Top Bottom