mwanza_kwetu
JF-Expert Member
- Mar 2, 2011
- 693
- 182
Yerico pls confirm this
Acha kuficha aibu wewe. Utarukaruka sana lakini ukweli ni kuwa babu kapopolewa na mawe. Hii yote ameponzwa na tamaa ya posho. Alishatahadhalishwa lakini hakusikia. Watu walio eneo la tukio wanathibitisha wakati wewe ulie Dar unajifanya kukanusha. dr Slaa hata kama atapigiwa simu bado ataendelea kukataa tu wakati ana ngeu machoniWanajamvu na Mods,
Habari hii imetiwa chumvi zaidi nakuwa ni UONGO mkubwa,
Mkutano haukuvunjika kama huyu masalia anavyowadanganya,
Mkutano umeisha salama kabisa kama ilivyo mikutano ya vituo vingine kwenye ziara hii,
Mods ili mjiridhishe mpigieni simu Dr Slaa awape ukweli huenda ndio mtaamini,
Tulijadili wiki iliyopita kuhusu safari hii, na tulio wengi tulisema si vema kwa sasa, na pengine viongozi kitaifa wangebaki kwanza na shughuli za kitaifa maifisini na hawa wa kanda wafanye hiyo mikutano.
Viongozi wa Chadema lisemwalo lipo, kwamba pengine ushupavu unaweza kusababisha matukio kama haya, kudharau tahadhari za kiintelijensia si mwafaka katika masuala ya ushindani wa kisiasa.
Baada ya tukio la kuwaondoka katika uongozi baadhi ya viongozi wa Chadema kitaifa kisha uongozi wa kitaifa kutembelea maeneo ambayo ni ya waathirika ni mapema mno kama ulivyosema.
Viongozi Chadema jaribuni kuwa wasikivu kwa ushauri mzuri mnaupewa, binafsi nilikuwa nashangazwa na msafara huu wa Dr. Slaa kwenda Kigoma kwa kipindi hiki wakati bado kesi ingalipo na hali haijatulia.
Kujiamini mno wakati mwingine huweza kusababisha mitafaruku na matukio kama haya.
acha kejeli basi
hebu uangalie upinzani kwa jicho la tatu kwa sababu ili nchi iendelee tunawahitaji sana watu hawa
Mkutano Umemalizika Salama Tu Nimeongea Na Makene,
Mkuu, huyu babu ametolewa kafara na akina Mbowe. Kwao kupigwa mawe ni ushujaa eti wanapoza makali ya Zito. Hakika hawa viongozi ni wa ajabu sanaKama kweli Dr. Slaa hapendi vurugu, basi aahirishe mkutano uliopangwa kufanyika Mwandiga - nyumbani kwa akina Zitto
Itakuwa ni ujuha na kiburi cha ajabu kwenda huko. Nina uhakika anaweza kuhisi nini kitatokea baada ya matukio ya Kasulu mjini. Kama hujui kusoma, hata picha huelewi??
Upo usemi usemao usitukane mkunga na uzazi ungalipo. Leo doctor Slaa ameponea mikononi mwa polisi ambao mara zote amekuwa akiwa kejeli kwa maneno yake ya dharau, amelazimika kuahirisha mkutano under polisi escorts. Pole babu ubishi ni utumwa utamuacha Mashumbushi wako kwa ujeuri wako.
Nani atamchagua huyu kikongwe?
"Usitukane wakunga uzazi ungalipo". Bi kidude.
Dr slaa ona police leo ndio wamekuokoa.